Kaka yangu kamtia mimba mama yetu mdogo. Hili lipoje kwa Wanyakyusa?

Kaka yangu kamtia mimba mama yetu mdogo. Hili lipoje kwa Wanyakyusa?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Ipo hivi miaka kama kumi nyuma, baada ya baba yangu kufariki, tuliitwa na shangazi zetu tukapelekwa huko Tukuyu Busokelo tukapewa mji na kuambiwa sisi ndio tutakaoutunza mji, sababu ni baba yetu alikuwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia Yao ya watoto watatu, na mbaya zaidi shangazi zetu hawapo hapa Tanzania. Mmoja kaolewa Zambia na mwingine yupo zake Uingereza kwa miaka mingi sasa

Baada ya kupewa mji Tukuyu ilibidi tukae vikao na ndugu zetu na tukajaribu kuwaeleza kuwa, kwa hali ilivyo itakuwa ngumu sisi kurudi Tukuyu kwa sababu sie pia tumetawanyika na nyumbani Njombe hapana mtu zaidi ya mama na mimi na mimi nipo jombe kwa kulazimika kusimamia biashara na shughuli alizokuwa anafanya mzee, ukitoa makaburi ya babu, bibi ,baba na ndugu wengine waliozikwa pale hakuna kingine , hata ukisema ufanye shughuli za kiuchumi kule tukuyu kupo slow sana Wana ardhi ndogo hata Heka 20 hazifiki, so management ya Tukuyu itakuwa technically tuff,

Kwenye mazungumzo tukamuomba baba yetu mdogo kwenye ukoo, huyu baba yetu mdogo ameishi na marehemu baba yetu na kusomeshwa ( mahusiano ya baba yetu mdogo na sisi yapo hivi " ukitoa kusomeshwa,kutolewa mahari na baba nk pia baba yake alikuwa ni babu yetu mdogo walifuatana na babu yetu mzaa baba) baba yetu mdogo alijaribu kukata kwa sababu na yeye anaishi Mbeya mjini na kajipata sana na hayupo interested na maisha na mifumo ya tukuyu.
Baada ya kumsihi sana baba mdogo kuwa yeye ndiye apokee kijiti Cha marehemu baba ( kuwa incharge wa ule mji) alikataa kabisa ila akatupa option kuwa Mbeya kwake yupo na shemeji yake wa kike (mdogo wa mke wake kabisa) akatueleza huyo shemeji yake ndoa yake ilivunjika akiwa na watoto wawili, yupo tu mjini labda ndiye akae pale na sisi still tutakuwa ndio wahusika wa mji ule , tunatakiwa tujihusishe na tamaduni za kule kuchangia misiba, kutembelea ule mji ,kusalimia majirani, kuendeleza ule mji kwa kupanda mazao kama parachichi migomba nk ili tu pasipotee ). Kweli baba mdogo akamuomba yule shemeji yake ( kiheshima ni mama mdogo kwetu ukizangatia ni shemeji yake baba mdogo na ukaribu wetu na baba mdogo ni mkubwa sana) Tunashukuru alikubali na ukizingatia yeye ni mzawa wa tukuyu ( sehemu kunaitwa masoko)

Kweli Akahamia pale nilichokifanya nikapeleka mifugo na kumpatia mtaji kidogo wa kuendesha maisha kule kijijini (lengo la kupeleka mifugo ni kufanya mji uwe active pasionakane pametupwa kabisa)

Shida ilianzia hapa mwaka 2022, kaka yetu mkubwa akatushauri December lazima twende kule kijijini, kweli tulienda tuka kaa pale, tukaona mazingira sio rafiki sana( nyumba za kizamani , eneo kubwa ni vichaka ) so tukaazimia tujenge nyumba inayoendana na miaka ya sasa na tufungue shamba, Tukachangishana then tukaanza ujenzi wa msingi, baada ya kuondoka tukawa tumeazimia nyumba iishe kabla ya December 2023

Kabla ya December Tulikuwa tumechangishana pesa inayotosha kumalizia Kuta na kupaua nk , ilipofika October kaka yangu tuliyefuatana alisema amechoka na pilika za mjini so December ataenda tukuyu kama sehemu ya mapumziko yake na akajitolea ataifanyia nyumba finishing na atamaliza Kila kitu( binafsi nilifurahi sana kwa sababu 1. Muda wa kwenda tukuyu nilikuwa Sina) , basi ilipofika December akashuka kule Tukuyu na mafundi wake Toka dar, kweli alijenga nyumba na kuanza kufanya finishings. Kumbe akiwa kule akawa anajipigia yule mama yetu pale

What happen there ni mimba na yule mwanamke ana mimba, aliyekuja kusema ni mke wa kaka yangu baada ya kugundua simu za broo hazipo sawa, shemeji kaniambia ukweli, nimewashirikisha kaka zangu wengine wamefedheheka sana na tukio lilivyo na tunaona aibu sana japo mhusika haoni shida yoyote Wala haonekani kujali na kibaya zaidi nilipo jaribu kumuliza alikubali na akanihidi atamfanya yule mwanamke mke mdogo na eti itasaidia atakuwa anarudi kule tukuyu na kupita mara nyingi akitoka kwenye biashara zake .

Anadai Atamuacha pale yule mwanamke na anadai anataka amfungulie duka kule kule kwenye kamji kadogo kanaitwa lwangwa, hapa tupo njia panda tunafanyaje, je yule mwanamke sisi tutakuwa tunamwitaje shemeji au mama mdogo kama tulivyozoea , vipi Ile jamii kule wakijua itakuwaje? Wale ndugu zetu kule Kijijini watakuwa wanatuonaje wakija kujua. Je, baba mdogo atakuwa ametuweka kwenye kundi gani, mke wa bab mdogo atakuwa anatufikiriaje je tutakuwa tunamwita mama mdogo au shemeji na kwa mila za Kinyakyusa hilo lipoje au tujiandae tu kurogwa?
 
Ipo hivi miaka kama kumi nyuma , baada ya baba yangu kufariki, tuliitwa na shangazi zetu tukapelekwa huko tukuyu busokelo tukapewa mji na kuambiwa sisi ndio tutakaoutunza mji ,sababu ni baba yetu alikuwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia Yao ya watoto watu, na mbaya zaidi shangazi zetu hawapo hapa Tanzania mmoja kaolewa zambia na mwingine yupo zake uingereza kwa miaka mingi sasa,..... Baada ya kupewa mji tukuyu ilibidi tukae vikao na ndugu zetu na tukajaribu kuwaeleza kuwa kwa hali ulivyo itakuwa ngumu sisi kurudi tukuyu kwa sababu sie pia tumetawanyika na nyumbani njombe hapana mtu zaidi ya mama na mimi, so management ya tukuyu itakuwa technically taff, kwenye mazungumzo tukamuomba baba yetu mdogo kwenye ukoo( baba yake alikuwa ni babu yetu mdogo walifuatana na babu yetu mzaa baba) baba yetu alijaribu kukata kwa sababu na yeye anaishi mbeya mjini na kajipata sana, baada ya kumsihi sana akatupa option kuwa mbeya kwake yupo na shemeji yake wa like ( mdogo wa mke wake kabisa) akatueleza huyo shemeji yake ndoa yake ilivunjika akiwa na watoto wawili, yupo tu mjini ). Tukamuomba basi yeye ndiye akae pale ,kweli akakubali, so akahamia pale nilichokifanya nikapeleka mifugo na kumpatia mtaji kidogo wa kuendesha maisha kule kijijini. Shida ilianzia hapa mwaka 2022 kaka yetu mkubwa akatushauri December lazima twende kule kijijini , kweli tulienda tukaa tukaona mazingira sio rafiki sana so tukazimia tujenge nyumba inayoendana na miaka ya sasa , kweli tukachangishana then tukaanza ujenzi wa msingi, baada ya kuondoka tukawa tumeazimia nyumba iishe kabla ya December 2023 , tukawa tumechangishana na kaka yangu tuliyefuatana akajitolea ataifanyia nyumba finishing na atamaliza Kila kitu, basi ilipofika December akashuka kule tukuyu na mafundi wake Toka dar , kweli alijenga nyumba hadi na kuanza kufanya finishings ** kumbe akiwa kule akawa anajipigia yule mama yetu pale , what happen there ni mimba na yule mwanamke ana mimba ,aliyekuja kusema ni mke wa kaka yangu baada ya kugundua simu za bros hazipo sawa , shemeji kaniambia ukweli , nimewashirikisha kaka zangu wengine wamefedheheka sana na tukio lilivyo na tunaona aibu sana japo mhusika haonni shida n kaniambia atamfanya yule mwanamke mke mdogo atamuacha pale na anadai anataka amfungulie duka kule kule kwenye kamji kadogo kanaitwa lwangwa , hapa tupo njia panda tunafanyaje , vipi Ile jamii kule wakijua itakuwaje na je kwa mila za kinyakyusa Hilo lipoje au tujiandae tu kurogwa
Kuna laana zakifamilia ni ngumu kuziondoa mpaka ufanye kafara ya kuchinja .
 
Wala haina shida, ungejua mila za kinyakyusa miaka 50 tu nyuma ungezimia.

Ilikuwa hivi, kama baba yako akifariki basi unarithi mali zake zote pamoja na wake zake wadogo (wazee walikuwa na wake wengi).

Hao wake wadogo unazaa nao kabisa, lakini watoto wanahesabiwa kuwa wa baba yako, yaani wanakuwa wadogo zako kimila japo ni wa kwako kabisa.

Hii ilikuwa pia kwa wake za kaka zako. Japo mwanamke alikuwa na uhuru wa kukataa ila wengi walikuwa wanakubali.

Sasa huyo unayemwita mama mdogo wala hamna undugu naye wa damu, acha bro ale mema ya nchi.
 
Bro wako alichelewa sana kuwa na mke wa kijijini, yani lazima kijijini uwe na mji na mke sasa vijinja nani ataangalia na kung'olea migomba na amasimbi? Oya ukija tena nicheki uwa naenda sana luteba kule wanyakyusa wa kule wana pedigree nzuri sana za ng'ombe wa maziwa waliwaibia kitulo enzi hizo. Kyala akutule
 
Ipo hivi miaka kama kumi nyuma , baada ya baba yangu kufariki, tuliitwa na shangazi zetu tukapelekwa huko tukuyu busokelo tukapewa mji na kuambiwa sisi ndio tutakaoutunza mji ,sababu ni baba yetu alikuwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia Yao ya watoto watu, na mbaya zaidi shangazi zetu hawapo hapa Tanzania mmoja kaolewa zambia na mwingine yupo zake uingereza kwa miaka mingi sasa,..... Baada ya kupewa mji tukuyu ilibidi tukae vikao na ndugu zetu na tukajaribu kuwaeleza kuwa kwa hali ulivyo itakuwa ngumu sisi kurudi tukuyu kwa sababu sie pia tumetawanyika na nyumbani njombe hapana mtu zaidi ya mama na mimi, so management ya tukuyu itakuwa technically taff, kwenye mazungumzo tukamuomba baba yetu mdogo kwenye ukoo( baba yake alikuwa ni babu yetu mdogo walifuatana na babu yetu mzaa baba) baba yetu alijaribu kukata kwa sababu na yeye anaishi mbeya mjini na kajipata sana, baada ya kumsihi sana akatupa option kuwa mbeya kwake yupo na shemeji yake wa kike ( mdogo wa mke wake kabisa) akatueleza huyo shemeji yake ndoa yake ilivunjika akiwa na watoto wawili, yupo tu mjini ). Tukamuomba basi yeye ndiye akae pale ,kweli akakubali, so akahamia pale nilichokifanya nikapeleka mifugo na kumpatia mtaji kidogo wa kuendesha maisha kule kijijini.(lengo la kupeleka mifugo ni kufanya mji uwe active pasionakane pametupwa kabisa) Shida ilianzia hapa mwaka 2022 kaka yetu mkubwa akatushauri December lazima twende kule kijijini , kweli tulienda tukaa tukaona mazingira sio rafiki sana so tukazimia tujenge nyumba inayoendana na miaka ya sasa , kweli tukachangishana then tukaanza ujenzi wa msingi, baada ya kuondoka tukawa tumeazimia nyumba iishe kabla ya December 2023 , tukawa tumechangishana na kaka yangu tuliyefuatana akajitolea ataifanyia nyumba finishing na atamaliza Kila kitu, basi ilipofika December akashuka kule tukuyu na mafundi wake Toka dar , kweli alijenga nyumba na kuanza kufanya finishings ** kumbe akiwa kule akawa anajipigia yule mama yetu pale , what happen there ni mimba na yule mwanamke ana mimba ,aliyekuja kusema ni mke wa kaka yangu baada ya kugundua simu za bros hazipo sawa , shemeji kaniambia ukweli , nimewashirikisha kaka zangu wengine wamefedheheka sana na tukio lilivyo na tunaona aibu sana japo mhusika haonni shida n kaniambia atamfanya yule mwanamke mke mdogo atamuacha pale na anadai anataka amfungulie duka kule kule kwenye kamji kadogo kanaitwa lwangwa , hapa tupo njia panda tunafanyaje , vipi Ile jamii kule wakijua itakuwaje, wale ndugu zetu kule kijijini watakuwa wanatuonaje wakija kujua, je baba mdogo atakuwa ametuweka kwenye kundi gani na je kwa mila za kinyakyusa Hilo lipoje au tujiandae tu kurogwa
Haina shida hii kwa desturi za kitanzania!
Kwanza ni shemeji wa baba mdogo! Hajazaliwa tumbo moja na wazazi wenu ( kwa maana ya kupokezana ziwa) huyo sawa na binamu hata kuoa unaoa kabisa kilichobaki ni kuweka mambo sawa na mke wa sasa aendelee kula mema ya Tunda!
 
Back
Top Bottom