Kakolanya atendewe haki

Kakolanya atendewe haki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Haiwezekani mchezaji anayedai haki zake atelekezwe tu hivihivi huku TFF inakodoa macho tu , huu ni zaidi ya uonevu .
 
Haki yoyote inadaiwa kwa utaratibu mkuu,,, c kwa kukiuka utaratibu,,,,, wachezaji weng wanadai stahiki zao ila kwa utaratibu maalum
Binafc nampongeza kocha kwa alichokifanya kwa kakolanya na ni funzo tosha kwa wachezaj wengine,,,,
Dirisha limefungwa,,, na kocha hamtak,, nadhan avunje tu mkataba
 
Kabla ya kuvunja mkataba mlipeni haki zake , kwanza mkataba mlishauvunja kitambo baada ya kukiuka makubaliano
 
Haiwezekani mchezaji anayedai haki zake atelekezwe tu hivihivi huku TFF inakodoa macho tu , huu ni zaidi ya uonevu .
Ni sahihi kudai haki yake, lakini kanuni ya dhahabu (golden rule) ni kutochukua sheria mikononi. Ndio maana unapomdhuru mwizi wa mali yako unaadhibiwa licha ya kuwa mwizi huyo alikukosea. Lakini usisahau na mwalimu naye anastahiki kutendewa haki na mchezaji. Kutoweka kambini bila ya kuwasiliana naye ni kumnyima haki hiyo. Naye ana haki ya kuidai, na ndivyo alivyofanya. Kwamba ili aridhike, mchezaji huyo atafutiwe timu nyengine au yeye aondoke. Kumbuka hajamfukuza Kakolanya, ameupa uongozi chaguo (options). Kwa hivyo mkuu si sahihi kusema kwamba Kakolanya kafukuzwa kwa kudai haki yake, la hasha. Ni kwamba Kakolanya amemkosea Mwalim na klabu ikaridhika na pendekezo la kuondoka yeye badala ya Mwalim. Klabu haijakataa kwamba anaidai haki zake, wala haiwezi kukwepa wajibu wa kumlipa.
Aidha, hiyo TFF unayoisema ingekuwa katika nafasi bora zaidi ya kumtetea kama angekimbilia huko kabla ya kuchukua sheria mikononi mwake. Mtu akishafariki hatibiwi, hufanyiwa uchunguzi kujua sababu ya kifo. Kakolanya ndiyo alishatoroka kwenye timu yake, TFF haiwezi kusema kuwa hakutoroka madhali uamuzi wa kutoroka haukufanywa kwa amri wala ridhaaa ya TFF ambayo haikuwa hata na Taarifa ya awali kwamba mchezaji mwenyewe amedhamiria kususia. Kwa hivyo haiwezi kuingilia swala la kitaratibu baina ya mchezaji na Mwalim. Inaweza tu kufanya uchunguzi juu ya ukubwa wa kosa lenyewe ili isaidie kuwashauri vizuri wasusiaji watarajiwa, lakini haiwezi kutia mkono maamuzi ya Mwalim wa timu iliyotorokwa.
 
Yanga ndiyo inayotakiwa kuvunja mkataba au 'kumfukuza' ili mwakani akatafute timu nyingine, kwa kiwango alichonacho hawezi kukosa timu! huyu mchezaji amenyanyasika sana ndani yanga, mbona kocha huyo huyo alikubali kuwapokea yondani, ajibu, shishimbi hawa wotee walikuwa na kesi kama ya kakolanya na 'wadau' wakawatimizia madai yao tena kwa noti ndefu kuliko hizo mil2 za kakolanya!......mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
Haiwezekani mchezaji anayedai haki zake atelekezwe tu hivihivi huku TFF inakodoa macho tu , huu ni zaidi ya uonevu .
Wewe ni mpenzi wa simba na JPM hater acha yanga wagange yao! Umemsikia coach kama bado endelea
 
Kabla ya kuvunja mkataba mlipeni haki zake , kwanza mkataba mlishauvunja kitambo baada ya kukiuka makubaliano
Do not be that much biased, coach hawezi vunja mkataba! Unajua agent wa kalolanya ni simba! It seems mna ajenda ya siri kuihujumu yanga kama mnavyomhujumu JPM
 
Yanga ndiyo inayotakiwa kuvunja mkataba au 'kumfukuza' ili mwakani akatafute timu nyingine, kwa kiwango alichonacho hawezi kukosa timu! huyu mchezaji amenyanyasika sana ndani yanga, mbona kocha huyo huyo alikubali kuwapokea yondani, ajibu, shishimbi hawa wotee walikuwa na kesi kama ya kakolanya na 'wadau' wakawatimizia madai yao tena kwa noti ndefu kuliko hizo mil2 za kakolanya!......mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Coach aliwaeleza wengine wakarudi yeye kajifanya kichwa ngumu! I believe kama tungekuwa na Macoach kama zahera Mpira wa TZ ungekua
 
Do not be that much biased, coach hawezi vunja mkataba! Unajua agent wa kalolanya ni simba! It seems mna ajenda ya siri kuihujumu yanga kama mnavyomhujumu JPM
huyo jpm anajihujumu mwenyewe kwa kujifanya mjuaji
 
Hayo mapungufu yako! He is the president and as long bado ni president jaribuni kumheshimu kama wamarekani wanavyomheshimu trump! Mna roho ya kwanini yeye si Lowasa tangu mwanzo
 
Twende jukwaa la siasa mkuu , huku si mahali pake , bali unachotakiwa kufahamu ni kwamba hatumchukii JPM peke yake , watanzania wote kwa umoja wetu hatuitaki ccm na makandokando yake kwa ujumla ukiwemo wewe
 
Mkuu sasa huku Siasa za nn? Si ungemfuata pm
 
Back
Top Bottom