Wawekezaji wapo kazini wanajenga mji wa kitalii Kijiji Cha mlungu hiki Kijiji kipo km56 kutoka rujewa makao makuu ya wilaya ya mbarali na kipo km 35 kutoka makambako tc kupitia saja na ndo eneo linapakana na mbuga ya ruaha tofauti ukipitia uwanja wa nduli Iringa km zaidi ya 100 wakati hichi Kijiji kinapakana na hii mbuga 👇👇👇👇👇👇👇DC MBARALI AFURAHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA CHUO CHA UTALII KIJIJI CHA MULUNGU MBARALI.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kanali Denis Filangali Mwila ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, siku ya leo Juni 03, 2024 , imetembelea Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Chuo cha Utalii, pamoja na Uwanja wa Ndege, unaotekelezwa na Taasisi ya Six Rivers Africa katika Kijiji cha Mulungu Wilaya ya Mbarali na kuridhishwa na Mradi huo.
"Tunawashukuru sana kwa kuweza kutuletea maendeleo katika Wilaya yetu ya Mbarali, kwa sababu Mradi huu utagharimu Tsh. Bilioni mbili nukta Nne (2,400,000,000/=) hata hivyo hapa kuna zaidi ya Wananchi karibu 50 wanaopata fedha kupitia mradi huu" ( yaani ajira za muda mfupi)
Pia, Kanali Mwila ameongeza kuwa, Mradi huu ni jitihada Mhe, Daktari Samia Suluhu Hassan katika sinema ya Royal Tour kuvitangaza vivutio vyetu, na vilevile analeta maendeleo kwetu kupitia miradi hii. Mbali na faida za Utalii, Kanali amesema mradi huu utaweza kisaidia Watu kujifunza umhimu wa Uhufadhi kwani Mbarali pia ni chanzo cha maji ya Mabwawa mengi; Bwawa la Mtera, Kidatu na hata katika Bwawa la Mwalimu Nyerere, Mbarali inatoa 15% ya maji yote katika Bwawa hilo.
Kwa upande wa Mkuu wa Oparesheni wa Six Rivers Africa, ndugu Abubakari Mure, amesema wanategemea kuanza kupokea wanafunzi mwezi wa Julai, mosi 2024 ambapo wanategemea kuanza na wanafunzi 60 kwa kila Kozi itakayokuwa inatolewa na Chuo hicho.
Jumla ya Kozi nne zimepangwa kufundishwa katika Chuo hicho ambazo ni; Guide Training, Chef raining, Manager training pamoja na Service Bingwa (housekeeping and waiters)
#NasimamanaMheDaktSamiaSuluhuHassan