"Walisema Jumatatu tar 10 saa mbili watakuwa ofisini lakini mpaka sasa hivi saa nne hamna mtu, tumeliwa! Vibali vyao vipo lakini kuna fenicha tu ambazo si za kwao, mpangishaji aliwapangisha jengo likiwa na kila kitu ikiwemo laptops, na mpangishaji anawadai pia kodi ya miezi miwili hawajalipa!"
Niko kwenye Kimbinyiko naelekea Dodoma nimekaa na wamama wawili wa makamo, naona wanalalamika Kalyinda haifunguki na wanashindwa kuingia tangu jana (naona mambo karibia yanawafika mdogo mdogo). Nikabaki nacheka moyoni, maana kuna mtu alikuwa ananishawishi kujiunga mpaka tumegombana, hatuongei...
Yeah, kuna group nshawahi kuunganishwa la jamaa wa kushtuana michongo ya hivi.
Yani wao wanaweka hela kitu ikiwa mpya mpya...ikifika mwezi wanatoa faida wanasepa kutafuta mpya nyingine.
Bora hata ya JATU inawezekana kuna staff hawakutimiza wajibu wao, lakini JATU niliwafuatilia ni really kabisa, tatizo wabongo huwa tunafeli kwenye mwendelezo wa jambo jema.