Kama ajira hazipo Kuna umuhimu wa vijana kwenda kwenye mafunzo JKT?

Kama ajira hazipo Kuna umuhimu wa vijana kwenda kwenye mafunzo JKT?

Vijana wengi siku za hivi karibuni wameonesha uzalendo wao kwa kujiunga na Jeshi La kujenga taifa (JKT) kwa kujitolea na kwa mujibu wa sheria pia. Lakini idadi kubwa ya vijana Hao wanakosa ajira baada ya kuhitimu mafunzo yao na kumaliza mkataba wao jeshini, hivyo wanaishia kurudi mtaani na kuanza kujihusisha na shughuli zilizokinyume na sheria kama WIZI, ukabaja n. K. Hii imekaaje kama ajira hazipo Kuna umuhimu wa vijana kwenda kwenye mafunzo?
Wanajitolea, kwenda jkt si ticket ya kupata ajira
 
Mimi nimelinda Gard world - diplomatic areas nilikuwa nakamata karibia 1M kasoro na sijapita JKT wala mgambo

Vijana watz wanakariri maisha Sana na kupoteza muda .

Hivi unafikiri hata ukipita JWTZ jambazi akiseti mipango yako hakupati?

MTU Kama upo na interest ya kulinda ajifunze kiingereza na CCTV camera akimaliza aende G4S , SGA n.k

Leo MTU anakimbilia Suma Jkt anaenda kulipwa 200K
 
Kwahiyo unaunga mkono JKT inazalisha ajira ya vibaka? Ndio national service act no 16-17 inavyosema kuwa vibaka wanazalishwa huko?

Vijana wakiingia JKT ndio ajira moja kwa moja?
Nini wanatoa huko?(lengo ni nini)
Hawazalishi ilo nakataa ila impact inayotokea moja wapo ni iyo baada ya vijana kumaliza muda wao na kukosa lile walilokuwa wanatamani kupata ndio inatokea ivyo
 
🪖🪖Nalilia nini......? 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️nalilia bakabakaaa ee unalilia nini wewe
 
Sijui mtajiajiri vipi maana ni juu yenu, lakini kipindi mnajiunga mliambiwa mkimaliza mafunzo mtapewa ajira?, kama ndio basi wamepokonya haki yenu na kama ni hapana basi tafuteni shughuli za kufanya Ili basi muweze kuishi au lah ajira zozote za majeshi zikitangazwa ombeni mnaweza mkapata kazi za aina hiyo.
 
Ana stress watu hawajui tu ukienda jkt unapoteza mawasiliano kabisa connection ile inapungua so unaporudi mtaani unalazimika iutafuta upya connection na inakuwa ngumu sna
Mnakosea mnapoleta double standard kati ya watu waliokosa kazi huko jkt na graduates au vijana wasio na ajira mitaani ,tatizo liko pale pale hata mkilipaka rangi za ujkt wala nini , tatizo ni ukosefu wa ajira kwa vijana na hapo ndio mzizi wa tatizo ,hii ya kuzunguka sijui jkt ni upuuzi ,mada iwe tatizo la ajira kwa vijana ,kwani graduates wanaotoka vyuoni baada ya muda mrefu wa masomo kwani wanakuwa na network gani au mtaji gani wa kuanza harakati kitaa ? , Si ndio hawa huwa mnawananga kila siku kwamba hawana akili za kujiajiri ?
Mlivyowanafiki mnakimbiza ndugu zenu jkt kwa kuhonga na na kuendekeza undugu ili wapate mterezo wa kazi kwenye majeshi halafu kila siku mnawatukana graduates au vijana wenye elimu wasio na ajira mtaani ,mna akili ninyi ?
Wanapokosa kazi kwenye majeshi ndio mnakuja kuanzisha mada za kipuuzi humu kwamba vijana wa jkt hawaajiriwi ,so what ?
 
Nchi yenye mifumo ya dhulma kama hii ,haya maumivu yatawakuta wengi .
Unakuta watu wameajiriwa kama walinzi ila wanalipwa laki na nusu , hebu piga picha mtu anaishije kwa laki na nusu , ndio maana wengi wanaishi kwenye deals za wizi ,lazima wakuibie tu
 
Kwani kupitia jkt ndio iwe sababu ya kupata ajira?Ila ninakiri ya kuwa Kijana aliyepata Mafunzo ya ukakamavu akiamua kujiajiri kwenye eneo hilo la ukabaji anakuwa na ufanisi wa hali ya juu.
 
Dira ya JKT
Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo , undugu, ukakamavu na kupenda kazi.

Dhima ya JKT
Kuwalea vijana wa Tanzania, ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.
 
Mimi nimelinda Gard world - diplomatic areas nilikuwa nakamata karibia 1M kasoro na sijapita JKT wala mgambo

Vijana watz wanakariri maisha Sana na kupoteza muda .

Hivi unafikiri hata ukipita JWTZ jambazi akiseti mipango yako hakupati?

MTU Kama upo na interest ya kulinda ajifunze kiingereza na CCTV camera akimaliza aende G4S , SGA n.k

Leo MTU anakimbilia Suma Jkt anaenda kulipwa 200K
Suma JKT haimtoi mtu kimaisha ni utumwa tu
 
Back
Top Bottom