Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) wamefanya ziara kwenye kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono cha MSD kilichopo Idofi,Makambako Mkoani Njo mbe.
Wakurugenzi hao wameshuhudia namna mpira ya mikono inavyozalishwa, kuanzia hatua ya kwanza hadi kukamilika kwake, zinapowwkwa kwenye vifungashio.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa MSD Mboyi Wishega amesema tayari kiwanda hicho kimepata ithibati ya ubora, yaani GMP, ambayo inawezesha kiwanda hicho kuanza kuzalisha na kuuza bidhaa ya mipira ya mikono.
Wishega ameeleza kuwa iwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono 20,000 kwa saa sawa na jozi 10,000 za mipira ya mikono kwa saa.
Ameongeza kuwa kuanza kwa uzalishaji kiwandani hapo utapunguza uagizaji wa bidhaa za mipira ya mikono kutoka nje ya nchi na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji Dkt. Pamela Sawa amesema uzalishaji huo utasaidia kuboresha utoaji huduma kwa wateja wa MSD kwani upatikanaji na ubora
wa bidhaa hii sasa utasimamiwa kwa ufasaha na Bohari ya Dawa (MSD), ambaye ndiye msambazaji wa bidhaa za afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA Amani Abdul Dello amesema amefurahishwa na mifumo iliyofungwa kwenye kiwanda hicho na kuongeza kuwa, kwa kiwanda hicho kupata ithibati ya ubora (GMP) ni hatua sahihi kukiwezesha kiwanda hicho kuanza kuzalisha na kuuza bidhaa hiyo nchini.