Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

1721980992905.jpg
 
Tunaendesha aina mbili za treni za mizigo yaani kupitia trafiki na treni za trafiki za ndani. Kupitia treni za trafiki husafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania hadi New Kapiri Mposhi nchini Zambia na kinyume chake. Treni za trafiki za ndani husafirisha shehena ya kati na zinaweza kuvuka au zisivuke mpaka. TAZARA pia hutoa huduma za treni za barabarani na huduma mchanganyiko za treni ambazo zimeundwa kukidhi mahitaji na mahitaji maalum ya wateja.

Viunganishi vya Mkoa

Njia ya reli ya TAZARA imeundwa kwa kupima 1067mm, ambayo inaruhusu kupitia shughuli za trafiki na reli nyingine za Kusini mwa Afrika, kama vile Spoornet ya Afrika Kusini, Botswana Railways, National Railways of Zimbabwe, Zambia Railways Limited Namibia Railways, Reli ya Msumbiji na Societe Nationale Des Chemins Des Chemins De Fer Du Congo Sarl ya DRC.

Kimsingi, mitandao yote ya reli katika sehemu ya Kusini mwa Afrika inaweza kufikiwa na TAZARA. Ikiwa na uwezo uliobuniwa wa tani milioni tano (5) za mizigo kwa mwaka, TAZARA imekuwa ikishughulikia trafiki kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA), na hivyo kutoa kiunganishi muhimu cha kikanda kati ya kanda za Kusini, Mashariki na Kati na nchi zingine za ulimwengu kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Terminus ya Mizigo

Tuna kituo cha kisasa cha kusafirisha mizigo, kilicho kamili na gantry cranes na vifaa vingine vya kuhudumia katika vituo vya New Kapiri Mposhi, Kasama, Makambako na Dar es Salaam. Vifaa hivi vinatoa njia ya haraka na bora kwa wasafirishaji na waagizaji kutoka kanda mbalimbali za Afrika kupakia na kupakua mizigo kwenye na kutoka kwenye mabehewa ya TAZARA.

New Kapiri Mposhi inashughulikia mizigo kutoka na kutoka mikoa ya Kusini na Afrika ya Kati, wakati Kasama inashughulikia eneo la Maziwa Makuu. Vilevile, Mbeya na Makambako huhudumia mizigo kutoka Malawi na baadhi ya maeneo ya Maziwa Makuu.

Kwa kuenea kwa kituo cha TAZARA, mizigo inasafirishwa kwa urahisi kutoka mkoa hadi mkoa. Kwa kuongezea, kuna kituo cha kibinafsi cha usafirishaji cha mizigo huko Kidatu ambacho kinashughulikia uhamishaji wa mizigo kutoka kwa mabehewa ya TAZARA ya geji pana (milimita 1,067) hadi kwenye mabehewa nyembamba zaidi ya (milimita 1,000) ya Shirika la Reli la Tanzania (TRL) kuwezesha kuunganishwa kwa Afrika Kusini, Kati na Mashariki
TAZARA-KAPIRI-TOUR-093.jpeg
1722137358131.jpg
 
HII BARABARA YA NJOMBE MANDA IKIKAMILIKA ITAWARAHISISHIA SANA NCHI JIRAN YA MALAWI NA ZAMBIA NK KUTUMIA HII BARABARA KWANI NI SHORTCUT UKITOKA BANDARI YA MANDA UNAVUKIA MJI WA CHILUMBA MALAWI AMBAKO KWOTE WAMESHA JENGA BANDARI NA BARABARA MAKAWI TAYARI BADO YA KWETU UJENZI NDO UNAENDELEA NA KUTOKA MANDA HADI BANDARI YA DSM NI KM 875 ZINAPISHANA KIDOGO NA DAR TO MBEYA HII ITASAIDIA KUPUNGUZA HATA FOLENI TUNDUMA mfano ukitoka kyera hadi Lilongwe ni km 675 wakati CHILUMBA hadi Lilongwe ni km 325 👇👇👇👇👇👇👇👇 CCM NJOMBE, RC MTAKA WARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA YA KIWANGOCHA ZEGE YA ITOLI-LUDEWA-MANDA

Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe wameupongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara ya Itoni - Lusitu kwa kiwango cha zege yenye urefu wa kilometa 50 ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Itoni -Ludewa - Manda (Km 211.4).

Barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Malawi na Tanzania upande wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania na ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vivutio vya utalii, kuwa kiungo kizuri kati ya mgodi wa makaa ya mawe (Mchuchuma) bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa. Pia Barabara hii ikikamilika itakuwa kiungo kizuri na barabara za ushoroba wa Makambako hadi Ruvuma.

Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani Njombe, Katibu wa CCM Mkoa wa mkoa huo Ndg Julius Peter amempongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ndiyo watekelezaji.

Amesema kuwa CCM imeridhishwa na ujenzi huo ambao ulisimama kutokana na mvua kubwa za El-Nino ambazo zilizokuwa zinaendelea kunyesha na baada ya mvua hizo kumalizika sasa amewasihi wakandarasi kuendelea na kazi ya ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Antony Mtaka amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetibu vikwazo vya miradi mbalimbali mkoani Njombe ambapo ameridhia kuanza kwa mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kutoa shilingi Bilioni 15 kulipa fidia pamoja na kukubali kuanza kwa mradi mkubwa wa chuma wa Maganga-Matitu.

Vikwazo vingine vilivyotibiwa ni pamoja na kuimarisha na kujenga miundombinu ya barabara ikiwemo kutoa jumla ya shilingi Bilioni 120.9 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itoni -Ludewa - Manda kipande cha Itoni - Lusitu kwa kiwango cha zege ambayo ni barabara yenye gharama kubwa kuliko zote Tanzania.

"Dhamira ya Mhe Rais kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha zege ndani ya muda kama ilivyokusudiwa, Pesa zipo wakandarasi wapo, tulipata changamoto ya mvua lakini kwa sasa miradi inaendelea na wananchi waanze kufuatilia fursa za uwekezaji zitakazoimarisha uchumi wao" Amekaririwa Mhe Mtaka

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa Wakala ya Barabara Tabzania (TANROADS) mkoa wa Njombe Mhandisi Ruth Shalua amesema kuwa Mkataba wa Ujenzi wa Barabara hii ulitiwa saini kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkandarasi M/s China Civil Engineering Construction Cooperation kutoka China tarehe 29 Machi, 2022 kwa gharama ya Shilingi 120.9 pamoja na VAT.

Amesema kuwa Mhandisi Mshauri anayesimamia mradi huo ni Cheil Engineering Co. Ltd ikishirikiana na kampuni ya Hana E&C Co. Ltd na ENGTEC Engineering (T) Ltd zote za Tanzania.

MWISHO
 
Mkuu mimi sipo kishabiki bali nitakupa ukweli,kwanza umekosea kulinganisha mkoa na wilaya,Njombe ni mkoa ina wilaya 4 na Halmashauri 6 ambapo mafinga na kahama zote ni wilaya.kwa kuangalia fursa za kibiashara katik hayo maeneo uliyotaja Njombe wilaya na hata Mkoa ipo mbali sana kuzidi hizo wilaya ulizozitaja.
Lakini kwa point yako sehemu ya wewe kuanzia fursa nitakushauri uende kahama kwa sababu zifuatazo
1.Ni vigumu sana kufanya biashara ya aina yoyote Njombe/mafinga kama sio mzawa au mshirikina
2.Njombe hamna mchanganiko wa watu wa mikoa mingine,tofauti na wafanyakazi wa serikalini,so bado wana mambo ya kizamani ya undugu na ukwetu.
So it is better uende kahama
Ukweli mtupu a see huku njombe watu wake ni wabinafsi hatari
 
Tarehe 2 mwezi wa Nane, 2024 Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) inakwenda kuandika historia mpya kwenye sekta ya madini kwa kuingia mkataba wa uchimbaji wa Chuma na mwekezaji kutoka China.

Mradi huo upo mkoani Njombe, Wilayani Ludewa. Hatua hii kubwa inakwenda si tu kulisaidia Taifa kuongeza mapato bali kuongeza ajira kwa Watanzania na kukuza mnyororo mzima wa thamani.

#ndc #shirikalataifalamaendeleo #investment #uwekezaji #nationaldevelopmentcorporation
1722254977967.jpg
1722254970270.jpg
 
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kushughulikia Barabara zilizoathiriwa na mafuriko/Mvua za El-Nino kwa mkoa wa Njombe.

Fedha hizo zimetumika kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya Barabara iliyoathiriwa na wananchi kushindwa kutoka eneo moja Kwenda jingine inapitika kwa haraka kama ambavyo serikali imekusudia.

Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya miradi ya Barabara inayoendelea na matengenzo mbalimbali Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Njombe Mhandisi Ruth Shaluwa amesema kuwa Maeneo ya miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoathiriwa na Mvua za El Nino mwezi Januari – Mei, 2024 ni Itoni – Ludewa – Manda Km 211.4; Sehemu ya Lusitu – Mawengi Km 50 (Maporomoko ya Udongo, Gangitoroli Km 62 – Km 64 na Jongojongo Km 82 – Km 85), ambapo kiasi cha shilingi Milioni 350 zimetumika.

Maeneo mengine ni Pamoja na Barabara ya Njombe – Makete Km 107.4 katika Maporomoko ya Udongo eneo la Mang’oto, Barabara ya Ikonda – Lupila – Mlangali Km 78.84 katika eneo lililokatika kwenye barabara na Maporomoko ya Udongo ambapo shilingi Milioni 383 zimetumika.

#kilichoborakabisa
1722447375895.jpg
 
KUMEKUCHA MOJA YA KAMPUNI YA KICHINA INAYOJENGA INDUSTRIAL PARK MAKAMBAKO NAONA NDO INAINGIA MKATABA NA NDC MKOA WA NJOMBE UNAENDA KULETA MAGEUZI YA KIUCHUMI WA VIWANDA
1722482701974.jpg
1722480576506.jpg
 
Back
Top Bottom