Ni kweli inasikitisha sana. Kuna kijana mmoja nilimpambania akapata nafasi ya kwenda JKT. Dogo kapigika kule Cheetah kwa miaka 2. Juzi nakutana naye amepakizwa kwenye guta na mwenzie.
Kwa furaha namuuliza za siku afande, nikijua amerudi likizo ya mwisho wa mwaka. Naona respond ya dogo haipo kama nilivyomchangamkia na nimjuavyo.
Akaniambia mkataba umeisha na wamenirudisha nyumbani. Dogo nilimtoa kwenye bodaboda aende huko sasa amerudi na kuwa msaidizi wa rafiki yake muendesha guta aliyekuwa anapiga naye bodaboda kabla ya kwenda JKT.
Dah, iliniuma sana na nilitaka nilete uzi hapa kulalamika hilo. Wanamapotezea muda watoto wa watu. Waache huu ukuda.