Just when you thought you've heard it all.....
Shida ya hawa wenzetu wanaoana hata watu wa karibu kabisa, mfano utakuta mara kadhaa mtu kamwoa mpwa wake, binamu wa kwanza, mtoto wa mama mdogo, mtoto wa mjomba, nk. Ni ajabu sana. Watoto wanaozaliwa humo mara nyingi wanakuwa na matatizo ya afya kwa vile damu yao ni moja - inazunguka humohumo tu. Wanakuwa dhaifu na hata vilema wa akili au maungo. Watu waende wakaoe mbali, wachanganye damu mpya, na kufungua milango mipya ya mahusiano na koo na familia zingine.Kwani ndoa ni nini? Maana kama weshakula tundi asa kwa nini anataka ushauri? Si angetaka ushauri kabla hajafanya hizo mara kadhaa? Ah jamani
Sijui pengine dini yake inamruhusu maana nimeshayaona ya hivi mengi tu kwa hawa ndugu zetu
Wacha waoane tu tatizo liko wapi? Umeambiwa kuwa kwa ndugu mtaimbo unalala doro? Ngoma inogileUkishavunja mwiko, mengine yote yanakuwa halali"!
Tumsaidieni huyu dada jamani....
ndugu wa ukweli ni mtoto wa dada kwani dada hasingiziwi mtoto, lakini baba anaweza kuletewa mtoto aso wake, na ndiyo maana hawa walikuwa kinyume na lile neno....'damu nzito kuliko maji'Inakuwaje mtu ukampenda kaka yako kimapenzi? inasikitisha sana
Hakika suala hili liko wazi kabisa katika Qur'an pale Allah Aliyetukuka Aliposema:Tumsaidieni huyu dada jamani....
Mimi ni msichana wa miaka 23, nina kaka yangu baba mmoja na mama tofauti. Yeye ananipenda na mimi nampenda na tumekwisha wahi kufanya mapenzi mara kadhaa. Yeye ameahidi kuwa atanioa. Sisi ni Waislamu, je ni sawa tunachokifanya kama sio sawa tufanyeje?"
Mhh nendeni kawaelezeni wazazi wenu nia na madhumuni yenu, majibu wakatayo wapa ni motisha tosha kabisaa!
Nisamehe lovie si kwamba nimeanza siasa kali hapana laaziz...mnh,
Mydear nawe ushaanza 'siasa kali?' 🙂
Dini ya Uislamu hairuhusu ndugu wa baba/mama mmoja kuoana, wala kujamiiana,...
Hakika suala hili liko wazi kabisa katika Qur'an pale Allah Aliyetukuka Aliposema:
Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia.... (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili ... Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu
an-Nisaa : 23
Mara nyingi watu uteleza katika baadhi ya mambo kwa sababu huchanganya Dini ambayo imekamilika na mila na desturi za kifamilia au kikabila. Na katika suala hili la ndoa Uislamu una sheria yake ambayo inatakiwa ifuatwe na kila Muislamu. Wale wanawake ambao mwanamume au mwanamke hafai kuwaoa/kuolewa wapo wazi katika Qur'an, hivyo wasiokuwa hao anaweza kuwaoa bila ya tatizo lolote. Je, hao wanawake ni wapi? Wao ni kama wafuatao:
1. Mama zenu.
2. Wanawake walio olewa na baba zenu (mama wa kambo).
3. Binti zenu.
4. Dada zenu (shaqiqi, kwa mama tu au kwa baba tu).
5. Shangazi zenu.
6. Halati zenu (mama mdogo).
7. Binti wa kaka zenu.
8. Binti wa dada zenu.
9. Mama waliowanyonyesha.
10. Dada zenu kwa kunyonya.
11. Mama wa wake zenu.
12. Watoto wenu wa kambo (wazawa wa wake zenu kwa mume mwengine).
13. Wake wa watoto wenu (muliowazaa).
14. Dada wawili kwa wakati mmoja.
15. Na wanawake ambao wameolewa (4: 22 24).
Kipengele cha suala lenu ni Na Baba mmoja. Binti wa baba yako akiwa baba yake mzazi ni Baba yako Mazazi... Hata kama mama ni tofauti, au baba tu au shaqiqi huwa hufai kumuoa kisheria.
Na hivyo ndivyo nyinyi ni ndugu kwa baba tu, basi haifai kwako kumuoa.
Allah Yaalam
Mbona hapa hawajakataza dada na kaka kuoana.........?