Kwako Ruttashobolwa,
1. Kuhusu maswali uliyoniuliza (mwanamke au mwanaume, nimeolewa n.k) nadhani si muhimu kukujibu. Hayaongezi wala kupungua chochote kwenye mchango wangu au wako.
2. Ingekuwa vema sana siku nyingine ukaelekeza mchango/ushauri/ufafanuzi wako kwa mtoa mada badala ya ku-attack wachangiaji wenzako. Hii haitamsaidia mleta mada.
3. Ni vizuri pia ukiteleza kuwa binadamu tunatofautiana katika mambo mengi sana, ikiwepo pamoja na mtazamo yetu kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Ninaloliona mimi kuwa ni sahihi si lazima like sahihi kwako pia. Kwa hiyo usilazimishe kila mtu kuendana "mental framework" yako. Haitawezekana.
Ni hayo tu. Asante.