Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Wengi huwa wanalazimisha kubakia na mtoto lakini bado atahangaika gharama za malezi kwa kusumbua watu baki au huyo mwanaume.Jamaa kaoa mke mwingine na hata mtoto hajamchukua ili aishi nae?
Ushauri kwa single mothers - mlio na mipango ya kuolewa, msipende kukaa na hao watoto, wapeni baba zao, mtoto akishaacha kunyonya, mtu yeyote anaweza kumtunza, ili mradinawe na upendo kwa mtoto, baba hawezi mchukia mwanawe.
Sasa tatizo nyie mnapenda kukaa na watoto ili muwatumie kama chambo cha kupata hela ya matumizi, mkija pata watu wa kutaka kuwaoa ndio mnawakimbiza wenyewe wakijua mna watoto na watoto wapo kwenu bado.
Mnang'ang'ania watoto na ilhali malezi yenyewe mnawapa mabaya, ya kumjaza mtoto chuki dhidi ya baba yake. Pole sana mdogo mtu kwa ndege kupeperuka.
Mwisho wa siku mtoto akikua na kuwa mtu mzima lazima atamtafuta baba yake. Hapo baba mtu ndipo anaanza kuchukua points. Unakuta mwanamke ahangaika na mtoto hadi kafika chuoni huko. Mtoto akibanwa na shida anamcheki mama ampatie mahitaji mama anakuwa mkali anamwambia mtoto kuwa zingatia masomo, achana na maswala ya mavazi sijui smartphone, sijui laptop tumia na wenzako.
Mtoto anapata wazo kuwa mimi si nina baba lakini? Anafanya mchakato wa kumtafuta anampata. Anakuta mwamba ana pesa ya kubadili mboga. Baba anamwambia mwanangu mimi nakupenda sana, ila mama yako hakuwa anataka mimi niwe karibu yako.
Chukua hii pesa kanunue Smartphone, mwezi ujao unikumbushe nikufanyie shopping ya mavazi na hiyo laptop unambie unayotaka kuna baba yako mdogo yupo Dubai nimuagize akuletee na hii laki mbili chukua kwaajiri ya chakula ikusindikize huu mwezi hadi mwezi ujao. Ukiwa na shida usisite kuniambia mwanangu nakupenda sana.
Kwann Single mother usionekane ni Mchawi miaka yote hii umelea mtoto mwenyewe kwa shida ila mtoto anakuja kuona kumbe baba yake ni msaada mkubwa ila kwa roho mbaya yako hukutaka amlee. Mtoto anaanza kukuchukia. Ukiongea baya juu ya baba yake anakuona una chuki dhidi ya baba yake kipenzi.
Mtoto akisikia baba yake anaumwa anapata wasi wasi balaaa anakwenda kukesha nae hospital na kumpikia chakula. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Single mother wa kizazi hiki mtajua hamjui maana ni mwendo wa kufungwa mabao home and away. Mtaelewa vizuri ile amri ya 6. USIZINI. Na mtaelewa vizuri kwann watu huwa wanaolewa halafu ndio wanapata watoto na sio kinyume chake.