Kajala: Siyo kwamba hakuna wanaume wanaonipenda, ila nikiwa na Harmonize nakuwa na amani

Kajala: Siyo kwamba hakuna wanaume wanaonipenda, ila nikiwa na Harmonize nakuwa na amani

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwigizaji mashuhuri wa filamu nchini, Kajala Masanja, amefunguka kuhusu sababu zinazomfanya arejee kwenye mahusiano na msanii wa muziki wa Bongo Flava, Rajab Abdul Kahali 'Harmonize', kila wanapotengana. Kajala ameeleza kuwa utulivu na amani anayoyapata akiwa na msanii huyo ndivyo vitu vikuu vinavyomvutia kupita mahali pengine popote.

1790595776629.png

Akizungumza wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha 'A List', Kajala alieleza kuwa ingawa anatambuliwa na wanaume wengi wenye nia njema, moyo wake hupata amani ya pekee pindi anapokuwa na Harmonize.

“Unajua kuna muda inakuwa ni ngumu kueleweka, siyo kwamba mimi sina wanaume wa maana wanaonipenda, wapo wengi sana wanakuja, ila mimi kuna namna fulani nakuwa na amani na furaha nikiwa na Harmo kuliko sehemu zingine," alisema Kajala.

Kauli hiyo imeweka wazi hisia zake za ndani kuhusu mahusiano yao ambayo yamekuwa yakifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wao pamoja na jamii kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom