Wakuu
Kwa hiyo huyu Kala Jeremiah anaamini kuwa hizi No Reforms No Election zimekuwa nyingi kwa sababu Rais Samia ni mwanamke na ni mama?
Angalieni jinsi ya kumtetea Rais. Kauli kama hizi sio za kumsaidia Rais bali zinamuharibia yeye na taasisi yake
=============
Anaandika Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram:
"Maoni yangu kuhusu kelele zinazoendelea ni kelele zilizopata mwanya wa kumuonea rais huyu kwa kuwa ni mama, ni kelele zilizotengenezwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa.
Wananchi fungueni macho na masikio mtasikia zitokako kelele hizi. Mama huyu kafanya kazi kweli kweli, ni rais kwelikweli lakini kwa maslahi ya kisiasa tumeamua kubeza kazi njema alizofanya rais wetu. Swali langu je ni nani miongoni mwa hao anayeweza kuwa rais bora kama Samia Suluhu Hassan ??? Au tunaliamsha tu hatujui sababu na matokeo."
View attachment 3361965