Watu wangu wa Njombe asanteni kwa ushiriki wenu kwenye hii thread, ningependa kuhitimisha mada hii kwa kuja taarifa kutoka kwa Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mhe.Seleman Jafo. Tanzania nzima maeneo yaliyokizi vigezo vya kuwa Manispaa ni matatu tu.
Waziri wa TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema Serikali inatambua maeneo matatu hapa nchini ambayo serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi kuwa Manispaa kutokana na kukidhi vigezo vya kujitosheleza kimapato.
Mhe.Jafo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani na Halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita na muda wowote kuanzia sasa maeneo hayo yatapandishwa hadhi kuwa Manispaa pindi mchakato utakapokamilika.
Na kwa taarifa yenu kwa kanda ya ziwa baada ya Mwanza Jiji (Rock city) mji unaofuata kwa shughuli za kibiashara ni Kahama mjini yaani hata Geita mji, Bukoba mji, Shinyanga Mji na Musoma mji, Bariadi mji (Simiyu) wanasubiri sana.
MKOME KULIGANISHA DHAHABU NA MISITU
Kahama VS Njombe/Mafinga - JamiiForums
View attachment 1424014