hoja yako nataka niikubali kwa sababu haijadispute wazo napendekeza kwako. haya unayoyasema yanawezekanaje? yanawezekana kwa sababu tunayo inherent weakness. nataka nipendekeze kwamba hiyo inherent weakness SI uwezo wa kufikiri. Bali kwamba tunao uwezo mkubwa wa kufikiri, isipokuwa katika maumbile yetu ipo anti-dote ya fikra endelevu, ambayo ni selfishness.
mwaka 1964 nadhani ilikuwa ile, au pengine 1963, nikiwa mdogo lakini naweza kukumbuka matukio ya wakati huo, nilikuwa naumwa. tumetoka nyumbani na mama yangu mzazi kwenda kwa tabibu. yule mzee hakuwahi kusoma mahala popote kuhusu acupuncture au mbinu nyingine wanatumia binadamu wengine. tumefika pake, mama naye alikuwa na matatizo yake. yule mzee alichukua kipande cha pembe ya ng'ombe yapata nchi nne za pembe ule upande wa juu. kule kwenye ncha ya pembe kulikuwa na nta yenye rangi nyeusi hivi. alichemsha maji, akaosha sehemu ya mgongoni kwangu palipokuwa panauma, akanikanda kidogo kwa namna ya kusafisha kwa majani fulani, kisha akachanja chale hapo. hadi hii leo chale hizo zipo hapo kiunoni kwangu. yule tabibu akachukua kitu chenye ncha kali akaweka kishimo upande wa juu wa ile pembe ya ng'ombe kupitia kwenye ile nta halaf nikaamriwa kuinama fulani hivi. baadae aliweka ile pembe hapo kwenye chale na kunyonya hadi ile pembe ikashika pale kwa kutumia nguvu ya pumzi ambayo imezuiwa kutoka baada ya yeye kuziba kile kishimo. hii ilikuwa njia ya kusafisha damu kwa kuondoa damu chafu. nilipona.
Leo hii waganga wa muhimbili na kwingineko wanakamua majibu kama kwamba sisi hatukuwahi kujua hayo. nani anakwambia hatuna akili? Wazungu wanagundua kitu, wanashea ujuzi, kizazi kinachofuata kinaboresha ujuzi ule ndo maana leo hii tuna cd players badala ya gramophone, tuna flash disc badala ya floppy. Ndiyo maana leo tuna magari badala ya matoroli. Wanashea knowledge ili kizazi cha baadae kijue pa kuanzia.
Ubinafsi unatuzuwia waafrika kuongeza ujuzi. Wazungu wanasaidia mtoto mwenye kipaji hata kama si mtoto wako. Sisi mtoto mwenye kipaji anatafutiwa sumu afe. Tatizo la mtu mweusi ni ubinafsi--siyo uwezo wa kufikiri.
nikubaliane nawe kwamba tunalo tatizo la kukubali kila kitu kimesemwa na mzungu. hata kama ni upuuzi. na ukitaka kujua hilo angali tatizo la Zimbabwe.
Mugabe hana kosa kutaka wazungu wagawe ardhi yao. labda si kuchukua yote, lakini kugawa ardhi ile equitably hapakuwa na kosa kabisa katika fikra ile. ni taifa gani la kiafrika limejitokeza kumsaidia mugape? kinyume chake hii miafrika imekubaliana na wazungu eti zimbambwe hakuna demokrasia. aliyekwambia demokrasia ndo jibu la kila tatizo nani? si kila anachosema mzungu ni sawa. Mengine wanayasema kulinda maslahi yao ya miaka hamsini ijayo.