Nilikuwa namdadisi mtaalamu wa milipuko,akawa ananieleza risasi ukiipiga juu ikimaliza mita zake inashuka na inakuwa haina nguvu haiwezi tena kuua mtu,huyo aliyeuawa mwanza alipigwa risasi,na swali aliloniuliza huyo mtaalamu wa milipuko je inakuwaje vurugu za wamachinga uende na bunduki ?je unaweza kumpiga mtoto wako kwa kutumia panga kama akikukosea?
One million dollar question,,,je polisi wameruhusiwa na nani kuua raia?na kwa nini wanatumia nguvu kubwa sana siku hizi?enzi za nyerere,mwinyi,mkapa kulikuwa na kamatakamata za uzururaji lakini hatukuwahi sikia mtu kauawa inakuaje sasa hv polisi wanakuwa hivyo?je ni kuwatisha wananchi wasijaribu kufuatilia haki zao?