Kaka zetu, hayo mabegi ni vipi kwani?

Pale uliposema kama mmetoka Mbwinde, umenikumbusha shemeji yangu wa kike kijiji alichozaliwa kinaitwa Umbwinde, basi anajisifu utamsikia, "mimi ndiyo wa Umbwinde, nimeoga maji ya mto mimi".

Wanawake huwa mnakosea mnapofikiri sisi wanaume ni kama nyinyi..

Namaanisha;
Mwanaume halisi havai nguo au kubeba begi ili kupendeza, tunabeba begi kwa kuwa lina accomplish kazi fulani. Tofauti na nyie mnabeba mikoba ili kupendeza tena hadi unamechisha rangi.

Mwanaume halisi havai au kubeba mkoba ili fasheni, yaani kwa kufuata fasheni, ukiona mwanaume anapenda kufuata fasheni, kutakuwa kuna tatizo mahali.

I REST MY CASE.
 
Dada wengine sie mafundi kuna
Nyundo
Misumeno
Kono bao
Pipe level
Na sometime hata randa. [emoji39][emoji39][emoji39]
 
Dada wengine sie mafundi kuna
Nyundo
Misumeno
Kono bao
Pipe level
Na sometime hata randa. [emoji39][emoji39][emoji39]
Wewe beba,Tena kwa kutamba,tatizo Ni wale wa benki😂
 
Nimempenda shemeji yako anajua kuthamini mbwinde kwao!😂😂 mwingine angejifanya hapajui Mbwinde..
 
Nimempenda shemeji yako anajua kuthamini mbwinde kwao!😂😂 mwingine angejifanya hapajui Mbwinde..
Usiombe!

Umbwinde ni 'intiria' kinoma mwanangu, unapita Sisitira unapandisha milimani. Kule huwezi kwenda na pikipiki, hata kwa baisikeli njia za kupita ni chache na kwa tabu, kule ni kwa miguu tu halafu wananchi kule bado wanatembea pekupeku tu kwenye michanga, unaweza ukadhani umekutana na Mrisho Mpoto, kumbe ni kitu laivu bila chenga!!

Lakini shemeji yangu humuambii kitu, akija Dar ni kujivunia tu, utasikia, " Mimi mzuri shemeji, wa Umbwinde mimi, nimeoga maji ya mtoni!"
 
Aisee wapo wachache Sana!hongera zake nyingi
 
Pamoja na mvuto tulionao humo ndani tunaweka VIPORO na MAJI YA BOMBA....maisha ya mjini ni changamoto shostito!

#Siempre JMT🙏
 
Pamoja na mvuto tulionao humo ndani tunaweka VIPORO na MAJI YA BOMBA....maisha ya mjini ni changamoto shostito!

#Siempre JMT🙏
Ewaaaa!, Umeongea ukweli wa wazi sana, siku hizi kula mgahawani bajeti inakaba, wakati wa kwenda kazini unajaza kabisa kwenye hotpot maharage na wali, muda wa lanchi wewe unafungua zipu ya begi tu, unaanza kukandamiza..
 
Swadaktaaaa👍
 
Mnazunguka tu ila tatizo uchumi hizo bag za biowing bei zake n rahis cheap Sana kwa sis wafanya kaz ngumu zinatusaidia Sana
 
Na bado kuna yale ya CPA, haha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…