Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.
Mama mkubwa ametuambia karogwa na mke wake sisi kama ndugu tutafute mganga tumnasue maana huenda kapewa rimbwata. Huwezi sahau nyumbani kwenu ukawa unatunza watu ambao sio nduguzo, kwanini Hao watoto wasipewe hela na ndugu zao huko halafu waje kwa kaka etu kuwa ombaomba, kila nikienda kumsalimia broo nawakuta wapo, kila rikizo za shule na vyuo wakifunga wanaenda kwa broo.
Halafu utasikia shemeji shemeji, shemeji ya minyoko. Kuna siku miaka mitatu nyuma nilikwazika kweli, niliomba pesa ya ada akasema hawezi nipa mkononi akaenda benki akalipia, ila ndugu wa mke wake akitaka pesa ya Ada anampa cash in hand ila mimi haniamini. Binafsi nimeacha hata kwenda kumsalimia ila ipo siku atanikumbuka tu
Fikra za kimasikini sana ndugu yangu. Kwanini unasubiri kusaidiwa je una kilema chochote? Kwanini wewe usiwe ndiye msaidiaji
Inawezekana kabisa tatizo likawa ni nyie ndugu na wala sio kaka zenu. Huwezi kuwa na ndugu tegemezi maana ukishafanya makosa ya ndugu kukutegemea basi watakutegemea maisha yao yote. Sehemu ambayo ni muhimu kusaidiana kama ndugu ni kwenye elimu tu. Lakini sijui miradi ya biashara au pesa za kujikimu wakati upo mtaani nashauri usisaide kabisa ndugu