Kahama VS Njombe/Mafinga

Huku kuna mvua za kistaarabu sio mvua za kipuuzi za kusini ambazo hazina pozi, Wakenya wanakuja kila mwaka hapa mabatini kusomba mchele unafikiri unatokea wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kuna mvua za kistaarabu sio mvua za kipuuzi za kusini ambazo hazina pozi, Wakenya wanakuja kila mwaka hapa mabatini kusomba mchele unafikiri unatokea wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Za kistaarabu ndio hizo mumeogelea kwenye mafuriko mwaka huu kama vyura.Umesikia wapi Nyanda za juu huku kuna mafuriko? Huku kuna mabonde ambayo ni mikondo ya maji ya asili na hatujengi mabondeni au tambarare kama huko kwenu
Mvua za ustaarabu ndio hizo zinawatia njaa na ukame kila mwaka,vueni tu samaki mle na chimbeni dhahabu mkaange mkuu itawatoa
 
Ogopa wilaya inayo-shindanishwa na baaz ya mikoa...

Najua unajua nazungumzia wilaya gan

...
Tunashindanisha miji ya Njombe/Mafinga vs Kahama na sio mkoa.Kimkoa tayari mkoa wa Njobe ni mikoa top 5 iliyoendelea na yenye watu wenye pesa na maisha mazuri kuliko huko machimboni kanda ya ziwa
 
kahama ni big business hub kwa watu wa shy,kigoma bukoba mtukula,tabora,na sehemu nyingi hasa nchi jirani hata kabla ya buzwagi,khm ilikuwa inapeperuka kibiashara hasa wakati ule barabara ilipokuwa mbovu na kutumia bandari kavu Isaka...kahama imetenga eneo jipya la viwanda baada ya lile la mwanzo kujaa(bukondamoyo) kwenda mwendakulima mondo....ukuaji na upimaji wa mji ni wa kazsi ni marachache kukuta ujenzi holela japo barabara bado sana..haitegemei madini hata wakati migodi ikifungwa mambo huendelea...kasi ya ukuaji wake umefanya kuzalishwa kwa halmashauri tatu zinazojisimamia zenewe ushetu, msalala na mji...vyote hapo juu nililkuwa naelezea halmashauri ya mji kahama..sio wilaya yyote....angalia grafu za nbs na takwimu za tra utajua wapi fursa inaangaza zaidi....
 
Umejitahidi kuelezea kwa logic but kwa nini haipewi hadhi ya Manispaa?
 
[emoji109][emoji109]
 
Pamoja na hayo nataka kujua ,Mfano mji wa Geita kwa miaka ya hivi karibuni umekuwa ukikusanya mapato ya ndani makubwa sawa na Manispaa ya Kigamboni wastani wa 8 bln kila mwaka na inaipita Kahama mbali tuu lakini mbona sisikii Geita ikiitwa bussiness hub kwa mantiki hiyo?
Hamuoni kwamba kigezo cha mapato mengi na kuwa bussiness hub haitoshi kuufanya mji kukua na kuendelea? Mapato ya Miji mingi kwa mfano Iringa,Tabora,Songea,Singida,Sumbawanga na Moshi ni nusu tu ya kinachokusanywa Kahama lakini miji hiyo ni mikubwa na ina maendeleo ya kimiundombinu na huduma sana, Kahama haiwezi kusogeza pua
The same applies to Njombe au ,pamoja ya kwamba sio mji wa biashara za kichuuzi na hauna mapato makubwa kama Kahama yet ukiangalia tuu unaona Njombe imeendelea kuliko Kahama kwa aspects zote sasa hii inakuaje? ufafanuzi tafadhari
 
Umesahau kuwapa hii mkuu,
Nyanda za juu kusini Wakazi wa huku tuna juhudi sana za kupanda miti, misitu Husaidia sana kubadilisha hali ya hewa na kustabilize, ukianzia Iringa, wilaya ya Kilolo na Mufindi zote zimekuwa covered na forests, Kule kwetu kilolo kwa Sasa ni misitu kila kona yaani kila familia ina shamba la miti, ukija njombe na Mbeya ni almost the same story, sehemu kama hizi hutasikia ukame kila mwaka, hilo ni moja,
Pili misitu hii imefanya Wakazi wa Kusini wawe na utajiri ambao ni sustainable, ndio maana hakuna nyumba za tembe Iringa, wala njombe, wala Mbeya, wala Sunbawanga, unakuta mtu wa kawaida kabisa amejenga nyumba yake Standard na ameweka na mfumo wa Umeme wa Solar,
Ukitoka pale Njombe uende hadi Makete kupitia njia ya Ikonda ndio utaelewa Mchango wa Wakazi wa Kusini katika kutunza Mazingira, sio kuchimba na kuacha mashimo na Kuharibu mazingira na kuacha watu na umasikini huku pesa ikitoweka na wafanya biashara wa Madini ambao wengi wala sio wa Nchi hii.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia, niliweka hizi parameters ambazo kama mtu mwenye akili lazima aziorodheshe kama viashiria vya Maendeleo,

1.Makazi ya Watu
2. Huduma za Elimu
3.Upatikanaji wa Huduma za Afya
4.Miundombinu ya Barabara
5. Huduma za Umeme na Maji safi kwa wananchi
6. Mazingira na Hali ya hewa
7.Viwanda
Prove me wrong kama kuna hata moja kati ya hayo Kahama imezidi Mufindi.
Kufananisha kahama na mufindi ni dharau...

Kahama wako vzur ase...

msidanganyane hapa

...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…