Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Usagara
20250129_095510.jpg
 
Haya baada ya kuwa na mji wa viwanda na biashara tic wanaongea 👇👇👇👇👇👇Mkoa wa Njombe ni mkoa unaokuwa kwa kasi kiuchumi hasa kupitia uwekezaji wa viwanda.

Miongoni mwa viwanda vinavyoleta mageuzi makubwa ni Avo Africa Tanzania Ltd, kiwanda cha kuchakata parachichi ambacho kimekuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima na wananchi wa Njombe kwa ujumla.

Kiwanda hiki, kilichosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mwaka 2021, kimeleta mapinduzi katika sekta ya kilimo kwa kutoa soko la uhakika kwa wakulima wa parachichi.

Wakulima zaidi ya 4,000 wamenufaika moja kwa moja kwa kuuza mazao katika mradi huu, huku wengine wakijipatia ajira katika kiwanda hicho.

Kupitia Avo Africa Tanzania Ltd, wakulima wa Njombe sasa wana mahali salama pa kuuza parachichi zao, wakihakikishiwa kipato endelevu.

Kiwanda hiki kinajihusisha na uzalishaji wa mafuta ya parachichi, bidhaa inayopata soko kubwa ndani na nje ya nchi. Kwa njia hii, thamani ya zao hili imeongezeka, na wakulima hawalazimiki tena kuuza parachichi kwa bei ya hasara.

Zaidi ya hayo, kiwanda hiki kimetengeneza fursa mpya za ajira kwa wakazi wa Njombe. Wafanyakazi wa viwandani, wasambazaji wa malighafi, na hata wajasiriamali wanaoendesha biashara zinazohusiana na uzalishaji wa mafuta ya parachichi wote wamenufaika kwa namna moja au nyingine.

Afisa Uwekezaji wa kanda hiyo Bi. Privata Simon amesema kuwa pamoja na mchango huo mkubwa kiuchumi mnamo mwaka 2024, Avo Africa Tanzania Ltd ilitunukiwa tuzo ya mlipaji bora wa kodi wa mwaka kwa mkoa wa Njombe.

Hii ni ishara kuwa mbali na kusaidia wakulima na wafanyakazi wa mkoa wa Njombe, kiwanda hiki kimechangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia kodi na mapato mengine yanayotokana na biashara yake.
IMG-20250131-WA0002.jpg
 
MAKAMBAKO NI MWENDO WA VIWANDA 👇👇👇👇👇👇🚍Mwekezaji Aomba Eneo kwa Ajili ya Kiwanda cha Kuchakata Mafuta ya Parachichi Njombe

Njombe, 29 Januari 2025 – Mwekezaji kutoka Elworld Agro & Organic Foods Ltd, Bw. Parakh Gupta, amefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kusaini kitabu cha wageni, ambapo alipokelewa na Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Katika mazungumzo yao, Bw. Gupta alimweleza Mhe. Mtaka kuwa ujio wake unalenga kutafuta fursa za uwekezaji katika kilimo cha kisasa na maendeleo ya miundombinu. Alisisitiza kuwa Elworld Agro & Organic Foods Ltd inaangazia zaidi kilimo hai (organic farming).

Aidha, Bw. Gupta aliomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta yatokanayo na parachichi pamoja na ekari zaidi ya 200 kwa ajili ya kilimo cha parachichi. Alibainisha kuwa uwekezaji wake utawapatia wakulima wa parachichi soko la uhakika nchini Tanzania na India.

Pia, aliahidi kuwa kampuni yake itawawezesha wakulima kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya kurahisisha uandaaji wa mashamba ya parachichi, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa mazao.

"Ni heshima kubwa kwetu kukutana na Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya majadiliano na uwasilishaji wa wazo letu la kuwekeza katika maboresho ya miundombinu ya mkoa wa Njombe," alisema Gupta.

Ujio wa mwekezaji huyo unaashiria fursa ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali katika kukuza kilimo na kuboresha miundombinu mkoani Njombe, hatua ambayo inaweza kuwanufaisha wakulima na jamii kwa ujumla.
 
Ubaruku, Na igawa , moja ya kata ambazo zitaunda halmashauri ya mji rujewa ambayo itapakana na wangingombe km 40 kutoka makambako sub town zinazidi kuchangamka na km 116 hadi mbeya city
1731093793250.jpg

1738464092166.jpg
1709901587833.jpg
 
Back
Top Bottom