Mdogo wako alichumbiwa na mvulana na ametoswa kisa kazaa.
Mwambie tu mdogo wako aache kufukuzia wavulana maana hawana moyo wa kuishi na mwanamke aliyezaa.
Mwambie afukuzie wanaume watu wazima wenye akili hao huwa hawamkatai mwanamke eti kisa ana mtoto.
Mwanaume anaposimamia maslahi yake anaitwa mvulana, sijui utoto hajakua, mara hajitambui, au hawezi majukumu yaani maneno kadha wa kadha ili mradi tu kuprove nadharia kuwa mwanaume anatakiwa kubeba mizigo ya mwanamke hata kama haimhusu, huu ni upuuzi wa kihistoria ambao vijana wa sasa wanaukataa sababu wameshaona madhara yake.
Wanawake jamii imewafichia makucha sana especially maeneo ambayo wanakosea kwa makusudi na kujivika sura ya uhanga wa kusababishiwa kwamba haikuwa dhamira yao kukosea jambo ambalo si kweli.
Ukitaka uone makusudi ya watoto wa kike tazama hawa mabinti wa sasa age kuanzia 16 hadi 25 watazame matendo yao halafu jaribu kukaa nao chini uongee nao kuwapa nasaa na kukemea tabia zao. Kama sio kukuona una akili za kizee na kukijibu kwa kejeli na dharau basi watakaa kimya na kujifanya wamekuelewa kumbe moyoni na akilini ameshakupuuza.
Kuna binti alikuwa na miaka 21 anatoka na jamaa ana miaka 38 amejikoleza mbaya. Jamaa ameshazaa na wanawake watatu na kawatelekeza na watoto wao. Binti akaenda kuishi kabisa kwa jamaa eti anashindana na kuwakomesha wanawake waliokuwapo kimahusiano na mwanaume previously, kisa jamaa alikuwa kampangishia chumba akimlipia kodi na akamuweka katika duka lake auzee.
Tena mojawapo ya hao wadada alimfuata kwa busara kabisa kama mdogo wake akamwambia mdogo wangu mimi ni mkubwa sana kwako nakushauri kama dada yako nisikilize, achana na huyu mwanaume atakuharibia future yako wewe ni binti mdogo, tafuta mwenzako ambaye mtaweza jenga malengo pamoja na mtalewana huyu hakufai anakutumia tu sababu ya uzuri wako. Binti alimpuuza. Akaona wanamuonea gere, akaamua kujibebesha ujauzito wa jamaa as if mwenzake anashida na watoto zaidi.
Fast Forward leo hii, binti ana hali ngumu hawana maelewano na jamaa ananipigia simu na kunielezea tamthiria ya vituko anavyofanyiwa na jamaa na namna anajipanga sasa kutafuta mtu serious ili waanze mahusiano serious [emoji23][emoji23].
Mwingine nilikaa nae chini akiwa na miaka 21,ni mdogo wangu ambaye nasali nae jumuiya. Nilimsihi asije kuingia mahusiano na mume wa mtu au mtu mzima mwenye familia maana ndizo story alikuwa analeta sana. Aiseeee karudia huko huko tena. Nakuja mkuta ana mtoto amepata na kijana ambaye anafamilia yake ya watoto wawili na mke wa ndoa kabisa.
Sasa namtazama nasema huwa ni hamsikii au huwa mnataka kuona ladha ya ujinga kwenye matendo yenu. Sasa yupo busy kutafuta kazi ili alee mtoto mwenyewe,anajifanya amejutia sana maamuzi yake ya kupata mtoto na mwanaume wa mtu.
So mabinti huwa wanafanya kusudi wengi wao. Hizi mbaga za ilikuwa bahati mbaya sijui sikujua sijui nini na nini ni sound tu za kuficha uozo.