Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Hapana jamii iendelee hivi hivi kuwanyooshea vidole ili mabinti wasiozaa wapate ari zaidi ya kujitunza kwa kutambua thamani yao kama wanawake. Kazi ya kuwasimanga Single mothers iendelee kwa kweli.
 
Kabisa,sio wanarukaruka kama bisi Tu hapa
 
Hii ni ishu ya Probability chance. Kinachoangaliwa ni je,kipi kina uwezekano mkubwa zaidi wa kutokea?. Kati ya Mzazi wa hovyo kulea watoto hovyo au Mzazi muadilifu kulea watoto hovyo au Mzazi wa hovyo kulea watoto waadilifu au Mzazi muadilifu kulea watoto hovyo?
 
Sio uchoy na roho mbaya. Acheni zinaa, ukifanya zinaa tegemea mimba, acheni zinaa sbr mfunge ndoa.
 
Janiffer, kua mkweli kama.ni wewe unakubali kuolewa na mwanaume tyr ana mtoto ? Ukijua kabisa akishakuoa yule mtoto mtakua mnaish nae nyumba moja ??
 
Hawawezi kuelewa kama wanareason kwa hisia badala ya uhalisia
 
Kiwanja tayari Kina risk kubwa ya kuwa na Migogoro..!

Aongeze Maombi.. !

Mara nyingi Singo Maza huolewa na Wanaofanana nao yaani Singo Faza. Wote wakijaaliwa watoto Kwenye ndoa hawaanzii Moja Kuhesabu..!
Na tatizo la single mom wengi nao huwa hawataki au hawapendi kuolewa na single Dad! Hapo ndiyo mziki mnene unawasumbua!!
 
Kama ninyi wanawake mnavyokuwa wagumu kutuelewa kuanzia maisha ya chini ya kulala sakafuni na sisi ni ngumu kuwaelewa story ya kuwa na mtoto halafu mnasema ilikuwa ni bahati mbaya au hamkuwa mkijitambua.

Yaani wewe ulale na mtu usijui matokeo yake kweli kama sio kufanyana vilaza ni nini basi hapo?
 
Hii nguvu vijana tunayoitumia kuwashambulia warembo walio single maza tungeiwekkeza kuwashambulia na kuwakataaa CCM na kazi zao zote hii nchi tungekuwa zaidi ya Nchi za scandinavia
Aliyekwambia ugomvi wa vijana na CCM ni wakimahusiano ya kimapenzi na watoto wa nje ya ndoa ni nani?! Yaani unashindwa kutofautisha Siasa na Mapenzi.
 
Kwahiyo unataka kusema wanaume wa kisukuma hawana akili timamu si ndio?! Ngoja waje hapa.
 
Legezeni masharti mtatuua.....iwe tu hakuna mawasiliano basi walau
Hamna kitu cha namna hiyo. Hivi vitu mnachukulia poa sana ila vina madhara makubwa sana upande wa mwanaume kwa baadae. Kama wewe unahisi ni sawa then kutana na mwanaume hana hata mia mbovu halafu anzisha nae mahusiano na awe na watoto wake amepata na mwanamke mwingine au wanawake wengine, then wewe na yeye mpate watoto wenu then uwalee wote kama wanao huku na wewe ukichangia 50% ya gharama kuwasomesha kuwalisha, kuwavalisha na matunzo mengine.
 
Hivi hili swala singo faza huwa haliwahusu eeh
Single father umewahi sikia wapi? Mwanamke unapoanzisha mahusiano kindezi then huyo mtoto ni project yako wewe by 90% utadirect wewe sio mwanaume.

Na mwanaume akiwa anapenda sana mtoto wake hadi akamchukua yeye hautamuona kwako wewe mwanamke labda akishakuwa mkubwa, ila mtoto atalelewa upande wao kwa bibi yake na hautasikia kuna mwanamke anapiga simu kwako kukwambia chochote so utakuwa free.
 
Ni saba sio mitano. Mtoto anatakiwa kwenda kwa baba yake kuanzia miaka 7 kuendelea.
 
Mwanaume anaposimamia maslahi yake anaitwa mvulana, sijui utoto hajakua, mara hajitambui, au hawezi majukumu yaani maneno kadha wa kadha ili mradi tu kuprove nadharia kuwa mwanaume anatakiwa kubeba mizigo ya mwanamke hata kama haimhusu, huu ni upuuzi wa kihistoria ambao vijana wa sasa wanaukataa sababu wameshaona madhara yake.

Wanawake jamii imewafichia makucha sana especially maeneo ambayo wanakosea kwa makusudi na kujivika sura ya uhanga wa kusababishiwa kwamba haikuwa dhamira yao kukosea jambo ambalo si kweli.

Ukitaka uone makusudi ya watoto wa kike tazama hawa mabinti wa sasa age kuanzia 16 hadi 25 watazame matendo yao halafu jaribu kukaa nao chini uongee nao kuwapa nasaa na kukemea tabia zao. Kama sio kukuona una akili za kizee na kukijibu kwa kejeli na dharau basi watakaa kimya na kujifanya wamekuelewa kumbe moyoni na akilini ameshakupuuza.

Kuna binti alikuwa na miaka 21 anatoka na jamaa ana miaka 38 amejikoleza mbaya. Jamaa ameshazaa na wanawake watatu na kawatelekeza na watoto wao. Binti akaenda kuishi kabisa kwa jamaa eti anashindana na kuwakomesha wanawake waliokuwapo kimahusiano na mwanaume previously, kisa jamaa alikuwa kampangishia chumba akimlipia kodi na akamuweka katika duka lake auzee.

Tena mojawapo ya hao wadada alimfuata kwa busara kabisa kama mdogo wake akamwambia mdogo wangu mimi ni mkubwa sana kwako nakushauri kama dada yako nisikilize, achana na huyu mwanaume atakuharibia future yako wewe ni binti mdogo, tafuta mwenzako ambaye mtaweza jenga malengo pamoja na mtalewana huyu hakufai anakutumia tu sababu ya uzuri wako. Binti alimpuuza. Akaona wanamuonea gere, akaamua kujibebesha ujauzito wa jamaa as if mwenzake anashida na watoto zaidi.

Fast Forward leo hii, binti ana hali ngumu hawana maelewano na jamaa ananipigia simu na kunielezea tamthiria ya vituko anavyofanyiwa na jamaa na namna anajipanga sasa kutafuta mtu serious ili waanze mahusiano serious [emoji23][emoji23].

Mwingine nilikaa nae chini akiwa na miaka 21,ni mdogo wangu ambaye nasali nae jumuiya. Nilimsihi asije kuingia mahusiano na mume wa mtu au mtu mzima mwenye familia maana ndizo story alikuwa analeta sana. Aiseeee karudia huko huko tena. Nakuja mkuta ana mtoto amepata na kijana ambaye anafamilia yake ya watoto wawili na mke wa ndoa kabisa.

Sasa namtazama nasema huwa ni hamsikii au huwa mnataka kuona ladha ya ujinga kwenye matendo yenu. Sasa yupo busy kutafuta kazi ili alee mtoto mwenyewe,anajifanya amejutia sana maamuzi yake ya kupata mtoto na mwanaume wa mtu.

So mabinti huwa wanafanya kusudi wengi wao. Hizi mbaga za ilikuwa bahati mbaya sijui sikujua sijui nini na nini ni sound tu za kuficha uozo.
 
Umeeleweka mkuu, lakini sio sngle mther wte wanauhusiano na wazaz wa bba zao, wengne waliachana kwa karaha sana so hata comm hamna, wengne walishakabdh mtt upande wa baba so comm hamna, kwahyo sio single mother wote wanauhusiano na baba zao na pia sio wte walipata mimba kwa makusud,


Kuna wengine walianza relation pasipo hata kujielewa kama 15yrs au 16 yrs nalo ni tatzo ambalo linaplkea mtoto.
 
Kabisa, mke wangu alinikuta na mtoto mmoja. Sina mazoea ya kuwasiliana na mzazi mwenzangu, wakati mwingine hadi mwaka unaisha hatujawasiliana. Mtoto yupo kwangu sasa mke wangu atapata wasiwasi gani? Wanawake hawawezi tena walivyo na tamaa hawa watu.
Kama X tu akirejea na kibunda anamlainisha akili sembuse mwanaume ambaye amezaa nae mtoto. Unajua kuzaa na mwanaume sio jambo ndogo[emoji23],ndani ya nafsi yake kuna sauti inamwambia ulikabidhi uzazi wake kwa huyu mwanaume akakupa mbegu yake ukapata nae mtoto huyu ni baba mtoto wako yaani yeye anakumiliki wewe kama mama mtoto wake. So hata asipomwita kwa maswala ya uhusiano wao bado ana nguvu ya kumwita kwa nguvu ya jina la baba mtoto, atakataa?
 
Tena mojawapo ya hao wadada alimfuata kwa busara kabisa kama mdogo wake akamwambia mdogo wangu mimi ni mkubwa sana kwako nakushauri kama dada yako nisikilize, achana na huyu mwanaume
Ila unawalaumu zaidi wanawake lakini wanaowaribia future hao wanawake huwalamu 😂😂

Pamoja na hayo umesomeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…