Pre GE2025 Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Pre GE2025 Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndivyo alivyowaambia Wananchi kwamba anakwenda kumshughulikia kwa nafasi yake nimeangalia ile Crip YUTUBE
Sasa unamfukuza mtu anayetunza maeneo ya Umma ili kesho mje mjenge shule, zahanati, Solo etc

Huu utakuwa ni ujinga wa kiwango cha lami
 
Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya....

Distinction without a difference

Point is, Kahama stands out in developmental statistics strictly because of massive mining industry. Simple as. Si kwa sababu ya bureaucrats Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Hebu tuambie kuhusu Geita
 
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga na kulitetea Taifa letu na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili.

Mhe Paul Makonda, Majuzi wakati ukiwa hapa Kahama kuna jambo lilinishtua na roho ikaumia sana wakati unalazimisha yule dada Caroline apewe eneo ambalo ni mali halali ya Serikali (Umma).

Mhe Paul Makonda, Nilishangaa zaidi kuona kwanini hawa watu wabaya watumie jukwaa lako kutengeneza Uongo na kutaka kuiba mali za umma zilizopo kihalali huku wakikuhusisha wewe katika nia zao hizo ovu?

Mhe Paul Makonda, yule mama Caroline aliyekuwa anakulilia kisanii pale viwanjani Mimi namfahamu na mgogoro wake pia naufahamu vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho ulidanganywa.

Mhe Paul Makonda, Nafahamu Mama huyu tangu alivyoshindwa kesi katika mahakama ya Wilaya ya Ardhi Kahama na baadae akakata rufaa Mahakama kuu Shinyanga mahakama zote hizi zilitamka kuwa lile ni eneo la Serikali (umma).

Mhe Paul Makonda, Kama utataka kujiridhisha zaidi mwambie akuletee uamuzi wa mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga kama alivyodai mbele ya umma kuwa ameshinda kesi.

Mhe Paul Makonda, Ukweli kuhusu madai ya Caroline unaweza pia kuwauliza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Sophia Mjema au aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha ambae Sasa ndio Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu hawa wote wanamfahamu Caroline na eneo pia wanalifahamu watakupa ukweli wote.

Mhe Paul Makonda, najiuliza kwanini mtu atake kuchukua eneo la Umma na wewe bila kujali Wala kudadisi kwa kina unataka kumpa sapoti achukue mali ya Serikali (umma) kwani huoni kama kwa kufanya hivyo unachochea mgogoro zaidi?

Mhe Paul Makonda, Nataka nikueleze kuwa Kahama tunamkurugenzi ambae kwanza hanunuliki lakini pili ni mtu mwadilifu na anauchungu na mali za Serikali ndio maana unaona hataki janja janja hizi za watu kupora mali za umma.

Mhe Paul Makonda, Wilaya ya Kahama imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka na Watanzania wanalijua hili ukilinganisha na Halmashauri nyingine zote hapa Tanzania bara na hata huko Visiwani.

Mhe Paul Makonda, kama Kuna sababu tatu kubwa za Kahama kuwa hivi ilivyo Leo basi moja ni uwepo wa huyu mkurugenzi mwadilifu na ndio sababu Halmashauri zote Tanzania wanakuja kujifunza hapa Kahama " Mkurugenzi huyu ni shamba darasa kitaifa "

Mhe Paul Makonda, Mkurugenzi huyu kaitoa Kahama kwenye Halmashauri ya Wilaya hadi leo ni "Municipal council" Waswahili tunasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe ukweli ni kwamba binadamu wote tunayo madhaifu ila huyu anajitahidi sana kuyapunguza.

Mhe Paul Makonda, Najua unajua mtu anayefañya kazi vizuri wakati wote hapendwi hasa na majizi na wapigadili, Ukweli mchungu huyu jamaa sio mwizi Wala mlarushwa TAMISEMI wanajua hivyo na ndivyo ilivyo.

Mhe Paul Makonda, hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Tanzania kama sio Kahama tena hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa miradi ya maendeleo kwa Fedha za ndani kama sio Kahama au hebu nitajie Wilaya moja inayoitwa Mkoa wa Kikodi hapa Tanzania kama sio Kahama.

Mhe Paul Makonda, Tunapopata vijana waadilifu na Waaminifu kama hawa lazima tuwapongeze na kuwatia moyo nasio kuwakemea na kuwadhalilisha mbele ya halaiki bila kujali kazi kubwa wanayoifanyia nchi yetu.

Mwisho, Tupelekee salamu zetu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwambie kura zake za mwaka 2025 Kahama zimetimia hata kama Uchaguzi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.

Ni mimi Mabula Malunde Sitta.
Kama ni ridhaa yangu huyu anakuwa Mkurugenzi mpaka anastaafu
 
Kwani Tarime hakuna mining, Geita Je? Don't be bias
Angalia na ukubwa wa mining wewe, Kahama kumejaa watu kwa ajili ya machimbo ya dhahabu, kuanzia wachimbaji wadogo mpaka wakubwa, huko Geita, Tarime, hakuna kiasi kikubwa kama kilichopo Kahama,
 
Angalia na ukubwa wa mining wewe, Kahama kumejaa watu kwa ajili ya machimbo ya dhahabu, kuanzia wachimbaji wadogo mpaka wakubwa, huko Geita, Tarime, hakuna kiasi kikubwa kama kilichopo Kahama,
Kahama Buzwagi ilishafungwa
 
Huyo Mkurugenzi au Afisa wa serikali atakayetekeleza maelekezo ya Makonda bila baraka za waziri au katibu mkuu wake atakua hajui Utumishi wa umma , Makonda is no body kwenye ranking ya Utumishi wa umma yeye anaongea tu .
 
Back
Top Bottom