Kalapina awataka wale waliomteka Roma Mkatoliki wakamteke na Yeye ili awaonyeshe Kazi

Kalapina awataka wale waliomteka Roma Mkatoliki wakamteke na Yeye ili awaonyeshe Kazi

Kuna kipindi nilisomaga kitabu cha willy gamba,

Basi nikatoka hom ili nipambane na migambo waliokua wanatoza kodi mtaani maana walikua wanaboa kinyama

Namshukuru Mungu walinivunja meno mawili tu

Mkuu umenichekesha sana duh!!!
 
Kwanza ANGEROPOKA kumsema BWANA YULE..halafu ndy ATAMBE MAJUKWAANI
 
Kinachomsaidiaga uyu akianzisha fujo anapata back up kwa jamaa zake Wa kikosi.kama alivyopigana na bou nako.wanapigana wawili Mara kikosi kizima kinavamia wakiona mwenzao maji ya shingo.inatakiwa mmoko kwa mmoko. Mimi mwenyewe namfua tu ata kama ana kifua
BOU NAKO alimuita wazichape tena mpaka kesho ajamfuata na bou nako anaingia bongo kama kawa na alitunga wimbo akamuambia kalapina wew ni shoga njoo tuzichape uone
 
Kalapina kamchenjia aliyesambaza habari hii ...anasema kanukuu anavyotaka kinyume na alichosema ....kamwambia lazima alipe kwa uongo huu ....
 
Kalapina ana hamu tu, kasikia habari mwenzie katatuliwa malinda na yeye anataka.
 
au kama vipi aende kibiti akatangaze kua wale wanaoua watu waende wakamuue yeye, awaoneshe kazi.
 
Anaonekana hajui maana ya kutekwa.
Kama watu wanauwezo wa kumbeba mnyama kifaru na ubabe wake,anapelekwa kuwekwa rebo wakimaliza wanamludisha polini.

Kuliko mtu.siku yakimkuta hatasema itabakia kua siri yake.
 
Kinachomsaidiaga uyu akianzisha fujo anapata back up kwa jamaa zake Wa kikosi.kama alivyopigana na bou nako.wanapigana wawili Mara kikosi kizima kinavamia wakiona mwenzao maji ya shingo.inatakiwa mmoko kwa mmoko. Mimi mwenyewe namfua tu ata kama ana kifua
[emoji3] [emoji3] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.

Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji ) “ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.

Haya Watekaji ( Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba beach ) Kalapina huyo anawakaribisheni mkamteke na Yeye ili mkapate Kipondo / Kipigo ambacho inawezekana hata huko Chuoni Kwenu Wakufunzi wenu ama hawakuwafundisha au walisahau kuwafundisha.

Shikamoo Kalapina

Nawasilisha
Kuna ukweli ndani, hutakiwi kujilegeza kabisa...nakubaliana naye. Mwaka 2007 niliwekwa kati na wazee [jambazi],ila sikulegea japo nilijeruhiwa ila na mimi nilimpa kubwa mmoja...nikawatoroka. Safi sana K.Pina
 
Hivi anayaonaga kweli Yale ma vipisi yanayo mlinda mkemia,yaje matatu hata bila chuma mbona lazima uongee sauti ya chumbani
Tuacheni masihara lakini watekaji wakiwa kama wale wababe wa nape so kalapina atajipatia bastola kirahisi tu!
 
Back
Top Bottom