Kaka yangu kamtia mimba mama yetu mdogo. Hili lipoje kwa Wanyakyusa?

Kaka yangu kamtia mimba mama yetu mdogo. Hili lipoje kwa Wanyakyusa?

Katika watu ambao hawaruhusiwi kuwaoa ni kina mama wadogo, Shangazi, watoto kaka au wadogo zako maana hiyo ni laana.
Mbona hamsemi Putin atapata laana gani,haya mambo ya laana ni mzigo
 
Mama mdogo ni nduguu, maana unaweza nyonya ziwa lake, pindi mama mzazi akiwa hayupoo!! Kosa kubwa hili.
Kwa nilivyomuelewa huyo anayemuita mama mdogo (aliyejazwa) ni shemeji wa baba ake mdogo yaani mdogo wa mke wa baba ake mdogo aishie huko mjini mbeya.
Huyo mamdogo sio wa kumzaa ametoka koo ingine huko. Sema tu itakuwa siyo heshima kwa baba mdogo na familia yake.
 
Bro alipewa uno la tukuyu+mlo wa ndizi unakuta kitu nta nta na lile baridi ,lazima umwagilizie bustani ndani ya fensi,,,,halafu za kuku wa kienyeji zinashawishi sana kutembea pekupeku,,,......kongole kwa blaza
 
Ipo hivi miaka kama kumi nyuma , baada ya baba yangu kufariki, tuliitwa na shangazi zetu tukapelekwa huko tukuyu busokelo tukapewa mji na kuambiwa sisi ndio tutakaoutunza mji ,sababu ni baba yetu alikuwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia Yao ya watoto watu, na mbaya zaidi shangazi zetu hawapo hapa Tanzania mmoja kaolewa zambia na mwingine yupo zake uingereza kwa miaka mingi sasa,..... Baada ya kupewa mji tukuyu ilibidi tukae vikao na ndugu zetu na tukajaribu kuwaeleza kuwa kwa hali ulivyo itakuwa ngumu sisi kurudi tukuyu kwa sababu sie pia tumetawanyika na nyumbani njombe hapana mtu zaidi ya mama na mimi, so management ya tukuyu itakuwa technically taff, kwenye mazungumzo tukamuomba baba yetu mdogo kwenye ukoo( baba yake alikuwa ni babu yetu mdogo walifuatana na babu yetu mzaa baba) baba yetu alijaribu kukata kwa sababu na yeye anaishi mbeya mjini na kajipata sana, baada ya kumsihi sana akatupa option kuwa mbeya kwake yupo na shemeji yake wa kike ( mdogo wa mke wake kabisa) akatueleza huyo shemeji yake ndoa yake ilivunjika akiwa na watoto wawili, yupo tu mjini ). Tukamuomba basi yeye ndiye akae pale ,kweli akakubali, so akahamia pale nilichokifanya nikapeleka mifugo na kumpatia mtaji kidogo wa kuendesha maisha kule kijijini.(lengo la kupeleka mifugo ni kufanya mji uwe active pasionakane pametupwa kabisa) Shida ilianzia hapa mwaka 2022 kaka yetu mkubwa akatushauri December lazima twende kule kijijini , kweli tulienda tukaa tukaona mazingira sio rafiki sana so tukazimia tujenge nyumba inayoendana na miaka ya sasa , kweli tukachangishana then tukaanza ujenzi wa msingi, baada ya kuondoka tukawa tumeazimia nyumba iishe kabla ya December 2023 , tukawa tumechangishana na kaka yangu tuliyefuatana akajitolea ataifanyia nyumba finishing na atamaliza Kila kitu, basi ilipofika December akashuka kule tukuyu na mafundi wake Toka dar , kweli alijenga nyumba na kuanza kufanya finishings ** kumbe akiwa kule akawa anajipigia yule mama yetu pale , what happen there ni mimba na yule mwanamke ana mimba ,aliyekuja kusema ni mke wa kaka yangu baada ya kugundua simu za bros hazipo sawa , shemeji kaniambia ukweli , nimewashirikisha kaka zangu wengine wamefedheheka sana na tukio lilivyo na tunaona aibu sana japo mhusika haonni shida n kaniambia atamfanya yule mwanamke mke mdogo atamuacha pale na anadai anataka amfungulie duka kule kule kwenye kamji kadogo kanaitwa lwangwa , hapa tupo njia panda tunafanyaje , vipi Ile jamii kule wakijua itakuwaje, wale ndugu zetu kule kijijini watakuwa wanatuonaje wakija kujua, je baba mdogo atakuwa ametuweka kwenye kundi gani na je kwa mila za kinyakyusa Hilo lipoje au tujiandae tu kurogwa
Ni watu wazima msiumize kichwa waacheni
 
Haina shida hii kwa desturi za kitanzania!
Kwanza ni shemeji wa baba mdogo! Hajazaliwa tumbo moja na wazazi wenu ( kwa maana ya kupokezana ziwa) huyo sawa na binamu hata kuoa unaoa kabisa kilichobaki ni kuweka mambo sawa na mke wa sasa aendelee kula mema ya Tunda!
Binamu inakuwa na aibu na maswali mengi ila huyu mamdogo wa kujuana naye baada ya dada ake kuolewa na baba mdogo mbali saaana
 
kama nimesoma kwa usahihi ni kwamba kaka yako amempa mimba mdogo wa mke wa baba yenu mdogo(ambaye naye siyo baba mdogo wa moja kwa moja ni mtoto wa Babu mdogo)

hapo hakuna undugu wowote Mimi nilidhani hata ametembea na huyo mke wa baba mdogo
 
Back
Top Bottom