Mkoa wa njombe now unaangaliwa kwa jicho jingine na Serikali kutokana na fursa ulizonazo 👇👇👇👇👇👇Mkurugenzi wa Cultural Museum Kutoka Arusha Atembelea Njombe kwa Lengo la Uwekezaji
Mkurugenzi wa Cultural Museum kutoka Mkoa wa Arusha, Bw. Wito Msafiri, amefanya ziara ya kikazi mkoani Njombe leo, tarehe 21 Novemba 2024, kwa lengo la kutazama fursa za uwekezaji wa Kijiji cha Utamaduni. Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, Bw. Msafiri alieleza dhamira yake ya kuanzisha mradi huo ili kukuza utalii wa kiutamaduni na uchumi wa mkoa huo.
Mhe. Mtaka alimkaribisha kwa furaha na kupongeza hatua hiyo, akisema, “Tunafurahi kuona wawekezaji wenye mtazamo wa kuendeleza utamaduni na utalii wanavutiwa na Njombe. Hii ni fursa kubwa kwa mkoa wetu, na tutatoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha mradi huu unafanikiwa.”
Mara baada ya kuwasilisha maelezo ya mradi huo, Bw. Msafiri alimkabidhi Mhe. Mtaka zawadi ya picha nzuri inayoonyesha kazi ya sanaa na kikombe cha kipekee, ishara ya kuthamini urithi wa kiutamaduni wa Tanzania.