BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
ndo jeshi la polisi hilo...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa unataka ufe wewe au uhai wa huyo jamaa....unathamani gan kwangu acha afe
Kwa hiyo huyo jamaa aliyeuwawa naye alikuwa angani? Itafika mahali wananchi tukichoka kusikia hizi lugha za kitoto kutakuwa hapatoshi. Mara kitu chenye ncha kali, mara kitu kizito chenye mshindo, na sasa ni angani ila ni bahati mbaya.
mkuu risasi ikishalipuka wakati inaenda hewan (ascending) inapoteza nguvu kbsa, ikirudi chin km karatas tu, haina madhara.Ni kweli ilimpata wakati inatoka juu kuja chini...."descending"
ukifuatilia utakuta ndo wale wanaonunua vyeti,Huyu mama Ag RPC anaitwa Lilian Matola. Sijui hata kama kweli alisoma Physics ya form II vinginevyo ni aibu tupu. Risasi ipigwe HEWANI halafu itelemke chini by gravitational force, inaweza kweli kumua mtu achilia mbali kumjeruhi?!
Uwongo mwingine ni wa kulidhalilisha JESHI la POLISI, na ku prove "folkore" kwamba POLISI wengi ni form four failure!
Na ukaambiwa marehemu Mwandosya hakuuliwa na Polisi ingawa picha zilionyesha hivyo, si uliamini? Mbona hii hutaki kuamini sasa??
Kuna mwandishi alimwuliza walikuwa wakiongea kwa njia ya simu,imekuwaje risasi zipigwe juu then ziue akajibu hilo wanalichunguza.
Nilikuwa namdadisi mtaalamu wa milipuko,akawa ananieleza risasi ukiipiga juu ikimaliza mita zake inashuka na inakuwa haina nguvu haiwezi tena kuua mtu,huyo aliyeuawa mwanza alipigwa risasi,na swali aliloniuliza huyo mtaalamu wa milipuko je inakuwaje vurugu za wamachinga uende na bunduki ?je unaweza kumpiga mtoto wako kwa kutumia panga kama akikukosea?
One million dollar question,,,je polisi wameruhusiwa na nani kuua raia?na kwa nini wanatumia nguvu kubwa sana siku hizi?enzi za nyerere,mwinyi,mkapa kulikuwa na kamatakamata za uzururaji lakini hatukuwahi sikia mtu kauawa inakuaje sasa hv polisi wanakuwa hivyo?je ni kuwatisha wananchi wasijaribu kufuatilia haki zao?
hapa tanzania polisi wanaongoza kuua,kisha ajali za barabarani!jee tuna haja ya kuwa na jeshi la polisi?
Mi nilijua kwamba hawawezi kuja na jipya hapo. polisi wa siku hizi sio wa kweli na ukiongozana nae ogopa kabisa!