Kama Bandari ya Bagamoyo lazima ijengwe, basi sio kwa masharti ya kuweka nchi rehani

Kama Bandari ya Bagamoyo lazima ijengwe, basi sio kwa masharti ya kuweka nchi rehani

Tukubaliane tusikubaliane Rais Samia kashakubali mradi wa Bagamoyo kwa masharti aliyoyakataa Magufuli na ambayo Kikwete aliyakubali. Kwa hivi sasa ni kiini macho kinafanyika. Watatumwa watu kimbelembele kuendesha mazungumzo.

Nionavyo mimi viongozi wabinafsi wamejaa kwenye ranks za CCM na bungeni kuliko wananchi wanavyofikiri. Kuna wanafikiri Magufuli kuhamishia makao makuu Dodoma na kufuta mpango wa Bandari Bagamoyo na huku kuwekeza maeneo ya ziwa aliafanya upendeleo. Kila mwananchi amejua masharti ya kuwekeza bandari ya Bagamoyo baada ya Magufuli kuyataja. Vinginevyo yalifanywa siri. Kwanini viongozi wetu wakubali mashari ya kidhalimu namna hiyo kama sio kwa sababu za maslahi binafsi?

Licha ya Rais Samia kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja itakua ulaghai kwa kua anayofanya ni tofauti. Mradi wa bagamoyo wananchi watataka kuona mashari yake sio yale ya kikoloni aliyowaambia Magufuli. Kama bandari lazima ijengwe sio kwa masharti ya kuweka nchi rahani. Ni bora mradi ufe au tuje tujenge wenyewe kwa fedha yetu.

Tulimsikia kikwete akisema wapwani hawangependa mji mkuu uhamie dodoma. Tumeona samia akirejesha shughuli za rais kila wakati Dar na sasa anataka bandari ya bagamoyo kujengwa kwa vyovyote.

Tatizo la huu mradi ni kwamba huwezi kuongea na kampuni mmoja tu halafu ukapata mkataba mzuri. Leo hii Raisi Samia akiongea na nchi nyingine ma mashirika tofauti hao wawekezaji wenyewe wata sign mkataba haraka sana.
 
Tukubaliane tusikubaliane Rais Samia kashakubali mradi wa Bagamoyo kwa masharti aliyoyakataa Magufuli na ambayo Kikwete aliyakubali. Kwa hivi sasa ni kiini macho kinafanyika. Watatumwa watu kimbelembele kuendesha mazungumzo.
Masharti gani hayo ? Wewe umeyaona ?

Sababu nadhani sio busara kuamini tu maneno kutoka kwenye kinywa cha mtu (mwanasiasa) ukizingatia kudanganya kwao ni desturi; nina uhakika hata wewe ushamsikia akidanganya (sasa kama alidangaya pale kwanini asidanganye hapa)
 
Kwa ushauri wajenge hiyo bandari pale kisesa,mwanza
🤣🤣🏃🏃🏃
 
hata tukisema alikuwa karukwa na akili,hoja yake ya kupanua bandari zilizopo badala ya hiyo vipi!!!

ukiwa mtu timamu sifa ya kwanza usikubali kila jibu,lakini pia usikatae kila jibu,bali chambua kwa utulivu.

2013 wakati rais wa china amekuja bongo,walisign na jk mikataba 14,ambayo sio wewe wala mimi tunaujua hata mmoja.lakini wote tunajua bandari wanaoitaka ni wachina,je si miongoni mwa ile mikataba 14 iliyosainiwa???hakuna nayejua.

basi haya tufanye magufuli alidanganya kama mnavyosema,nini hatma ya bandari ya tanga,mtwara na dsm baada ya hiyo kubwa kabisa kufunguliwa??

bahati tuliyokuwa nayo sisi watz kwa mchina ilikuwa moja,tayari tulikuwa tumemwona mchina anafanyaje kwa nchi alizofanya nazo biashara zikateleza.sasa sijui nini kinakuja,Mungu ibariki tz.

Ushauri wangu.

1. Tanga wa-specialize kwenye meli za mafuta.

2. Mtwara wa-specialize kwenye makaa ya mawe na chuma toka Liganga na mikoa ya kusini.

3. Bagamoyo wa-specialize kwenye transhipment. Wawe ni container port kama zilivyo Dubai, Djibouti,..

4. Dsm ibaki kama ilivyo kuwa ni multi-purpose port.

5. Katika MKATABA na Wachina hisa za TPA zisipungue 40%.
 
Baba bora na madhubuti sio yule anaejenga nyumba ya kifahari kwa pesa ya kulipa ada za shule za watoto wake, kununulia chakula cha familia.

Kiuhalisia baba yule alitegeneza baiskeli yake mbovu kwa kuchukua spea kutoka baiskeli nyingine iliyokuwa nzima inatembea. Amefufua mbovu akaua nzima. Kila sehemu ni kilio kwa gharama za Dodoma, chato, ndege, meli, reli na madaraja.

..Magufuli alikosea sana kutumia fedha nyingi kujenga Dodoma, na kununua ndege.
 
Hakuna Cha akili, huwezi kusikiliza upande mmoja ukahitimisha. Lazima tuangalie pande zote. Kama huo mkataba ungewekwa wazi kila mtu akaona ndipo tungechambua mbovu na nzima. Kwa sasa huwezi kutoa maoni kwa upande mmoja. Wakati utakapofika tutajua.
When....?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini unamwamini Magufuli? Hao wote hawana akili ila yeye tu? Subiri mambo yakae sawa. Hakuna aliyeuona mkataba halisi.
Magu alikua mdanganyifu wa mambo mengi sana but kwenye issue ya Bagamoyo, kinacho wazuia watu kusema leo kwamba Magu alidanganya ni nini? Kukaa kwao kimya kuhusu yale matamshi ya MAgu kuhusu Bagamoyo harbor kunasababisha sie wengine kuhisi kwamba huenda mwendazake alikua sahihi.
 
Baba bora na madhubuti sio yule anaejenga nyumba ya kifahari kwa pesa ya kulipa ada za shule za watoto wake, kununulia chakula cha familia.

Kiuhalisia baba yule alitegeneza baiskeli yake mbovu kwa kuchukua spea kutoka baiskeli nyingine iliyokuwa nzima inatembea. Amefufua mbovu akaua nzima. Kila sehemu ni kilio kwa gharama za Dodoma, chato, ndege, meli, reli na madaraja.
[emoji2][emoji1][emoji3][emoji3]
 
Ushauri wangu.

1. Tanga wa-specialize kwenye meli za mafuta.

2. Mtwara wa-specialize kwenye makaa ya mawe na chuma toka Liganga na mikoa ya kusini.

3. Bagamoyo wa-specialize kwenye transhipment. Wawe ni container port kama zilivyo Dubai, Djibouti,..

4. Dsm ibaki kama ilivyo kuwa ni multi-purpose port.

5. Katika MKATABA na Wachina hisa za TPA zisipungue 40%.

hakuna mtu asiyependa mwisho mwema katika hili,maana ni faida kwa wote.

kinachotutatiza wengine ni wasi wasi wa uaminifu kwenye hili jambo,$ 10 bln ni pesa nyingi mno,ambazo kuleta faida kwa mwekezaji sio swala la siku mbili,hasa kama ataruhusu opp katika bandari nyingine,je yuko tayari!!!ndipo maswala ya maiaka 100 yapoibuka.

wacha tuone mwisho wa hili,tutakuja wasimulia wajukuu zetu namna tulivyokuwa tunashauri na hatukusikilizwa.
 
Hakuna Cha akili, huwezi kusikiliza upande mmoja ukahitimisha. Lazima tuangalie pande zote. Kama huo mkataba ungewekwa wazi kila mtu akaona ndipo tungechambua mbovu na nzima. Kwa sasa huwezi kutoa maoni kwa upande mmoja. Wakati utakapofika tutajua.
uelekeo wa sa100 kwa kikwete ndo unawatia watu wasi wasi, amemuelekea mtu alieingia mikataba mingi mibovu kwa maslahi yake binafsi na hapa ndo tatizo kubwa linaanzia
 
Haha Samia aaipoweka wazi mikataba ya hii miradi hawezi kuongea akaaminika
 
Kwa nini unamwamini Magufuli? Hao wote hawana akili ila yeye tu? Subiri mambo yakae sawa. Hakuna aliyeuona mkataba halisi.
Ninakubaliana nawe kwa swali ulilouliza hapo mwanzo; ila sijui ni akina nani unaowasema kwa "Hao wote hawana akili ila yeye tu?"

Kama una maana ya Mama Samia, swali lile lile ulilouliza mwanzo linaweza kuulizwa pia kwa Samia. Kama amedhamiria kuuza mradi kwa wachina, hayo ya mazungumzo ni gheresha tu!

Matumaini yako ya "mambo yakae sawa" huna uhakika nayo.

Na bado "mkataba halisi" hutauona!
 
Tufanye hana akili, lakini kaongea vitu vyenye akili, tusivipuuze, tuvitazame vizuri kwa ajili yetu na siyo kwa ajili ya magufuli unayemdhania ni mjinga
Tatizo Mwendazake alikuwa muongo kiasi kwamba si rahisi kumuamini.
 
uelekeo wa sa100 kwa kikwete ndo unawatia watu wasi wasi, amemuelekea mtu alieingia mikataba mingi mibovu kwa maslahi yake binafsi na hapa ndo tatizo kubwa linaanzia
Mikataba mingi mibovu! Taja 2 tu! Kisha meka hapa jamvini tuione sio bla!bla tu!
 
Ili kuweka mambo sawa ni muda sasa serikali kuwa na transparency hasa kwenye mikataba muhimu yenye maslai kwa taifa na sio mkata mmoja tu bali hata ya madini nk
Sasa huo uwazi utatoka wapi wakati wanaodai katiba mpya mnawaona wajinga?!!yaani huo mkataba wa bandari ndio umewauma sana watu, utadhania ndio mkataba pekee ambao umefichwa?!!hiyo ya ndege iko wapi, ya sgr, bwawa la umeme, na miradi minginr yote inayojengwa.
 
Back
Top Bottom