…pia no one is forcing the guy to love/get married to the girl it’s his choice. In fact hata Mimi namlaumu huyo binti kwa kutomjulisha kijana mapema, she has no one to blame but herself!
Yuko hapa tunajadili not only in their context but kuna ka stigma against single moms vijana wanajazana ujinga, so lazima tu reason kwa upana sio tu kwa a single case!
Na mimi nakwambia hivi, stigma katika mapenzi ni haki ya mtu. Ndiyo maana ya mapenzi, kuamua nachagua kupenda hiki, sitaki kupenda kile. Bila stigma kungekuwa hakuna choice, na bila choice hakuna mapenzi.
Mapenzi yangekuwa siasa za "haki sawa kwa wote". Kila mtu anajichovyea, hakuna selectivity wala exclusivity. Hakuna mapenzi hapo.
Kuna watu wana stigma dhidi ya Wanigeria, huwaambii kitu.
Kuna watu wana stigma dhidi ya watu weusi.
Mimi kama mtu mweusi sitaki kuwalazimisha wanipende, nitaenda ninapopendwa. Sitawanyanyapaa kwa kutumia haki yao hiyo.
Kuna watu wana stigma dhidi ya wazungu, huwaambii kitu.
Kuna watu wana stigma dhidi ya wanawake wanene. Ni haki yao.
Ni haki yao through and through. Mapenzi ni kitu very personal and private.
Utafanya nini sasa? Utalazimisha mtu ambaye hapendi Wa Nigeria awapende?
Hiyo stigma ni haki yao, ukiwaingilia kwenye haki ya kuwa na stigma hiyo, umewanyanyapaa, wewe ndiye unakuwa na makosa. Unawalazimisha wapende kitu wasichopenda.
Hatupangiani nani wa kumpenda.
Hata wewe ukilazimishwa upende mtu usiyempenda hutafurahi.
Unajua mkiinyanyapaa stigma kitakachotokea ni nini?
Watu watajifanya wanawapenda hao single mothers ili wawe "political correct" tu, watawaoa, halafu ndoa zitajaa migogoro kila siku kutokana na stress za "nimeoa single mother kwa pressure za kijamii nisionekane nina stigma".
Hapo ndipo unakuta ndoa zisizo na amani, wanawake wanapigwa, mwanamme anaona kawa trapped kwenye ndoa.
Bora mtu aseme mimi sitaki kuoa single mother, siwapendi, na wala msimnyanyapae, aepuke kuingia kwenye ndoa isiyo na mapenzi ya kweli.
Ndiyo maana ku normalize stigma katika mapenzi ni kitu kizuri sana.