Pre GE2025 Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Pre GE2025 Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mhe Paul Makonda, Nataka nikueleze kuwa Kahama tunamkurugenzi ambae kwanza hanunuliki lakini pili ni mtu mwadilifu na anauchungu na mali za Serikali ndio maana unaona hataki janja janja hizi za watu kupora mali za umma.
Promo
 
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga Taifa na zi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.

Ni Mimi Mabula Malunde Sitta.
Mkurugenzi anahujumu mapato aondoke
 
Mbona unauliza nisicho kisema?

Mkuu hukunisoma. Miye nimekazia tu.

1. Huyo ni wa ndinga la 400m +
2. Barabara Kahama kwa halmashauri zote likely ni poorest.
3. Huyu bwana asemekana ni long serving mkurugenzi tangu enzi za JK.
4. Raia wa Taifa ananitaka kufika kujionea, nalikuwa huko juzi.
 
Sawa,

1. Kwani ndinga lile ni mali ya nani?

2. Long service inayoleta matokeo kama haya ubaya wake ni Upi?

3. Huyu ni Mkurugenzi wa Kahama Mji hizo Halmashauri zingine zinawakurugenzi wake

4. Barabara mjini ni nzuri binafsi sipendi Uchawa ila ukweli huyu bwana apewe maua yake
 
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga Taifa na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili.

Mhe Paul Makonda, Majuzi wakati ukiwa hapa Kahama kuna jambo lilinishtua na roho ikaniuma sana wakati unalazimisha yule dada Caroline apewe eneo ambalo ni mali halali ya Serikali (Umma)

Mhe Paul Makonda, Nilishangaa zaidi kwanini hawa watu wabaya watumie jukwaa lako kutengeneza Uongo na kutaka kuiba mali za umma zilizopo kihalali tena wakikuhusisha mpaka wewe katika nia zao hizo ovu!!?

Mhe Paul Makonda, yule mama Caroline aliyekuwa anakulilia pale viwanjani Mimi namfahamu na mgogoro wake kuanzia mwanzo mpaka mwisho naufahamu pia wote.

Mhe Paul Makonda, Mama huyu tangu alivyoshindwa kesi katika mahakama ya Wilaya ya Ardhi Kahama na baadae akakata rufaa Mahakama kuu Shinyanga mahakama zote hizi zilitamka kuwa lile ni eneo la Serikali (umma ) kama utataka kujiridhisha zaidi mwambie akuletee uamuzi wa mahàkama kuu Kanda ya. Shinyanga kama alivyodai mbele ya umma kuwa ameshinda kesi.

Mhe Paul Makonda, Ukweli kuhusu madai ya Caroline unaweza pia kuwauliza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Sophia Mjema au aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha ambae Sasa ndio Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu hawa wote wanamfahamu Caroline na eneo pia wanalifahamu watakupa ukweli wote.

Mhe Paul Makonda, najiuliza kwanini mtu atake kuchukua eneo la Umma na wewe bila kujali Wala kudadisi kwa kina unataka kumpa sapoti achukue mali ya Serikali (umma) kwani huoni kama kwa kufanya hivyo unachochea mgogoro zaidi?

Mhe Paul Makonda, Nataka nikueleze kuwa Kahama tunamkurugenzi ambae kwanza hanunuliki lakini pili ni mtu mwadilifu na anauchungu na mali za Serikali ndio maana unaona hataki janja janja hizi za watu kupora mali za umma.

Mhe Paul Makonda, Wilaya ya Kahama imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka na Watanzania wanalijua hili ukilinganisha na Halmashauri nyingine zote hapa Tanzania bara na hata huko Visiwani.

Mhe Paul Makonda, kama Kuna sababu tatu kubwa za Kahama kuwa hivi ilivyo Leo basi moja ni uwepo wa huyu mkurugenzi mwadilifu na ndio sababu Halmashauri zote Tanzania wanakuja kujifunza hapa Kahama ( Mkurugenzi huyu ni shamba darasa kitaifa )

Mhe Paul Makonda, Mkurugenzi huyu kaitoa Kahama kwenye Halmashauri ya Wilaya hadi leo ni "Municipal council" Waswahili tunasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe ukweli ni kwamba binadamu wote tunayomadhaifu ila huyu anajitahidi sana.

Mhe Paul Makonda, Najua unajua mtu anayefañya kazi vizuri wakati wote hapendwi hasa na majizi na wapigadili, Ukweli mchungu huyu jamaa sio mwizi Wala mlarushwa TAMISEMI wanajua hivyo na ndivyo ilivyo.

Mhe Paul Makonda, hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Tanzania kama sio Kahama tena hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa miradi ya maendeleo kwa Fedha za ndani kama sio Kahama au hebu nitajie Wilaya moja inayoitwa Mkoa wa Kikodi hapa Tanzania kama sio Kahama.

Mhe Paul Makonda, Tunapopata vijana waadilifu na Waaminifu kama hawa lazima tuwapongeze na kuwatia moyo nasio kuwakemea na kuwadhalilisha mbele ya halaiki bila kujali kazi kubwa wanayoifanyia nchi yetu.

Mwisho, Tupelekee salamu zetu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwambie kura zake za mwaka 2025 Kahama zimetimia hata kama Uchaguzi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.

Ni Mimi Mabula Malunde Sitta.
Wewe ni kilaza, chawa, muoga, kinyamsisi n.k mtu smart hawezi akawa anarudia rudia mheshimiwa makonda kila sehemu. Umetumwa na nani?
 
Sawa,

1. Kwani ndinga lile ni mali ya nani?

2. Long service inayoleta matokeo kama haya ubaya wake ni Upi?

3. Huyu ni Mkurugenzi wa Kahama Mji hizo Halmashauri zingine zinawakurugenzi wake

4. Barabara mjini ni nzuri binafsi sipendi Uchawa ila ukweli huyu bwana apewe maua yake

1. Vyema umekubaliana nami katika hoja zote isipokuwa barabara:

Ubovu wa barabara Kahama

2. Ninakazia Kahama barabara ni mbaya mno na mji umedumaa.

3. Kusema kilichopo so uchawa; kwani wewe ni chawa wake?
 
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga Taifa na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili.
uzi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.

Ni Mimi Mabula Malunde Sitta.
Tunampongeza ajirahidi Kahama iwe Mkoa kisha Jiji hata kama atafia hapa sisi tunataka maendeleo tu
 
Sawa,

1. Kwani ndinga lile ni mali ya nani?

2. Long service inayoleta matokeo kama haya ubaya wake ni Upi?

3. Huyu ni Mkurugenzi wa Kahama Mji hizo Halmashauri zingine zinawakurugenzi wake

4. Barabara mjini ni nzuri binafsi sipendi Uchawa ila ukweli huyu bwana apewe maua yake
TUkianzia ktk ajira tu tutaona mapungufu, tukienda ktk mapato na matumizi tutamkataa mapema
 
Haraka haraka kwenye mada,

Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga Taifa na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili.
Baada ya kufanya investigation nimetaarifiwa Mbunge alitengeneza watu ila wamkatae Mkurugenzi kisa Mbunge anataka Mkurugenzi nae awe Msukuma na hamtaki kabisa Mkurugenzi, nawewe endelea kufanya utafiti wako

OVA:
 
Back
Top Bottom