Kama biashara zilikufa na kufungwa miaka 5 iliyopita, hizi faida za mabenki zilitoka wapi?

Kama biashara zilikufa na kufungwa miaka 5 iliyopita, hizi faida za mabenki zilitoka wapi?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Ukikaa na kusikiliza watu unaweza kufikiri Tanzania ilisimama kwa miaka 5 na hakuna kilichofanyika lakini uchumi unaongea tofauti.

Bank ya crdb imetoa taarifa ya faida kwa miaka 5 iliyopita, faida imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 300.

2018 Bilioni 64
2019 Bilioni 120
2020 Bilioni 165
2021 Bilioni 268

Hizi za NMB.
2021 Bilioni 291
2020 Bilioni 210
2019 Bilioni 144
2018 Bilioni 100.

Kipindi kile cha Magufuli watu wakawa wanasema anapika dataz benki zinalazimishwa kupika data ila sasa hivi sisikii hizo hadithi.

Unajiuliza kama biashara zilikua zimekufa na kufungwa, banki hizo faida zimetoa wapi?

Faida ya benki inatokana na biashara za mikopo. Sasa kama biashara zimekufa, banki zilikua zinakopesha majini na kutengeneza faida?

 
Zile zilikua propaganda za wezi mkuu waliminywa mno.

Kwa sasa wanajiachia hivyo hutasikia kelele za aina yeyote ile.

Mfano mwingine ni exports mwaka 2019 zilikua juu sana ila kwa sasa zimeshuka lakini hawa majangili hawatalizungumzia hilo.

Exports mwaka 2019 zilifikia dola bilioni 9.7 pato la juu kabisa katika historia ya Taifa letu.

Ila hao majamaa maongo maongo hayatasema.
 
2025 mgombea Urais wa Chadema ni Sukuma gang wenye chama wameshaamua!
Mmh! Thubutu. Mwenyekiti Mbowe ndiye wa kwanza kuulaani utawala wa jiwe. Ndiye aliyehutubia taifa kwa kusema "Never and Never Again".
. Upo hapo ewe sukuma gang?
 
Mmh! Thubutu. Mwenyekiti Mbowe ndiye wa kwanza kuulaani utawala wa jiwe. Ndiye aliyehutubia taifa kwa kusema "Never and Never Again".
. Upo hapo ewe sukuma gang?
Hata kwa Lowassa Ilikuwa hivyo hivyo mlibana mwisho " kimnyelamomo" kikachanika kidume laigwanani kikazama Ufipa

Mchagga haachagi hela popote pale duniani
 
hutaki kuamini kama Jiwe aliua biashara?
Wafanyabiashara wengi walikua hawalipi kodi stahiki na mapato mengi ya nchi yalikua yanaingia mifukoni mwa watu badala ya hazina.

Kuziba mianya hiyo inatarajiwa kabisa kuwa wahusika wasingefurahia na hawakufurahia wala kumpenda.

Wezi wana nguvu sana ingawa ni wachache.
 
Back
Top Bottom