Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Ili kuoa single mother lazima kuzingatia yafuatayo;

1. Lazima ushuhudie kaburi la baba wa mtoto.
2. Cheti cha kifo ( majina ya cheti yafanane na ya kaburi pamoja na kufuatilia uhalali wake ofisi za RITA)
3. Upate video ya mazishi kujiridhisha

NB:
Hakuna kitu kinaitwa mimba ya bahati mbaya.
SASA WEWE JICHANGANYE, HAKUNA RANGI UTAACHA IONA.
Inna
 
inasikitisha lakini kuna fundisho hapa.. kiumbe wa watu hana hatia. lakini uliposema 'mwanaume mzuri ana maisha yake' nadhani jibu lako liko hapo..jamaa amefanya kila kitu kwa steji yake, anatafuta wa kufanana naye hivyo hivyo,pengine wakati anajitengenezea hayo maisha mdogo wako alikuwa ana'tafuta' mtoto+ plus drama za wazazi wenza hakuna mtu anayezipenda kiukweli... siku mdogo wako atakuja kumkabidhi mtoto ili jamaa ampeleke kwa baba yake and that is emasculating
 
Haina madhara hio 😀!!!
Mimi kuwa na mtoto ni alama kuwa rijali. Wewe kuwa na mtoto bila ndoa ni alama kuwa huna akili. Boyaaa
Ha ha haaa...hawatambui nafasi yao katika jamii hao, wanajikuta kutaka kutambulika kama tunavyotambulika sisi.
Matukio yanatutambulisha tofauti, halafu wanakuja kutulilia sisi eti kuwa na mtoto siyo shida, kasema nani?
La kuoa mwanamke asiye bikira waliokubali wamelivumilia, sasa wanataka waoe wenye watoto, what next? Watataka hata wakiwaoa wakubali ku share na wanaume waliozaa nao sababu wamewakuta na ni wazazi wenzao.
Jamii inapaswa kumheshimu mwanamke katika nafasi yake, lakini jamii inayowaendekeza wanawake na kuwasikiliza kwa kila kitu kamwe haijawahi kuwa salama.
 
Siyo wote, kwa wenzetu waislamu hawana shida kwenye kuoa mwanamke mwenye mtoto, Kimbembe kwa wasiyo waislamu, kwasababu wao waislamu kuoa na kuachana ni jambo la kawaida utakuta mwanamke kaolewa na kuachika zaidi ya mara tatu na kazaa watoto kwa wanaume tofauti, Sasa kwa sisi Vijana wa kikristo au kwa wapagani hatuja zoea na siyo tamaduni zetu kuona Mama zetu wame zaa watoto kabla ya kuolewa, Tamaduni za mama wakiafrika ni kuzaa na mume mmoja tu, kama kazaa watoto kumi basi baba yao ni mmoja tu.
Correct [emoji3514]
 
Sijui nipo off topic , hivi kwanini watoto tuseme wanne waliozaliwa na baba tofauti ila mama ni mmoja ,Huwa hakuna ile family bond , yaani ule upendo baina ya ndugu na ndugu?[emoji848]
Ni kweli 100%
 
Samahani unaweza kuweka namba ya huyo jamaa hapa nimpigie nimpongeze?

Unasema huwaelewi wanaume kuhusu kukataa watoto wa single moms yaani umeshindwa hata kujiuliza hapo alipoangalia mpaka future za watoto atakaowazaa kwamba vipi wataambiwa na mama yao wasizini wakati yeye alizini kabla hajaolewa,jiulize hata wewe mama yako angezaa nje then leo akwambie usizini ungemuelewa?
 
Wewe unataka mechi ianze na aggregate kama ya yanga?.
Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka Sasa nimejifunza haya kuhusu singomothers,
° wanawake huwazalia watu waliowapenda sana, hivyo Hadi anazaa Maana yake amempenda sana, hakuna bahati mbaya.
° Singo mothers Wengi Huwa na mawasiliano na waliowazalisha, na hivyo hufanya ngono several times .
° Ukiwa singo mother ni vigumu sana kuolewa, unless singo mother uwe na hela.
 
Back
Top Bottom