Kama ajira hazipo Kuna umuhimu wa vijana kwenda kwenye mafunzo JKT?

Kama ajira hazipo Kuna umuhimu wa vijana kwenda kwenye mafunzo JKT?

Ni kweli inasikitisha sana. Kuna kijana mmoja nilimpambania akapata nafasi ya kwenda JKT. Dogo kapigika kule Cheetah kwa miaka 2. Juzi nakutana naye amepakizwa kwenye guta na mwenzie.

Kwa furaha namuuliza za siku afande, nikijua amerudi likizo ya mwisho wa mwaka. Naona respond ya dogo haipo kama nilivyomchangamkia na nimjuavyo.

Akaniambia mkataba umeisha na wamenirudisha nyumbani. Dogo nilimtoa kwenye bodaboda aende huko sasa amerudi na kuwa msaidizi wa rafiki yake muendesha guta aliyekuwa anapiga naye bodaboda kabla ya kwenda JKT.

Dah, iliniuma sana na nilitaka nilete uzi hapa kulalamika hilo. Wanamapotezea muda watoto wa watu. Waache huu ukuda.
Mimi binafsi siwezi mpeleka ndugu yangu kule jkt kama sina uwezo wa kumtoa kule nitampeleka nikiwa na uwakika wakumtoa kule kwenda kwenye ajira ila siwezi ni lawama
 
Ukijitolea haimaanishi ndo utaajiriwa mbona hata wao wanasema kabsa bora wangesema wanaenda kuwaajiri ndo mngelalamika nyie ni kama tu watu waliosoma chuo wakakosa ajira tena bora wa chuo ana ujuzi
 
Ni sahihi ndio maana vipo vyombo vingine vinavyochunga na kulinda nidham za raia na kutoa hukumu za kiraia
Ambazo so far nazo zina meno ya kumwajibisha Askar wa akiba kipindi akizingua
Ila wanatakiwa wasifundishwe vitu vyote kama matumizi ya silaa watu watajifunza kwenye kozi ya ajira ambayo atakayo bahatika kwenda
 
Ukijitolea haimaanishi ndo utaajiriwa mbona hata wao wanasema kabsa bora wangesema wanaenda kuwaajiri ndo mngelalamika nyie ni kama tu watu waliosoma chuo wakakosa ajira tena bora wa chuo ana ujuzi
Ni kweli lakini hao ndio nguvu zaki kubwa kujenga miradi mfano ukuta wa meleleni wamejenga vijana af wanakuja kuajiliwa watu wa mtaani mbaya sana hii
 
Wanatofauti sana graduate mwenye akili anajipanga na anatoka na mtaji wa kuanzia maisha ila kijana wakujitolea huwezi pata mtaji kwa posho ya 45k unayo pewa kila mwisho wa mwezi tofauti na graduate anaepewa laki6 kwa awamu mkuu
Nitakupa dada🤣🤣
 
Ni kweli kwa kiasi fulani mtu anatoka akiwa kachanganyikiwa kapoteza miaka miwili hakuna alichopata anarudi mtaani ana anza upya inaumiza sana mwisho wa mwezi anapata 45 kijana baada ya makato wakati uho wenzake washampita mbali kimaisha inaumiza wanaporudishwa mtaani mtu anatakiwa kuanza upya yaani
Kwahiyo unaunga mkono JKT inazalisha ajira ya vibaka? Ndio national service act no 16-17 inavyosema kuwa vibaka wanazalishwa huko?

Vijana wakiingia JKT ndio ajira moja kwa moja?
Nini wanatoa huko?(lengo ni nini)
 
Hizo Ajira uchwara hata MTU asipozipata

Ni ujinga mkubwa Kijana smart kwenda
Jkt kulima mboga
 
Hakuna jkt mwizi wewe. Hao vijana wanajiheshimu sana waliotoka jkt
Hivi kwanini Jeshi lisiwachukue hao vijana wa Jkt?, wengine wanatabika tu mitaani kwa kulinda malindo yenye njaa kila leo kupoga vizinga, huku wakubwa wao wanoingia mikataba wakineemeka.
 
Back
Top Bottom