Kale ka nchi kanaweza kuvamiwa na kushambuliwa, lakini mwisho wa siku, mvamizi ataambulia kujuta na kusaga meno

Kale ka nchi kanaweza kuvamiwa na kushambuliwa, lakini mwisho wa siku, mvamizi ataambulia kujuta na kusaga meno

Sjawahi kujua ni kivipi Israel huwa ni vigumu kupigika!
Ukiondoa hiyo Imani ya kusema ni taifa la Mungu, lakini Je, Mungu hachukii kisirani?

Mbona hicho kitaifa kina watu na viongozi wenye kisrani sana

Ni kagomvi mpaka nachukia, hakaogopi nchi kubwa wala mhuni kama Irani

Naomba kujua, mafunzo ya kijeshi jeshi la Israel hupata kutoka jeshi la nchi gani?

Je, tuna nchi ambayo hupewa mafunzo na jeshi la Israel kwa sasa? Jeshi hilo ni mahiri kiasi gani katika medeni za kivita?

Ni taifa dogo na lenye watu wachache, cha ajabu ndio taifa linaloogopeka zaidi Duniani

Ni taifa lenye jeshi imara zaidi ya nchi kama Iran, Saudi Arabia, brazil, na hata North Korea n.k

Africa tuna kwama wapi?

Mfano kama Nchi yangu Tanzania!

Hatujisikii aibu kuwa na nchi kuuubwa, lakini hatuwezi kabisa kuwa kwenye position kama hizo?

Mimi napenda mashindano siku zote, huwa sipendi kuachwa nyuma, ndivyo ninavyojisikia wivu nchi yangu kuwa nyuma kiasi vile

Tutafikia lini hapo? Kiasi cha kumkoromea hata Marekani, china, urusi na hata nchi yoyote?
Unazungumzia kupigika kwa aina gani wakati waislael zaidi ya 800 wameuwa.

Hili ni pigo kubwa sana kwenye Historia ya taifa la Israel.

Kwa shambulio la Jumamosi hii, Hamas wamefanikiwa kwa zaidi 100% kwa sababu lengo la Hamas lilikuwa kulipiza kisasi na kuonya walowezi wa Kiyahudi wanaoishi katika maeneo ya Palestina.
 
Unazungumzia kupigika kwa aina gani wakati waislael zaidi ya 800 wameuwa.

Hili ni pigo kubwa sana kwenye Historia ya taifa la Israel.

Kwa shambulio la Jumamosi hii, Hamas wamefanikiwa kwa zaidi 100% kwa sababu lengo la Hamas lilikuwa kulipiza kisasi na kuonya walowezi wa Kiyahudi wanaoishi katika maeneo ya Palestina.
Zingatia mantiki ya kile kimeandikwa hapo mkuu
 
naona misri nao kuna askari polisi ameua watalii wa wili wa kiyahudi. hao watalii nao walitakiwa wajifanye ni wamarekani, kujitambulisha kama wayahudi kwenye ardhi ya mwarabu ilikuwa very risky. hata hivyo, hiyo ni dosari kwenye utalii wa misri sasa.
Ardhi ipi ya waarabu? Hao waarabu waliokuja 1500's. Sema ardhi ya Waafrika.
 
Israeli anapigikia vizuri sema Huwa anakingiwa kifua na kaka mkubwa Marekani.Hii ni Aibu kwa Mossad kujifanya wanaongoza Kwa Intelligence duniani.
Israel no propaganda tu,hana lolote.hakuna vita yoyete amewahi kupigana na akashinda,anapigana na wala tende na harua tu.
 
Wao hawajui si wanaua kwa mafungu hawawezi kuchagua huyu ni Nani na huyu Ni yupi???
Mataifa kadhaa yameanza kutangaza kwamba watu wao pia wameuawa. kuna raia wa ufaransa, nepal, marekani na nchi kadhaa wameuawa. wengine walikuwa wanafunzi.
 
Wao hawajui si wanaua kwa mafungu hawawezi kuchagua huyu ni Nani na huyu Ni yupi???
ila huu ndio ugaidi halisi, imagine badala ya kupigana na wanajeshi trained kama wewe, unaenda kupiga raia ambao hata hawako trained, wengine wanafunzi. kuna mama mmoja analia mtoto wake aliondoka mexico kuja shule, amechukuliwa mateka na wamempeleka gaza. kama wao ni wanaume, si wapigane na wanajeshi wa israel? unashambuliaje raia wasio wanajeshi? ndio ugaidi huo.
 
Lakini mwisho wa siku watabaki kama moja ya mataifa walioivamia Israel na kumteka jenerali wa Israel! Wape credit..
Haisaidii maana mwisho wa siku ushinde. Sasa kwa mfano Israel akivamia Gaza akaichukua yote utakuwa umepoteza au umewin.
 
mapigo mengi huwa ni usiku. kwahiyo hadi kesho asubuhi, kuna mengi tutasikia. israel wanasubiri giza liingie kusiwe na makamera, hapo ndipo wanachapa. hamas wamefanya jambo baya sana.
Makamera wakati kila siku wanaua waandishi wa habar
 
Back
Top Bottom