- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Inadaiwa kuwa Kalonzo Musyoka amefanya kikao cha siri leo na Rais William Ruto mjini Narok, ambapo walifikia makubaliano ya kushirikiana kabla ya uchaguzi. Haya yanajiri huku kukiwa na uvumi kwamba upinzani unampendelea Edwin Sifuna kuwa mgombea wao wa urais, akisaidiwa na mgombea mwenza kutoka Mlima Kenya, ambaye inadaiwa ni Kiharu MP Ndindi Nyoro.
Kwa mujibu wa madai hayo, Kalonzo hayuko tayari kuwa mgombea mwenza na badala yake anapendelea kumuunga mkono Ruto, ambaye inadaiwa tayari alimuahidi kumuunga mkono mwaka 2032. Kabla ya hapo, baada ya uchaguzi wa 2027, Kalonzo anadaiwa kuahidiwa nafasi ya kupendekeza Mawaziri (CSs) watano na Makatibu Wakuu (PSs) 13.
Madai hayo pia yanasema kuwa Kalonzo ameagizwa kuendelea kujionyesha kama kiongozi wa upinzani hadi pale upinzani utakapomtangaza mgombea wake rasmi, ndipo atakapohama rasmi na kujiunga na upande wa Rais Ruto.
Inadaiwa kuwa waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na JB Muturi, Mutuse, na Seneta Enock Wambua.

- Tunachokijua
- Wiper Yakanusha Vikali Madai ya Kalonzo Kujiunga na Ruto
Chama cha Wiper Patriotic Front kimekanusha vikali taarifa zilizosambaa mtandaoni zikidai kuwa kiongozi wake, Kalonzo Musyoka, amefikia makubaliano ya kisiasa na Rais William Ruto au yuko mbioni kujiunga na serikali.
Katika taarifa iliyochapishwa kupitia kurasa rasmi za chama, Wiper ilieleza kuwa chapisho linalodai Kalonzo amejiunga na Ruto ni la uongo na kuwataka Wakenya kutopotoshwa na propaganda hizo. Chama kimesisitiza kuwa Kalonzo anaendelea kuwa sehemu ya WANTAM Movement na United Alternative Government, akisisitiza kuwa dhamira yao ya kuiongoza Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027 haijabadilika.
Taarifa hiyo inajiri baada ya ujumbe wa mtandaoni kudai kuwa Kalonzo alifanya kikao cha siri na Rais Ruto mjini Narok na kufikia makubaliano ya kushirikiana kabla ya uchaguzi wa 2027. Hata hivyo, Wiper imesisitiza kuwa madai hayo hayana msingi na imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo hazijatolewa kupitia njia rasmi za chama.
Chama hicho kimewahimiza Wakenya kutoshiriki kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa, kikisisitiza kuwa msimamo wa Kalonzo na Wiper kuhusu muungano wa upinzani unasalia ule ule.