Kama binadamu kuzaa kwa uchungu ni adhabu vipi kuhusu ng'ombe, mbuzi, nguruwe na wanyama wengine wanaozaa kwa uchungu?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
17,119
Reaction score
32,195
Wadau na waamini wa biblia na Korani nina swali kwetu

Hivyo vitabu vinasema Mungu alimpa mwanamke adhabu ya kuzaa kwa uchungu sababu ya kufanya dhambi ya kula tunda la mti wa kati katika bustani ya Eden

Naulizia vipi kuhusu wanyama wengine ambao nao wanazaa kwa uchungu, walifanya kosa gani?
Tunaona dhahiri wanyama jamii ya mamalia karibu wote wanazaa kwa uchungu kama binadamu.

Mfano Simba, fisi, chui, mbwa, mbwea, ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, farasi na ngamia.
Hivi vitabu vyetu vimeacha maswali mengi sana yanayo hitaji majibu ili tuviamini pasi na shaka.

Mtazamo wangu:
Naamini Mungu yupo na binadamu ameumbwa na Mungu.

Naamini dini na vitabu vyake kuna mengi ya kutunga kwa lengo la kuwatisha binadamu au kuwapa faraja au kuhamasisha.

Hakuna pepo wala motoni sijui jehanamu.

Naamini matendo ya uongo, wizi, uuwaji, tamaa mbaya ni dhambi kwa mukutadha wa maadili na kuwafanya watu waishi vizuri bila misukosuko.

Uasherati na uzinzi dhambi sababu ya kuepusha migogoro ya familia na maradhi yaambukizayo kwa ngono.

Kiufupi dhambi ni chochote kibaya kwa maisha ya binadamu au ustawi wa jamii na siyo sababu Mungu amekataza. Mungu ametuumba ametuacha huru kwa kila jambo.

The choice is ours.

Nasisitiza hayo juu ni IMANI YANGU TU. Siyo yaliyo thibitika pasi na shaka kisayansi au kidini au kifalsafa.
Karibuni tujadili.
 
Wadau na waamini wa biblia na Korani nina swali kwetu.
Hivyo vitabu vinasema Mungu alimpa mwanamke adhabu ya kuzaa kwa uchungu sababu ya kufanya dhambi ya kula tunda la mti wa kati katika bustani ya Eden.
Naulizia vipi kuhusu wanyama wengine ambao nao wanazaa kwa uchungu, walifanya kosa gani?
Tunaona dhahiri wanyama jamii ya mamalia karibu wote wanazaa kwa uchungu kama binadamu.
Mfano Simba, fisi, chui, mbwa, mbwea, ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, farasi na ngamia.
Hivi vitabu vyetu vimeacha maswali mengi sana yanayo hitaji majibu ili tuviamini pasi na shaka.
Mtazamo wangu: Naamini Mungu yupo na binadamu ameumbwa na Mungu.
Naamini dini na vitabu vyake kuna mengi ya kutunga kwa lengo la kuwatisha binadamu au kuwapa faraja au kuhamasisha.
Hakuna pepo wala motoni sijui jehanamu.
Naamini uongo, wizi, uuwaji, tamaa mabya ni dhambi kwa mutabdha wa maadili na kuwafanya watu waishi vizuri bila misukosuko.
Uasherati na uzinzi dhambi sababu ya kuepusha migogoro ya familia na maradhi yaambukizayo kwa ngono.

Kiufupi dhambi ni chochote kibaya kwa maisha ya binadamu au ustawi wa jamii na siyo sababu Mungu amekataza. Mungu ametuumba ametuacha huru kwa kila jambo. The choice is ours.
Nasisitiza hayo juu ni IMANI YANGU TU. Siyo yaliyo thibitika pasi na shaka kisayansi au kidini au kifalsafa.
Karibuni tujadili.
Mkuu, kumbe na wewe umeshajiuliza hilo swali, hahaha 😂.

Vitabu vitakatifi vinaporojo sana.

Ngoja Pulchra Animo: aje na utetezi wake.
 
Tena fisi inasemekana anazaa kwa uchungu kupita binadamu
Yes.
Kama ulikuwa akilini kwangu wakati naandika.
Nilikumbuka habari ya fisi.
Nasikia jike anazaa kupitia uke ambao unafanana na uume kwa maumbile. Hivyo njia nyembamba Sana.
Wakati fulani fisi wanakufa au kuumia vibaya sana wakati wa kuzaa.
 
Yes.
Kama ulikuwa akilini kwangu wakati naandika.
Nilikumbuka habari ya fisi.
Nasikia jike anazaa kupitia uke ambao unafanana na uume kwa maumbile. Hivyo njia nyembamba Sana.
Wakati fulani fisi wanakufa au kutumia vibaya sana wakati wa kuzaa.
Wana theologia wanachenga sana hili swali wakidai ni lugha ya ki theologia zaidi, hivi vitabu vina ujanja mwingi wakutoroka maswali magumu.
 
Wanyama wanafyatua watoto kirahisi, tulipokuwa watoto wadogo tuliona wanakunya watoto. Mkao wa binadamu anapotoa mtoto ni shughuli pevu mtu anaweza kunya kinyesi wakati wa kujikakamua mtoto atoke kwenye njia ya uzazi, ile tunaiita mbunye, mbususu a.k.a K. Kwa binadamu ni uchungu, kwa wanyama ni kama kunya tu!
 
Wadau na waamini wa biblia na Korani nina swali kwetu.
Hivyo vitabu vinasema Mungu alimpa mwanamke adhabu ya kuzaa kwa uchungu sababu ya kufanya dhambi ya kula tunda la mti wa kati katika bustani ya Eden.
Naulizia vipi kuhusu wanyama wengine ambao nao wanazaa kwa uchungu, walifanya kosa gani?
Tunaona dhahiri wanyama jamii ya mamalia karibu wote wanazaa kwa uchungu kama binadamu.
Mfano Simba, fisi, chui, mbwa, mbwea, ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, farasi na ngamia.
Hivi vitabu vyetu vimeacha maswali mengi sana yanayo hitaji majibu ili tuviamini pasi na shaka.

Mtazamo wangu:
Naamini Mungu yupo na binadamu ameumbwa na Mungu.
Naamini dini na vitabu vyake kuna mengi ya kutunga kwa lengo la kuwatisha binadamu au kuwapa faraja au kuhamasisha.
Hakuna pepo wala motoni sijui jehanamu.
Naamini matendo ya uongo, wizi, uuwaji, tamaa mbaya ni dhambi kwa mutabdha wa maadili na kuwafanya watu waishi vizuri bila misukosuko.
Uasherati na uzinzi dhambi sababu ya kuepusha migogoro ya familia na maradhi yaambukizayo kwa ngono.

Kiufupi dhambi ni chochote kibaya kwa maisha ya binadamu au ustawi wa jamii na siyo sababu Mungu amekataza. Mungu ametuumba ametuacha huru kwa kila jambo. The choice is ours.
Nasisitiza hayo juu ni IMANI YANGU TU. Siyo yaliyo thibitika pasi na shaka kisayansi au kidini au kifalsafa.
Karibuni tujadili.
Ni sayansi ya kawaida ya mwili ingawa mazwazwa ya dini yaliitumia kutokana na kutojua kuwahadaa waumini. Hata wadudu hutaga mayai kwa uchungu.
 
Back
Top Bottom