Kaka yetu anasaidia ndugu wa mke wake, sisi hatusaidii

Kaka yetu anasaidia ndugu wa mke wake, sisi hatusaidii

Fikra za kimasikini sana ndugu yangu. Kwanini unasubiri kusaidiwa je una kilema chochote? Kwanini wewe usiwe ndiye msaidiaji

Inawezekana kabisa tatizo likawa ni nyie ndugu na wala sio kaka zenu. Huwezi kuwa na ndugu tegemezi maana ukishafanya makosa ya ndugu kukutegemea basi watakutegemea maisha yao yote. Sehemu ambayo ni muhimu kusaidiana kama ndugu ni kwenye elimu tu. Lakini sijui miradi ya biashara au pesa za kujikimu wakati upo mtaani nashauri usisaide kabisa ndugu
Hii ni kweli kabisa

Halafu wanaona kama.ni haki yao kuwapa fedha ya kujikimu
 
Kuna workmate mmoja naye anasomesha wadogo wa mkewe sasa hivi aliyenaye ni wanne, mmoja kamaliza Chuo (alianza kumsomesha toka kidato Cha kwanza), wa pili naye yuko chuo na huyu watatu yupo sekondari. Ajabu wadogo zake wakija kusoma wanaishia kukaa mwaka kisha wanaondoka.

Hili limenifikirisha sana na kuapa kuwa wa kwanza kumhudumia ni ndugu yangu wa tumbo moja. Hata wakiwa wakorofi damu ni nzito kuliko maji. Hawa hawakuachi kwenye shida.
 
Mpwanyungu,Mpwanyungu,Mpwanyungu nimekuita mara3 pambana upate vya kwako
1658513606202.jpg
 
Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.

Mama mkubwa ametuambia karogwa na mke wake sisi kama ndugu tutafute mganga tumnasue maana huenda kapewa rimbwata. Huwezi sahau nyumbani kwenu ukawa unatunza watu ambao sio nduguzo, kwanini Hao watoto wasipewe hela na ndugu zao huko halafu waje kwa kaka etu kuwa ombaomba, kila nikienda kumsalimia broo nawakuta wapo, kila rikizo za shule na vyuo wakifunga wanaenda kwa broo.

Halafu utasikia shemeji shemeji, shemeji ya minyoko. Kuna siku miaka mitatu nyuma nilikwazika kweli, niliomba pesa ya ada akasema hawezi nipa mkononi akaenda benki akalipia, ila ndugu wa mke wake akitaka pesa ya Ada anampa cash in hand ila mimi haniamini. Binafsi nimeacha hata kwenda kumsalimia ila ipo siku atanikumbuka tu
Dah kitu kilicho nishinda mm nikumuomba ndugu yangu anisaidie! Atakam ninashida vep siwez kumuomba bola nife2 nashida zangu japo brother ang anauwezo mkubwatu wakimaisha
 
Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.

Mama mkubwa ametuambia karogwa na mke wake sisi kama ndugu tutafute mganga tumnasue maana huenda kapewa rimbwata. Huwezi sahau nyumbani kwenu ukawa unatunza watu ambao sio nduguzo, kwanini Hao watoto wasipewe hela na ndugu zao huko halafu waje kwa kaka etu kuwa ombaomba, kila nikienda kumsalimia broo nawakuta wapo, kila rikizo za shule na vyuo wakifunga wanaenda kwa broo.

Halafu utasikia shemeji shemeji, shemeji ya minyoko. Kuna siku miaka mitatu nyuma nilikwazika kweli, niliomba pesa ya ada akasema hawezi nipa mkononi akaenda benki akalipia, ila ndugu wa mke wake akitaka pesa ya Ada anampa cash in hand ila mimi haniamini. Binafsi nimeacha hata kwenda kumsalimia ila ipo siku atanikumbuka tu

Ndugu wengi kama si wote wa mwanamke pamoja na mwanamke mwenyewe wanahisi kuwa ni haki yao kuishi kwa mme wa dada yao na ni kwamba wanahaki zaidi ya kuliko ndugu wa mume na wanafikiri ni wajibu wa mwanaume wa ndugu yao kuwasaidia yaani wanafikiri ni lazima na ni wajibu wako wewe mwanaume kuwasaidia stupid mwanaume yoyoe unao soma ujumbe huu tambua na ujitambue sio wajibu wako na si lazima kusaidia ndugu wa mke ni hiari wewe umeoa mke huyu mkeo ndio wajibu wako kumtunza kumlinda kumvisha na kila kitu kinacho husu binadamu kuishi wanafuata watoto mkijaariwa ikiwa umetoka familia masikini basi wazazi wako ni namba 3 wanafuata ndugu zako kwa kiasi na wazazi wa mke kwa kiasi halafu ndugu wa mke kwa hiari labda narudia tena labda huyu mwanamke awe na kazi yake eidha kwa elimu alio someshwa na wazazi wake au ndugu zake ikapelekea awe na kipato chake binfsi hapo utawajibika kwa ku balance kipato chake ndio kifanye shughuri hiyo ya misaada ya ndugu zake na ukitaka amanina kuishi kwa upendo na mkeo epuka kukaa na wazazi wako ndugu zako au ndugu wa mkeo au wazazi wake nyumbani kwako
 
Kuna workmate mmoja naye anasomesha wadogo wa mkewe sasa hivi aliyenaye ni wanne, mmoja kamaliza Chuo (alianza kumsomesha toka kidato Cha kwanza), wa pili naye yuko chuo na huyu watatu yupo sekondari. Ajabu wadogo zake wakija kusoma wanaishia kukaa mwaka kisha wanaondoka.

Hili limenifikirisha sana na kuapa kuwa wa kwanza kumhudumia ni ndugu yangu wa tumbo moja. Hata wakiwa wakorofi damu ni nzito kuliko maji. Hawa hawakuachi kwenye shida.
Wengi hawatakuelewa maana akili zao nizakike
 
Mimi binafsi maisha ya kuomba pesa kwa ndugu kwa namna yeyote nilisha jipiga marufuku .... tafta pesa zako kwa jasho lako

1: Kwanza utaheshimika nyumbani
2:Utakuwa na uhuru nazo
3: Utaepuka dharau zisizo na msingi

Nakusisitiza wewe na nduguzako wengine tafteni pesa zenu kwa jasho lenu omba omba huleta unyonge hasa kwa watoto wakiume ..... umenielewa meku???
😂😂😂😂🤩🤩🤩🤩
 
Back
Top Bottom