Biblia imetuasa kuheshimu mamlaka za nchi ..Sasa kama atutaki kuheshimu mamlaka lazma tutalipa gharama. Naona sasa tunataka kubariki siasa za udini kwenye nchi yetu.
Usiwe kasuku wa kukariri ili kuulinda uovu. Biblia haisomwi kama kitabu cha hadithi. Usisome mstari mmoja na kuanza kupiga kelele kuwa umeijua biblia.
Nenda kasome tena biblia, ukaone ni mara ngapi manabii wa Mungu walitoa maonyo makali kwa wafalme, na wafalme waliokaidi wakapokea adhabu ya Mungu? Unataka kusema hao manabii wa Mungu walikiuka maagizo ya Mungu kwa kuwaeleza watawala uovu wao? Baadhi ya maelekezo ya kwenye biblia, ni specific kwa events zilizokuwa zikiendelea mahali na wakati fulani. Yaani agizo lilitolewa kwa sababu kulikuwa na tukio fulani, na agizo lilitolewa kuhusiana na tukio hilo. Umewahi pia kuona kwanye biblia, imeandikwa kuwa wanawake muiingiapo hekaluni fumbeni vinywa vyenu, kaeni kimya, msinene chochote? Je, ni kweli wanawake hawatakiwi kunena chochote hekaluni. Kama ni mtaalamu wa maandiko unajua kabisa kuwa ujumbe ule haikukusudiwa kwa makanisa yote, bali lile lilikuwa ni agizo specific kwa kanisa la mahali pale kutokana na vitendo vya wanawake walipokuwa wamepewa nafasi ya uongozi ndani ya kanisa, wakaamini kuwa sasa wao wamekuwa bora zaidi kuliko wanaume. Mtume alipopewa taarifa hiyo, akawazuia wanawake wale kuendelea na uongozi katika kanisa lile.
NB: Utawala unaotenda uovu unatakiwa kuonywa na watu wa Mungu. Mkristo hustahili kuunga mkono kwa namna yoyote ile utawala ambao unajua kuwa ni dhalimu, unaodhulumu haki za binadamu wenzako au zako mwenyewe.