Mr Beast
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 311
- 435
- Thread starter
- #101
"...hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Tanzania kama sio Kahama tena hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa miradi ya maendeleo kwa Fedha za ndani kama sio Kahama au hebu nitajie Wilaya moja inayoitwa Mkoa wa Kikodi hapa Tanzania kama sio Kahama."
1. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilikusanya Tshs billioni 32 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.
Bado kuna Halmashauri za Manispaa za Temeke na Kinondoni ambazo zilikusanya mapato kuizidi Manispaa ya Ubungo. Kwa hiyo Kahama bado ni mtoto tu kwenye kundi la Manispaa.
Halafu kuhusu ushindani wa makausanyo ya mapato, TAMISEMI wameweka Halmashauri katika makundi: Kuna Miji Midogo, Miji, Manispaa, Wilaya, na Majiji. Kahama ipo kundi la Manispaa, hata hivyo haiwezi kushika namba moja.
2. Kuhusu Wilaya ya Kahama kuwa Mkoa wa Kikodi pekee. Tarafa ya Kariakoo iliyopo Wilaya ya Ilala ni Mkoa wa Kikodi; Tarafa ya Mbagala iliyopo Wilaya ya Temeke ni Mkoa wa Kikodi. Mifano ipo mingi. Kwa hiyo siyo kweli.
3. Halmashauri ya Manispaa ya Kahama haikupandishwa hadhi kutoka Halmashauri ya Wilaya na kuwa Halmashauri ya Manispaa. Isipokuwa, Halmashauri ya Mji wa Kahama ndiyo uliopandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Wilaya ya Kahama ina Majimbo matatu: Kahama Mjini, Ushetu na Msalala. Jimbo la Kahama Mjini ndilo linabeba eneo lote la Manispaa ya Kahama.
Majimbo ya Ushetu na Msalala yana Halmashauri yake ya Wilaya( sikumbuki jina)
4. Ukisema kuna Halmashauri zinakuja Kahama kujifunza basi ni hivi, Kahama wenyewe madiwani walienda Manispaa ya Ubungo kujifunza namna ya kukusanya mapato haswa ya Stendi. Halmashauri nyingine zilizoenda Ubungo ni Mwanza Jiji, Ilemela MC, Tanga Jiji, na wengine wa kule Zanzibar. Hata Arusha Jiji walienda Ubungo.
5. Halmashauri zote nchini zenye mapato makubwa zikeruhusiwa na TAMISEMI kutumia sehemu ya mapato yake kufanya miradi ya maendeleo. Sasa hata kama Kahama inatumia sehemu ya mapato katika miradi ya ndani, haiwezi kuzizidi Halmashauri kama Temeke, Kinondoni na Jiji la Dar es Salaam zenye mapato mengi kuishinda Kahama.View attachment 2886962
Kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Kahama Manispaa ilijiwekea lengo la kukusanya bilioni 10.25 za Kitanzania wakati Manispaa ya Ubungo ilikusanya bilioni 32 za Kitanzania.
MADIWANI UBUNGO WAWASILI HALMASHAURI YA MINISPAA YA KAHAMA
- Leo Oktoba 31, 2022 Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Ubungo pamoja na wataalamu wa idara mbalimbali leo wameanza ziara katika Halmashauri ya Manispaa Kahama - Ziara hiyo ni ya kujifunza juu ya masuala makuu mawili ikiwa ni suala la ukusanyaji bora zaidi wa mapato ya Halmashauri pamoja n