Ushawahi kumuona Mbwa akiwa anazaa? Mimi nimewahi muona Mbwa akiwa anazaa Mbwa halii hapigi makelele na kutapatapa ila sura yake inakua na huzuni, hakuna anaemsaidia Mbwa kuzaa zaidi ya kujizalisha mwenyewe na kuwaokoa watoto wasife kwa kukosa pumzi anapowatoa ndani ya placenta mbwa anao uwezo wa kuzaa watoto mpaka 10 na humchukua masaa mengi mpaka kuhakikisha watoto wote wamezaliwa salama bila msaada wa kiumbe mwingine yoyote bila kupiga kelele bila kuonyesha shida yoyote na anapomaliza watoto wanaanza kunyonya maziwa mara moja bila ya kujali kwamba Mama yao amechoka au la na hua na kazi ya kuwapa joto wasife na baridi
Binadamu kwanza anahitaji msaada pindi anahitaji kuzaa na huzaa kwa tabu sana hulia sana kwa maumivu makali mno pindi anapojifungua na uhitaji msaada ili asije akaiharibu njia yake ya uzazi na hapo ndipo uchungu unapoingia
Subiri kwanza wewe unahitaji maelezo mengi ili kichwa chako kielewe nitakupeleka chumba kujifungua wajawazito ujionee nini kinachotokea binadamu sio mbuzi au ng'ombe, ng'ombe anapozaa huangaika tu na kiumbe chake kikiwa kinamtoka huku akijisaidia mwenyewe bila kuhitaji msaada wowote mpaka kiumbe kinatoka na kua kiumbe hai sio sawa na mwanadamu, mwanadamu anapitia mateso kipindi hicho cha kuzaa mtoto sio kipindi cha kuzaa tu kipindi chote cha kubeba mimba mpaka anajifungua ni kipindi cha kuishi kwa mateso na uchungu anashindwa kulalia tumbo yeye ni kulalia mgongo tu muda wote maana akilalia tumbo kaua kiumbe na ndio maana wengi wakishajifungua wanakua na matatizo ya mgongo kwa kipindi fulani sasa huo ndio uchungu wenyewe usimfanishe binadamu na paka hata kidogo