PreGE2025 Kala Jeremiah: Kelele zinazoendelea zimepata mwanya wa kumuonea Rais huyu kwa kuwa ni mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu

Kwa hiyo huyu Kala Jeremiah anaamini kuwa hizi No Reforms No Election zimekuwa nyingi kwa sababu Rais Samia ni mwanamke na ni mama?

Angalieni jinsi ya kumtetea Rais. Kauli kama hizi sio za kumsaidia Rais bali zinamuharibia yeye na taasisi yake

=============

Anaandika Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"Maoni yangu kuhusu kelele zinazoendelea ni kelele zilizopata mwanya wa kumuonea rais huyu kwa kuwa ni mama, ni kelele zilizotengenezwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa.

Wananchi fungueni macho na masikio mtasikia zitokako kelele hizi. Mama huyu kafanya kazi kweli kweli, ni rais kwelikweli lakini kwa maslahi ya kisiasa tumeamua kubeza kazi njema alizofanya rais wetu. Swali langu je ni nani miongoni mwa hao anayeweza kuwa rais bora kama Samia Suluhu Hassan ??? Au tunaliamsha tu hatujui sababu na matokeo."

Screenshot_20250609-133846_Instagram.jpg
 
Bora yupi!? ambae amzidi mama kwenye kuuza bandari,misitu etc..
Huyo bora aje auze ikulu, auze mlima kilimanjaro, tukiamka asubuhi tukute mabango taifa limeuzwa kila mtu ahame kwa amri ya mahakama ya kimataifa !??
 
Chawa wameishiwa sera kabisa. Sasa ndo nini hii?

Naungana na mtoa mada. Hapa mnamuharibia Rais

Lucas Mwashambwa fundisha wenzako namna ya kumsifia Rais. Hapa wanaharibu
 
ndugu zangu wa no reform no election kwaiyo hoja zetu zimekuwa kelele
 
Wakuu

Kwa hiyo huyu Kala Jeremiah anaamini kuwa hizi No Reforms No Election zimekuwa nyingi kwa sababu Rais Samia ni mwanamke na ni mama?

Angalieni jinsi ya kumtetea Rais. Kauli kama hizi sio za kumsaidia Rais bali zinamuharibia yeye na taasisi yake

=============

Anaandika Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"Maoni yangu kuhusu kelele zinazoendelea ni kelele zilizopata mwanya wa kumuonea rais huyu kwa kuwa ni mama, ni kelele zilizotengenezwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa.

Wananchi fungueni macho na masikio mtasikia zitokako kelele hizi. Mama huyu kafanya kazi kweli kweli, ni rais kwelikweli lakini kwa maslahi ya kisiasa tumeamua kubeza kazi njema alizofanya rais wetu. Swali langu je ni nani miongoni mwa hao anayeweza kuwa rais bora kama Samia Suluhu Hassan ??? Au tunaliamsha tu hatujui sababu na matokeo."

View attachment 3361965
Kashafulia huyu
 
Back
Top Bottom