Kaimu RPC Mwanza: Risasi zilipigwa hewani bahati mbaya ikampata mtu Mmoja na kumwua...

Kaimu RPC Mwanza: Risasi zilipigwa hewani bahati mbaya ikampata mtu Mmoja na kumwua...

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
Nimemsikiliza huyo Mama hata jina lake sikutaka kulijua.
Anasema Police walifika pale kutuliza ghasia, huku wakirusha au piga risasi juu kwa BAHATI MBAYA ikampata Raia Mmoja.

Nataka kujua hawa waliojeruhiwa walikuwa wamekaa hewani huko zilipo pigwa Risasi.

...huyo mama yupo sawa kweli...alafu anasema wanachunguza, wanachunguza nini wakati Risasi zilipigwa hewani na ilimpata bahati huko huko juu.

Kaimu kamnda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ofisa Mnadhimu
(SO) SSP Lilian Matola ,
alitihibitisha kutokea kwa
vurugu hizo ambazo
zilisababisha kifo bna majeruhi na kwamba jeshi hilo lilingia mtaani kutuliza ghasia hizo ambazo zilidumu kwa saa nne.

Alisema askari mgambo wa jiji wanaotuhumiwa
kusababisha kifo na majeruhi
hao wanashikiliwa na jeshi
hilo kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa SSP Matola , mgambo hao wa jiji walitumia risasi hizo za moto kwa nia ya kujihami na kundi la
wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakiwashambulia kwa mawe..

Aidha Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula,
aakizungumza na wandishi
wa habati kwenye ukumbi wa jiji jana jioni alisema hakukuwa na opereshani
maalumu ya kuwaondo
machinga katika meneo hao bali shughuli za kawaida za halmashauri hiyo kuhakikisha jiji liakuiwa safi.
 
Nime msikiliza huyo Mama hata jina lake sikutaka kulijua.
Anasema Police walifika pale kutuliza ghasia,huku wakirusha au piga risasi juu kwa BAHATI MBAYA ikampata Raia Mmoja.

Nataka kujua hawa waliojeruhiwa walikuwa wamekaa hewani huko zilizopo pigwa Risasi.

...huyo mama yupo sawa kweli...alafu anasema wanachunguza,wanachunguza nini wakati Risasi zilipigwa hewani na ilimpata bahati huko huko juu.

Mkuu....hivi wewe ulitegemea maelezo tofauti na hayo?Tegemea tena maelezo yafuatayo baada ya uchunguzi wao...Alipigwa na chuma chenye ncha kali, alitaka kupora duka la mfanyabiashara mwenye asili ya ki asia....mengine ongezeni
 
Kwa hiyo huyo jamaa aliyeuwawa naye alikuwa angani? Itafika mahali wananchi tukichoka kusikia hizi lugha za kitoto kutakuwa hapatoshi. Mara kitu chenye ncha kali, mara kitu kizito chenye mshindo, na sasa ni angani ila ni bahati mbaya.
 
huyu mama ni kati ya wanawake waliopata kazi kwa njia ya chupi hata mimi nimesikiliza taarifa ya habari ya saa1 asubuhi kweli inasikitisha sana. lakini ukiwa muongo kweli lazima uzae waongo maana baba (ccm) yao ni muongo ndio hao wazaliwa walisha ridhishwa
 
Hahahahaaa nilidhani niko peke yangu kumbe tumeskia wengi, yaani wametoa taarifa kkaribia tatu hivi kwa tukio moja, ukiacha hiyo ya RPC ambayo ndio pengine nilikua naitegemea kidogo iwe na kaukweli fulani kuna ile inayosema kuwa, Mmachinga aliyepigwa risasi alipigwa na Mgambo baada ya kutoa sime na kutaka kumkata nayo Mgambo ndipo mgambo akaamua kujihami, nikajiuliza hivi kumbe siku hizi hawa mgambo wanapewa silaha za moto? Nikajinyamzia, Mara kwenye gazeti lingine wakasema aliepigwa risasi ni Mpiga Debe anaitwa Greda, hapa napo nikajiuliza vurugu za wamachinga mpiga debe anapigwaje risasi, nikakaa kimya pia, nikaambiwa pia kuwa Ni Polisi ndiowalifyatua risasi hewani na ikampata kwa bahati mbaya huyu marehemu mmachinga wetu, nikaona maajabu mengine haya, kumbe risasi zinapiga kona siku hizi au pengine zinapeperushwa na upepo!!!!!!

Mara wale askari wameshawekwa kizuizini kwa kutumia silaha za moto mara wale mgambo wa jiji wamekamatwa wako ndani, mmmh nilipofikia hapa nikaamua niamke nikatafute kahawa nipate kikombe labda naota..................
 
Nchi ya kusadikika!!
Hivi,watanzania tutaendelea kuuawa na kuwa wapole hata lini?
 
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, hawa polisi wanaona watu wapuuzi dawa yao inachemka
 
Ni kweli ilimpata wakati inatoka juu kuja chini...."descending"
 
Huyu mama Ag RPC anaitwa Lilian Matola. Sijui hata kama kweli alisoma Physics ya form II vinginevyo ni aibu tupu. Risasi ipigwe HEWANI halafu itelemke chini by gravitational force, inaweza kweli kumua mtu achilia mbali kumjeruhi?!

Uwongo mwingine ni wa kulidhalilisha JESHI la POLISI, na ku prove "folkore" kwamba POLISI wengi ni form four failure!
 
hivi akiwa anasema hivo,waandishi wa habari awaruhusiwi kuuliza? au wanaamin,ili ni changa la macho ata mtoto mdogo uwezi mdanganya
 
hivi akiwa anasema hivo,waandishi wa habari awaruhusiwi kuuliza? au wanaamin,ili ni changa la macho ata mtoto mdogo uwezi mdanganya

Kuna mwandishi alimwuliza walikuwa wakiongea kwa njia ya simu,imekuwaje risasi zipigwe juu then ziue akajibu hilo wanalichunguza.
 
Maskini jeshi letu la polisi mweeh mweeh

Kuua muue hata kutoa maelezo mjichanganye

Ili kumtendea haki victim tunaomba wahusika wa mauaji wafikishwe mbele ya vyombo husika sasa na kama sio sasa basi sasa hivi.

kila nafsi itaonja mauti. RIP bro
 
Back
Top Bottom