Kahama VS Njombe/Mafinga

acha porojo msingekuwa mnaongoza kwa umaskini..kama mji wote ni dhahabu mnasubiri nini kugeuza vibanda vyenu migodi badala yake mnagombania na wazungu michanga huko?
 
Mikoa kame! Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, Mara ni mikoa kame?! Labda shinyanga kidogo ndo Kuna kaukame, 🤣🤣🤣wewe utakuwa ulienda Dodoma si bure
 
Mkuu jaribu kuwa specific kanda ya ziwa ni kubwa na ina aina tofauti ya maisha kwa maeneo tofauti
 
Amen.

Hilo ni jiji la mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Millions of watu wamerundikana hapa mjini ili kujikimu simply mengi ya maeneo ya kanda ya ziwa yaliyosalia sio liveabe,ukame wa mara kwa mara na njaa ..Kanda hii,Kati na Pwani ndio mnaongoza kwa umaskini na kuishi kwenye tembe.Ndio maana si ajabu kukuta Miji michache sana imeendelea na maeneo mengi ni hovyo kabisa
Hali kama hii huwezi ikuta Nyanda za juu Kusini,,Kuanzia Ilula hadi Tunduma,all the way to Sumbawanga ni miji na vijiji vilivyoendelea..Kuanzia Makambako hadi Songea to mbamba bay huwezi kuta tembe na waganga njaa wanaozurura na kulundikana miji michache kama kanda ya ziwa
 
Mkuu jaribu kuwa specific kanda ya ziwa ni kubwa na ina aina tofauti ya maisha kwa maeneo tofauti
Shinyanga,simiyu,Mara isipokuwa Tarime na Musoma mjini,Mwanza yote kasoro mjini,Geita huko..Hapo naikubali kagera tuu maana ni green the whole year kama tu huku Nyanda za Juu Kusini
 
Mikoa kame! Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, Mara ni mikoa kame?! Labda shinyanga kidogo ndo Kuna kaukame, 🤣🤣🤣wewe utakuwa ulienda Dodoma si bure
Kwenye hiyo orodha toa Kagera tuu,the rest ni pata potea,kunyesha kukauka..Nimeishi mwanza mara kadhaa mvua zinanyesha watu wakipanda zinakata njiani wakati mimea bado kukomaa sio kwamba hazinyeshi kabisa..Hali kama hiyo huwezi ikuta Nyanda za juu kusini
Hata mwaka huu mvua zimenyesha sana nchi nzima lakini kutokana na mazingira yenu ya tambarare kuna mafuriko kila kona huko kwenu tofauti na kusini ambako maji yana mikondo yake ya mabonde hatujapata hizo shida kama kwenu huko na ukanda wa Pwani..Huko ni maeneo hovyo kabisa ya Kuishi
 
Kuna miji watu wanaichukukia Poa sana, mtu akipita tu akiwa safari tayari huo mji anaujua sana.
Kahama ni Mji uliochangamka sana na Njombe ni Mji uliojengeka vizuri hata ukubwa.
Kahama fananisha na Mnafunga na Makambako japo Kahama Wapo juu kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha juu zaid,i kupita na kukuta watu wanakimbizana tu barbarani kama gulioni ndio hicho tuu kinafanya watu waone kahama iko vizuri,mara utasikia usiku kama mchana na blaa blaa kibao za hivyo lakini kwenye kila aspect Kahama ni hovyo sana kulinganisha na Njombe
Miji sampuli ya Kahama ni Tunduma,Masasi,Ifakara,Mbinga,Makambako,Kibaigwa nk Mafina itoe hapo.Miji hiyo nimetaja .iko busy kama uko gulioni au mnadani ,no order lakini ni hovyo kabisa kwenye kila nyanja ipo kwa ajili ya kuchuma pesa tuu,but Njombe imejengeka na imesambaa sana..Ni makao makuu ya dayosisi 3 za makanisa wa RC,KKKT,Sabato na Taasisi mengine kibao..Ndio maana ukichukua hata aerial view ya Njombe ni nzuri kuliko Kahama.Kila mara nauliza kama Njombe haipiti Kahama kwa nini kuwe na mahotel na magorofa makubwa makubwa kuliko Kahama?
 
Mimi mwenyewe sijalinganisha ila nasema kanda ya ziwa sio pakame labda kama hujui maana ya ukame, kusini kunamvua nyingi kuliko kanda ya ziwa ila kanda ya ziwa sio pakame, hiyo misimu ya shidashida hujitokeza mara moja moja yaani ni kama huko kwenu imetokea mvua zimezidi sana, tarime, Serengeti, ngara, sengerema, geita, nk kote huko watu wanalima na kuvuna.
 
Sorry kanda ya ziwa ni kubwa mno.

Kuna Kagera(bukoba) ,Geita ,mwanza,mara,NK


Unaposema bukoba pakame wakati ndo wilaya inayoongoza Kwa mvua tz unashangaza.halafu unasema nyumba za tembe .sijui kama ulishawahi ona vijiji vya wahaya? Huko bukoba au muleba Kagera.


Mfano tu huko bukoba vijijin.

Hapa ni kijiji cha kabulala kata ya buganguzi wilaya ya muleba Kagera kanda ya ziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhan kama ulishawahi kutembelea uhayan huko bukoba Kanda ya ziwa. Mpaka huon aibu kuandika haya.

Nyumba unazoziona mbezi beach sijui mikocheni ndo zimejaa huko bukoba migombani.
Kwa Tanzania kidogo watu wa Kilimanjaro ndo wanaweza kuongea Kwa kujilinganisha na bukoba Kwa vijijin upande wa makazi na huduma za kijamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameshaitoa kagera kwenye list na mim mwanzon nilishangaa alipo-generalize
 
Hahaha ameshaitoa bukoba nadhan yeye alitaka kusema kwa wasukuma but akashindwa kuwa specific akataja kanda ya ziwa ambayo kiukweli ni kubwa na weather ni tofauti
Kiukwel kanda ya shinyanga ni kame na bado ni wavivu wa kujenga lakin huku vijijin bukoba watu wanajenga aisee
 
Acha kukurupuka,nilisha exclude mkoa wa Kagera ila huko kwingine ni matopeni tuu
 
Acha kiherehere mkurupuko,nilisha exclude mkoa wa Kagera in general ila the rest ni matopeni tuu
 
Huko kote ni semi arid,mvua kiduchi na zisizo na uhakika..nimetoa mfano unaweza lima msimu wa mvua za vuli huwa zunaanza wa tisa by february au january zinakata mazima wakati mazao bado,ko huwa kuna maisha ya kubahatisha sana kwenye kilimo tofautti na Nyanda za juu kusini,haijawahi tokea mvua kufeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…