Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Nyuzi za masela hizi 😅😅
Ni kweli. Na zinaanzishwa nyingi kweli kweli siku hizi. Anyways, ndoa ni makubaliano na kila mmoja ana vigezo vyake anavyoweka. Kigezo kimoja kinaweza kuwa ni kipengele cha kutokuwa na mtoto. Hiki anaweza kuweka mume au mke mtarajiwa. Haijalishi upande na kwa sababu ndoa ni kitendo cha makubaliano ya hiari, ni lazima tuheshimu pande zote. BTW mtu anapoficha status yake ya uzao mara mnapoonza relationship ana lengo gani? Kuwa na mtoto ni jambo kubwa sana na ndilo linatakiwa litajwe kabla hamjaji-commit kwenye uhusiano!
 
Upo sahihi kabisa. Hili tatizo si la upnde mmoja tu. Hivi vijogoo vinavyozalisha ovyo ovyo hivi tabu sana. Unamkuta binti ana 20 yrs ila tayari ni single mother. Aisee inaumiza sana.

Na wanawake anzeni kukataa kuolewa na single fathers.

Mm ni Me
Kweli kabisa 😂😂mpira uanze moja mojaa au bila bila
 
Yote kwa yote hoja za jamaa ni za kweli kabisa kwa wanawake, swala la kuamua kubeba hivyo hivyo msimuamulie, anachoogopa hua kinawafuata watu wengi sana, mwanamke hukutana na mzazi mwenzie na kuzini huko mitaani kwa kigezo Cha mtoto, mi mwenyewe ni mwanaume najua wazi na nimejionea kwa macho haya haya na ufahamu huu huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ostaadhat wewe ujanani hukuwahi kuzini?
AlhamduliLlah Allah kaniepushia dhambi hiyo. Sijawahi kuzini na awaepushie wale wote wanaofikiria kuzini na wanaozini.


Kwanza nnajiuliza na nnakuuliza, hivi una zini ili iweje? Wakati muumba wako kakuonya usiisogelee zinaa. Siyo kuzini tu, hata kuisogelea zinaa hakutufai kabisa wanaadam.

Uzuri wa Uislaam umetupa na nini cha kufanya kuzuia machafu, tusiache salat, salat zinatuepusha na uchafu wote .
 
AlhamduliLlah Allah kaniepushia dhambi hiyo.


Kwanza najiuliuliza na nnakuuliza, hivi una zini ili iweje? Wakati muumba wako kakuonya usisogelee zinaa. Siyo kuzini tu, hata kuisogelea zinaa hakutufai kabisa wanaadam.
Kwa hiyo hukuwahi kuwekwa kabla ya ndoa Faiza? Na baada ya ndoa hukuwahi kuwekwa nje? Mmmmh nina mashaka.
 
Katika mahusiano mapya usitoe historia yako ya mahusiano ya nyuma kwa bwana mpya, au sema kwa ufupi sio unamwambia kuwa mpaka hapo yeye ni mwanaume wa 7 kwako ndani ya mwaka mmoja!
Sasa kuficha mahusiano ya nyuma, angali unamtoto tayari ??
Huyo mtoto si inaonyesha kuwa ulikuwa kwenye mahusiano
 
Aaaa
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…