#COVID19 Kaka yangu amefariki kwa ugonjwa wa CORONA

Mtoto wa Nyerere

Senior Member
Joined
May 21, 2021
Posts
129
Reaction score
689
Kaka yangu kafariki jioni hii kwa covid 19 hospital ya Bugando Mwanza hakika ni majonzi makubwa sana.

Alifikishwa hapo kwa matatizo ya uchovu tu na kwenda kucheki na hakupelekwa na mtu alienda akiendesha gari yake mwenyewe ila badae walimpima na kukuta ana corona akawekwa pale toka juzi Leo kazidiwa mchana Leo na jioni amelala akiwa bado ajawekwa kwenye oxygen.

Hakika ni majonzi makubwa.

He was a really man ameacha watoto wadogo na mke very sad indeed.
 
Poleni sana Mkuu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja kipindi hiki kigumu kwenu. 🙏🏾
 

Pole sana mkuu. Kasema SSH wanaobeza jitihada za huu ugonjwa ni vile hawajaguswa.

Tupate chanjo wakuu ugonjwa udhibitiwe kwanza.

Mengine baadaye.
 
Pole sana mkuu, Mungu awape faraja nyakati hizi za majonzi, chukueni tahadhari zote mualinde na wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…