Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Pale uliposema kama mmetoka Mbwinde, umenikumbusha shemeji yangu wa kike kijiji alichozaliwa kinaitwa Umbwinde, basi anajisifu utamsikia, "mimi ndiyo wa Umbwinde, nimeoga maji ya mto mimi".Jamani najua mko poa!
Hivi siku hizi kila kaka huku mjini naona kabeba begi mgongoni, hayo mabebi ni makubwaa sana, na yamekaa kishamba shamba hivi. Mengi Yao yameandikwa Biowang mengine Marcello, yaani unakuta mkaka mzuri, msafii kapendeza halafu kabeba li Biowang mgongoni, hivi mnawekaga nini humo jamani?
Itoshe kusema tu hayawapendezi, mnaharibu Sana muonekano wenu na hayo ma Biowang mnakuwa kama mmetoka Mbwinde bwana.
Hata kama ni laptops tafuteni mabegi mazuri, kwanza wengine hamna hata laptops kuna makaratasi tu humo, basi tu Tanzania likizuka Jambo basi ni nongwa kama wadada na vijora.
Acheni kumtajirisha Biowang na Marcello.
Asante kwa kuelewa
Wanawake huwa mnakosea mnapofikiri sisi wanaume ni kama nyinyi..
Namaanisha;
Mwanaume halisi havai nguo au kubeba begi ili kupendeza, tunabeba begi kwa kuwa lina accomplish kazi fulani. Tofauti na nyie mnabeba mikoba ili kupendeza tena hadi unamechisha rangi.
Mwanaume halisi havai au kubeba mkoba ili fasheni, yaani kwa kufuata fasheni, ukiona mwanaume anapenda kufuata fasheni, kutakuwa kuna tatizo mahali.
I REST MY CASE.