Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona wakati wa kuwapokea aliwapokea kirahisi tu bila hata kuthibitisha kwenye vyama vyao na wala kuomba sijui mihutasari, katiba wala viambatanisho vyovyote. Alikuwa amedhamiria kuitenda hiyo dhambi kwa maelekezo ya mwendazake. Lakini sasa anaona aibu anashindwa kuwatoa kwa vifungu vidogo tu vya sheria ambavyo hata spika wa zamani Pius Msekwa aliwahi kusema kwamba hao wabunge 19 kama wamefukuzwa na vyama vyao wanakuwa disqualified, taratibu za wao kurudi ndio inabidi wakazitafute mahakamani au kwenye rufaa ya Baraza Kuu.Kihalali jana kidogo ndugai nilimuelewa, Nikweli kua hawezi kuamua mtu moja au wawili kua huyu hatumtaki kwenye chama. Alicho kisema ni kua lazima waonyeshe procedures zilizofuatwa hadi kufikia uamuzi huo. Ni vikao kadhaa vilikaa kwa mujibu wa katiba yetu na viliazimia kuwafuta uanachama wanachama wetu hawa kwa kuwa wametenda makosa haya mbona ni kitu kirahisi tu?
unapoteza muda bure tu ungeanza kujiuliza hawa COVID19 wamewezaje kuingia mjengoni nani alimwandikia barua nduGAYe awapokee hao COVID19Ni kweli Spika Ndugai ana 'Mapungufu' yake, ila na Mimi GENTAMYCINE sasa taratibu naanza kuona pia kuna Matatizo ya 'Kimsingi' kwa upande wa Wapinzani ( hasa CHADEMA ) juu ya madai yao ama kwa Serikali au kwa Chama Tawala ( CCM )
Ushauri wangu tu Kwenu Marafiki zangu wa 'Kidemokrasia' nchini Tanzania CHADEMA kama Spika Ndugai kasema 'andiko' mlilompelekea ni 'Kipeperushi' basi nawaombeni mno anzeni Kujipanga hasa 'Kihoja' mnapojiandaa kwenda kukutana na Rais Samia katika Siku mtakayopangiwa ili baada ya kuonana nae asije kuwaita 'Wapuuzi' kwa yale mtakayoyawasilisha Kwake ambayo mmeyapania kweli kweli.
Kwa aina ya Uzungumzaji ule wa Spika Ndugai na ukiiangalia na 'body language' yake ( tena huku akijiamini kabisa ) tusifichane hapa ni lazima tu kutakuwa na Shida Kubwa ya 'Kiutendaji' kwa CHADEMA ila 'inafichwa' ama 'inafunikwa' tu kwa Mgongo wa Mapungufu ya Serikali na Chama Tawala chake cha CCM.
Ni wakati sasa wa Watu Makini ( Waelewa ) kuacha sana Kumshutumu Spika Ndugai 'Kimazoea' au kwa 'Kumkariri' na sasa tugeuke 'Kuwakosoa' hawa CHADEMA ili mwisho wa Siku tutende Haki kwa wote na tusijiingize katika 'Dhambi' ya kuja Kuitwa Wanafiki, Waongo na Wazushi tu wa Masuala.
CHADEMA anzeni 'Kujitathmini' haraka.
Saccos gani ambayo kipindi cha uchaguzi mkuu ukifika mnaangaika na vyombo vya dola na matamko ya vitisho hadi mnazima mitandao yakijamii?.Huna unachokijua wewe zaidi yakukaririshwa.Hicho chama hakina tofauti na saccos
Tutakaokuelewa hapa ni Sisi 'Brainiacs' wachache na Watu ambao tuko 'Neutral' katika Siasa za Tanzania, ila 'Imbeciles' na 'Hypocrites' wengi kamwe hawatokuelewa Mkuu.Hapa ndio naona pointi muhimu.
Chukulia mfano huu.
Mdee na jirani yake Mbowe wanagombania shamba.
Mbowe amekwenda mahakamani, na mahakama imetoa hukumu kwamba mdee hana haki katika shamba huisika.
Lakini, Mdee amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Baada ya rufaa hiyo kukatwa, Mbowe hawezi kuingia katika shamba linalobishaniwa na kuanza kulima wakati rufaa haijaamuliwa.
Katika mfano huu, uanachama wa wanaoitwa covid19 ndio shamba linagombaniwa. Wamekata rufaa.
Kitendo cha Chadema kuandika barua kwa Spika wakitaka awatimue ni sawa na kuingia kwenye shamba lililokatiwa rufaa na kuanza kulima.
Lakini, baadhi ya viongozi wa Chadema hawaoni umantiki huu. Sio sawa.
Kwa hiyo, mpaka hapo Spika Ndugai yuko upande sahihi, Chadema wako upande wa makosa.
Nashangaa hata mshauri wa kiroho wa Mbowe, ambaye ni PhD holder haoni ukweli huu.
Meseji zake anazozisambaza katika mitandao ya whatsapp zinathibitisha hitimisho hili.
Nimeona meseji moja imesindikizwa na picha ya kuku jike aliyeatamia "vifaranga wawili wenye sura ya paka."
Meseji nyingine inasindikizwa na picha ya muumini akiwa anatubu dhambi kwa kuhani.
Kosa la muumini ni "Father, yesterday I beat up a politician".
Na jawabu na mwendesha kutubio ni: "Confess your sins, not the good deeds."
Mitandao ya kijamii inaonyesha kwamba mwandishi wa meseji hizi ni Askofu Benson Kalikawe Lwalinda Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, mkoani Kagera.
Anachokifanya Askofu Ganonza ni kitendo cha disinformation by spinning.
Kuhusu neno spinning, namaanisha dhana hii:
"In public relations and politics, spin is a form of propaganda, achieved through knowingly providing a biased interpretation of an event or campaigning to influence public opinion about some organization or public figure."--Wikipedia.
Ushauri kwa timu Mbowe:
"Mshauri wako akikwambia jambo la kipumbavu ukalikubali na kulitekeleza, wakati anajua kwamba hilo ni jambo la kipumbavu, na akiwa anafahamu kwamba wewe unayeshauriwa unafahamu fika kwamba jambo hilo ni suala la kipumbavu, atakudharau kwa sababu ya namna unavyofikiri, kuamua na kutenda"--J.K. Nyerere.
Na mie naanza kukuelewa kuwa unamlalamikia muogaji anaemfukuza mwehu aliyechukua taulo lake.Taratibu naanza sasa Kumuelewa Spika.
Mie nilidhani jaji wa mahakama ndo anahitaji dondoo zote hizo. Ama kweli kuwa uyaone.Hata mimi sijawahi kuona duniani, ina maana hamuamini Katibu Mkuu wa Chadema? Haamini kama walikaa vikao? Ya nini kuomba viambatanisho vyoote hivyo wakati kinachotakiwa ni barua tu! Au na barua nyingine za kiofisi ni lazima kila kitu kiwe na viambatanisho kama ripoti?
Huo ndo ukweli.Bunge lina watumishi hewa 19.Mkuu Joka, kuna sehemu tatu za suala la Spika na Team Halima
1. Kwa wenye kumbu kumbu, Spika Mkwawa, Msekwa, Mang'enya, Sitta walikuwa na kauli za kiutu uzima
Kwa miaka ya karibuni na hasa mitano iliyopita kumekuwa na kauli za indhara na karaha kutoka kwenye kiti kile kile cha akina Mkwawa na Sitta .
2. Haihitaji ujuzi wa sheria kujua kwamba anachofanya Spika ni uvunjaji wa sheria.
Akiwa mkuu wa mhimili unaotunga sheria hili nalo linakera sana.
Mbunge akifukuzwa na chama chake kama ilivyokuwa kwa Sophia Simba automatic anapoteza Ubunge.
Ndivyo ilivyotokea siku zote, leo kwanini kwa Team Halima sheria ivurugwe na Spika?
3. Chadema kuna tatizo la kushughulikia Halima na Wenzake.
Siyo kazi ya Chadema kuamuru au kutaka wafukuzwe Bungeni.
Sheria ndiyo inayotaka hivyo na wala si wajibu wa Chadema kuiongelea , ni hisani tu.
Wanachotakiwa Chadema ni kumtaka Spika, na kwavile kuna barua na ushahidi , basi kupitia Mwanasheria wao amwandikie Spika akimtaka asitise kutumia jina la Chadema kwa wabunge hao, na kwamba wasihusishwe kwa jina au chochote kile. Na kwamba, ikitokea hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwemo kutafuta tafsiri ya mahakama
Chadema wanaweza kwenda mahakamani, si kutaka wafukuzwe Bungeni bali kuwataka Wabunge hao, Spika na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutohusisha, jina au shughuli zozote zile za chama na hao Wabunge. Hilo tu !
4. Si suala la Chadema kupinga uwepo wa Wabunge, bali ni suala la Walipa kodi kumtaka Spika asitishe malipo kwavile kufanya hivyo ni malipo yasiyo halali kama findings zingine katika audit.
Hili jamani si suala la Chadema, ni suala la wananchi kuhakikisha sheria zinafuatwa na kwamba hakuna abuse ya sheria zinazotuongoza wala hakuna aliye juu yake na kwamba, kodi zetu zinatumika kwa mujibu wa sheria zilizopo na si mtu au watu.
Hapa ndipo Watanzania wanatakiwa waamke, kodi zinazowalipa hao Wabunge si za Chadema ni za kwako wewe, mimi na yule.
Pascal Mayalla Ngongo
Naona anawatetea sijui kunanini.Huo ndo ukweli.Bunge lina watumishi hewa 19.
Daah!Huyu ndiyo Kakuzalisha wale Mapacha?
Duu hata wewe unaweza "kupeperushwa" na ngonjera za subwoofer kweli?! You can only ignore CDM at your own peril! Sio kwa CDM kukosa au kujenga hoja hata kidogo!Ni kweli Spika Ndugai ana 'Mapungufu' yake, ila na Mimi GENTAMYCINE sasa taratibu naanza kuona pia kuna Matatizo ya 'Kimsingi' kwa upande wa Wapinzani ( hasa CHADEMA ) juu ya madai yao ama kwa Serikali au kwa Chama Tawala ( CCM )
Ushauri wangu tu Kwenu Marafiki zangu wa 'Kidemokrasia' nchini Tanzania CHADEMA kama Spika Ndugai kasema 'andiko' mlilompelekea ni 'Kipeperushi' basi nawaombeni mno anzeni Kujipanga hasa 'Kihoja' mnapojiandaa kwenda kukutana na Rais Samia katika Siku mtakayopangiwa ili baada ya kuonana nae asije kuwaita 'Wapuuzi' kwa yale mtakayoyawasilisha Kwake ambayo mmeyapania kweli kweli.
Kwa aina ya Uzungumzaji ule wa Spika Ndugai na ukiiangalia na 'body language' yake ( tena huku akijiamini kabisa ) tusifichane hapa ni lazima tu kutakuwa na Shida Kubwa ya 'Kiutendaji' kwa CHADEMA ila 'inafichwa' ama 'inafunikwa' tu kwa Mgongo wa Mapungufu ya Serikali na Chama Tawala chake cha CCM.
Ni wakati sasa wa Watu Makini ( Waelewa ) kuacha sana Kumshutumu Spika Ndugai 'Kimazoea' au kwa 'Kumkariri' na sasa tugeuke 'Kuwakosoa' hawa CHADEMA ili mwisho wa Siku tutende Haki kwa wote na tusijiingize katika 'Dhambi' ya kuja Kuitwa Wanafiki, Waongo na Wazushi tu wa Masuala.
CHADEMA anzeni 'Kujitathmini' haraka.
UMSAJO ndio nini mkuu!Kuna 'Usamjo' mkubwa upo CHADEMA.
Utapeli Utapeli / Ujanja Ujanja wa sana.UMSAJO ndio nini mkuu!
Utakuwa mumoja wao, au unatabili tu?Wamegomea katiba mpya, wamegomea tume huru ya uchaguzi, huko mbeleni naona kutaibuka makundi ya kigaidi, yataanza mdogo mdogo, Kama vikundi vya kidini, lakini vikibeba madai ya kisiasa.
CCM haitoki madarakani kilaini
Kwa sasa kuna haja ya kutafuta watu timilifu ili waikomboe CDM. Waliopo ni makanjanja na watu waliopoteza dira na muelekeo kabisa.Utapeli Utapeli / Ujanja Ujanja wa sana.
KIGOGO 2014 ndio suluhisho la mgogoro kati ya CDM na wabunge wateule 19Ni kweli Spika Ndugai ana 'Mapungufu' yake, ila na Mimi GENTAMYCINE sasa taratibu naanza kuona pia kuna Matatizo ya 'Kimsingi' kwa upande wa Wapinzani ( hasa CHADEMA ) juu ya madai yao ama kwa Serikali au kwa Chama Tawala ( CCM )
Ushauri wangu tu Kwenu Marafiki zangu wa 'Kidemokrasia' nchini Tanzania CHADEMA kama Spika Ndugai kasema 'andiko' mlilompelekea ni 'Kipeperushi' basi nawaombeni mno anzeni Kujipanga hasa 'Kihoja' mnapojiandaa kwenda kukutana na Rais Samia katika Siku mtakayopangiwa ili baada ya kuonana nae asije kuwaita 'Wapuuzi' kwa yale mtakayoyawasilisha Kwake ambayo mmeyapania kweli kweli.
Kwa aina ya Uzungumzaji ule wa Spika Ndugai na ukiiangalia na 'body language' yake ( tena huku akijiamini kabisa ) tusifichane hapa ni lazima tu kutakuwa na Shida Kubwa ya 'Kiutendaji' kwa CHADEMA ila 'inafichwa' ama 'inafunikwa' tu kwa Mgongo wa Mapungufu ya Serikali na Chama Tawala chake cha CCM.
Ni wakati sasa wa Watu Makini ( Waelewa ) kuacha sana Kumshutumu Spika Ndugai 'Kimazoea' au kwa 'Kumkariri' na sasa tugeuke 'Kuwakosoa' hawa CHADEMA ili mwisho wa Siku tutende Haki kwa wote na tusijiingize katika 'Dhambi' ya kuja Kuitwa Wanafiki, Waongo na Wazushi tu wa Masuala.
CHADEMA anzeni 'Kujitathmini' haraka.
Waliteuliwa na nani?Chadema hawakuwateua hao wabunge