Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kaka wa Tundu Lissu, ambaye anaitwa Alute Mughwai Lissu amefichua kwamba mnamo mwezi Disemba mwaka jana 2025, aliwahi kufuatwa na moja ya viongozi wa juu wa Serikali, akimtaka kuandika barua kwa ajili ya kumuombea msamaha Lissu ili kesi yake ya uhaini iweze kumalizika kibinadamu.
Mzee Alute amefichua jambo hilo wakati alifanyiwa mahojiano na chombo cha habari cha The Chanzo, ambapo bila kumtaja kiongozi huyo, alikiri kuwahi kufuatwa kwa ajili ya jambo hilo ingawa halikuweza kufanikiwa.
Katika mahojiano hayo, amesema baada ya kukutana na kuzungumza na kiongozi huyo, alimwambia jambo hilo ni gumu kwa kuwa ili aweze kuandika barua ya kumuombea msamaha, basi ni lazima aone kweli ndugu yake huyo ametenda kosa aliloshtakiwa nalo, jambo ambalo amesema yeye haoni kama lina ukweli.
Aidha, amesema kupitia mazungumzo hayo, alimpa mapendekezo kadhaa kiongozi huyo ikiwemo kushughulikia juu ya waliohusika na tukio la kupigwa risasi kwa Lissu, kumlipa fidia za matibabu sambamba na kuiondolea vikwazo vya kisiasa CHADEMA.
Hatahivyo, Mzee Alute amesema baada ya kufikisha mapendekezo hayo, kiongozi huyo aliahidi kuwa atakwenda kuyafanyia kazi lakini hakukuwa na kitu kilichofanyika na hivyo mpango huo kutofikia muafaka wowote.