Kama Bucha za nyamapori zimeruhusiwa, kwanini Pembe za ndovu zenye thamani ya bilioni 186 zisiuswe?

Soma makala hii ya mwaka 2018 unaweza kupata mwanga The Sunk Cost Fallacy

Mapambano dhidi ya biashara ya pembe za ndovu​

Jamii Africa
Jamii Africa

4 years ago​
Baada ya China kufunga biashara ya pembe za ndovu, mtandao wa watumiaji wa teknolojia duniani wameungana kukomesha biashara hiyo haramu na bidhaa zake inayofanyika mtandaoni.
Hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za mashirika ya kimataifa na Serikali ikiwemo ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili wa Tembo ambao wako katika hatari ya kutoweka kabisa duniani .
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016 unakadiria kuwa mpaka sasa kuna Tembo 352,000 ambapo idadi hiyo imepungua kutoka milioni 1.3 mwaka 1979. Takwimu za sensa ya Tembo zinaeleza kuwa idadi ya Tembo barani Afrika imepungua kwa 30% kati ya mwaka 2007 na 2014. Tanzania nayo imekumbwa na anguko kubwa la idadi ya Tembo ambapo inakadiriwa kuwa wamepungua kwa 80%.
Kundi la wafanyabiashara ya mtandao, teknolojia na mitandao ya kijamii duniani watashirikiana na shirika la uhifadhi wa wanyamapori (WWF), Shirika la kimataifa la usafiri na Mfuko wa kimataifa wa Masuala ya wanyamapori (Ifaw).
Lengo la mtandao huo wa kutokomeza biashara ya wanyamapori ni kuzuia na kupunguza biashara hiyo kwenye majukwaa ya intaneti kwa asilimia 80 ifikapo 2020 na kuhakikisha biashara ya mtandao haihujumiwi na majangili na wafanyabiashara wasiofuata taratibu za kimataifa.
Kupitia mtandao huo utatengenezwa mfumo wa data za mienendo ya wanyamapori kwenye hifadhi, biashara ya bidhaa za tembo. Pia miongozo na taratibu za kufuata katika biashara ya wanyamapori inayofanyika mtandaoni ili kuepusha majangiri na watu wasio na nia njema kutumia teknolojia kufanya uhalifu dhidi ya wanyamapori.
online-coalition-820.jpg
Mashirika na makampuni yaliyojiunga na mtandao huo ni Mall for Afrika, eBay, Alibaba, Etsy, Baidu, Baixing, Huaxia Collection, Qyer, Kuaishou, Pinterest, Ruby Lane, Shengshi Collection, Tencent, Wen Wan Tian Xia, Zhongyikupai, Zhuanzhuan, 58 Group, Google na Microsoft.
Katika orodha hiyo utagundua kuna kampuni nyingi kutoka China, sababu kubwa ni kuwa kampuni hizo zinaunga mkono juhudi za Serikali ya nchi yao ambayo imepiga marufuku na kufunga biashara yoyote inayohusika na bidhaa za pembe za ndovu.
Kila kampuni itatengeneza na kutekeleza sera na mikakati yake ili kusaidia kukomesha biashara ya wanyamapori mtandaoni kwa kushirikiana na WWF na Ifaw; mashirika ambayo yanasimamia na kudhibiti biashara ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa WWF, Cawford Allan amesema wahalifu na majangili wanaua na kuuza wanyamapori na bidhaa zake kwasababu hakuna sera za pamoja kwenye mtandao wa intaneti.
“Kukosekana kwa chombo cha pamoja kunatengeneza tatizo. Haya makampuni yameona tatizo na wameungana kuhakikisha intaneti haitumiwi vibaya na wafanyabiashara haramu”, alisema Allan.
Kinachoendelea Tanzania
Serikali kwa kushirikiana na WWF, Machi mwaka huu walizindua kampeni ya kuwavalisha tembo kola ili kuhakikisha tembo waliobaki wanalindwa dhidi ya majangiri katika hifadhi za taifa.
Kampeni hiyo itaanza kutekelezwa kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Selous, ambayo kwa miaka 40 iliyopita imepoteza asilimia 90 ya tembo wote wanaopatikana Tanzania. Kampeni hiyo itawasaidia askari wa wanyamapori kukabiliana na majangiri na kuhakikisha idadi ya tembo inaongezeka katika hifadhi za taifa.
WhatsApp-Image-2018-04-13-at-11.16.18.jpeg
Tembo aliyevalishwa kola maalum kufuatilia mienendo yake

Mradi huo ambao utatekelezwa kwa miezi 12 ambapo tembo 60 katika hifadhi ya Selous watafungwa kola shingoni. Hatua hiyo itawawezesha wasimamizi wa hifadhi kufuatilia mienendo ya tembo, kubaini na kukabiliana na hatari yoyote dhidi ya wanyama hao.
Kola hizo zitaunganishwa na mfumo wa ‘satellite’ ikiwa ni njia iliyohakikiwa na wanasayansi katika kufuatilia mienendo na ulinzi wa Tembo. Kabla ya Tembo kuvalishwa kola maalumu anapewa dawa ya usingizi na kuchukuliwa taarifa zake za kiafya. Atafuatiliwa kokote aendako na ikiwa atakabiliwa na hatari, askari watajitokeza mara moja kumsaidia.
Kwa miaka 40 iliyopita ujangili wa Tembo katika hifadhi ya Selous ilichochewa na biashara ya pembe za ndovu ambazo zilikuwa zinahitajika sana katika bara la Asia hasa nchini China. Inakadiriwa idadi ya Tembo katika pori hilo ilishuka kutoka 110,000 hadi 15,200.
Mwaka 2014, Shirika la Elimu na Utamaduni (UNESCO) liliiweka Selous katika orodha ya urithi wa dunia ambao uko katika hatari ya kutoweka kwasababu ya matukio yasiyo ya kawaida ya ujangiri wa tembo
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Serikali ya Tanzania imetunza na kuhifadhia shehena ya pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 186.

Shehena hii imekamatwa kutoka kwa majangili kwa miaka mingi Sasa ila imewekwa tuu bila sababu zenye mashiko kwa kisingizio cha kulinda uhifadhi na kwamba kuuza ni kuhamasisha ujangili.

Sidhani kama hii ni hoja yenye mashiko ikiwa Serikali inatuhusu uwindaji wa Wanyamapori kibiashara na imeanzisha mabucha ya nyama pori mikoa mbalimbali.

Sasa tumekaa na mali ya mabilioni yote hayo kwa sababu zipi hasa?

Naishauri Serikali iuze hizo pembe za ndovu na pesa itakayopatikana itumike kuunda Mamlaka Maalumu ya Uhifadhi na Fidia kwa wanaoathiriwa na Wanyamapori kwa kuuwawa na wanyama ama kuharibiwa kwa Mazao yao.

Nchi ya Zimbabwe imetangaza kuuza shehena yake kwa ajili ya kupata pesa za uhifadhi na mambo mengine, Tanzania tunakwama wapi?

View attachment 2245762
 
Ndio ujinga gani umeleta hapa? Jikite kwenye hoja
 
Tembo wamekuwa wakiharibu mazao ya wakulima na juzi kati wameua watu, kama vipi ikitokea tembo wamefanya tukio baya basi pembe kadhaa zilizopo stoo ziuzwe kufidia uharibifu waliofanya......hii ni katika kutimiza ule usemi wa 'ukinizingua, nakuzingua.....'
 
Huo ni wehu.Kuchoma moto kunazuiaje ujangili?

Uchome pesa wakati una mahitaji kwenye jamii zinazopakana na Hifadh..

Itakuwa akili au matope?
Mkuu ungejua gharama za kiulinzi na uhifadhi wake unavyozigharimu hizi nchi, ni mala mia hata kuyachoma moto, na ni zaidi ya miaka 20, unatunza tu kitu, na hujui kama huko mbeleni hiyo biashara itaruhusiwa tena, na jinsi mambo yanavyoonekana sidhani kama itakuja kutokea kuruhusiwa tena.Na ndio maana baadhi ya nchi walishaamua kuyachoma moto tu.
Huwezi kuziita pesa wakati kuzi convert, ili ziwe pesa ni ngumu na inategemea watu wengine ndio wakupe ruhusa, na wakati huo huo zinazidi kukugharimu kuzitunza!!!
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Serikali ya Tanzania imetunza na kuhifadhia shehena ya pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 186.

Shehena hii imekamatwa kutoka kwa majangili kwa miaka mingi Sasa ila imewekwa tuu bila sababu zenye mashiko kwa kisingizio cha kulinda uhifadhi na kwamba kuuza ni kuhamasisha ujangili.

Sidhani kama hii ni hoja yenye mashiko ikiwa Serikali inatuhusu uwindaji wa Wanyamapori kibiashara na imeanzisha mabucha ya nyama pori mikoa mbalimbali.

Sasa tumekaa na mali ya mabilioni yote hayo kwa sababu zipi hasa?

Naishauri Serikali iuze hizo pembe za ndovu na pesa itakayopatikana itumike kuunda Mamlaka Maalumu ya Uhifadhi na Fidia kwa wanaoathiriwa na Wanyamapori kwa kuuwawa na wanyama ama kuharibiwa kwa Mazao yao.

Nchi ya Zimbabwe imetangaza kuuza shehena yake kwa ajili ya kupata pesa za uhifadhi na mambo mengine, Tanzania tunakwama wapi?

View attachment 2245762
Kwani hata zikiuzwa kipi kitabadilika kwenye maisha yako?
 
Jangili akiona hii picha si anachanganyikiwa?
 
Soma makala hii ya mwaka 2018 unaweza kupata mwanga The Sunk Cost Fallacy

Mapambano dhidi ya biashara ya pembe za ndovu​

Jamii Africa
Jamii Africa

4 years ago​
Baada ya China kufunga biashara ya pembe za ndovu, mtandao wa watumiaji wa teknolojia duniani wameungana kukomesha biashara hiyo haramu na bidhaa zake inayofanyika mtandaoni.
Hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za mashirika ya kimataifa na Serikali ikiwemo ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili wa Tembo ambao wako katika hatari ya kutoweka kabisa duniani .
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016 unakadiria kuwa mpaka sasa kuna Tembo 352,000 ambapo idadi hiyo imepungua kutoka milioni 1.3 mwaka 1979. Takwimu za sensa ya Tembo zinaeleza kuwa idadi ya Tembo barani Afrika imepungua kwa 30% kati ya mwaka 2007 na 2014. Tanzania nayo imekumbwa na anguko kubwa la idadi ya Tembo ambapo inakadiriwa kuwa wamepungua kwa 80%.
Kundi la wafanyabiashara ya mtandao, teknolojia na mitandao ya kijamii duniani watashirikiana na shirika la uhifadhi wa wanyamapori (WWF), Shirika la kimataifa la usafiri na Mfuko wa kimataifa wa Masuala ya wanyamapori (Ifaw).
Lengo la mtandao huo wa kutokomeza biashara ya wanyamapori ni kuzuia na kupunguza biashara hiyo kwenye majukwaa ya intaneti kwa asilimia 80 ifikapo 2020 na kuhakikisha biashara ya mtandao haihujumiwi na majangili na wafanyabiashara wasiofuata taratibu za kimataifa.
Kupitia mtandao huo utatengenezwa mfumo wa data za mienendo ya wanyamapori kwenye hifadhi, biashara ya bidhaa za tembo. Pia miongozo na taratibu za kufuata katika biashara ya wanyamapori inayofanyika mtandaoni ili kuepusha majangiri na watu wasio na nia njema kutumia teknolojia kufanya uhalifu dhidi ya wanyamapori.

online-coalition-820.jpg
​
Mashirika na makampuni yaliyojiunga na mtandao huo ni Mall for Afrika, eBay, Alibaba, Etsy, Baidu, Baixing, Huaxia Collection, Qyer, Kuaishou, Pinterest, Ruby Lane, Shengshi Collection, Tencent, Wen Wan Tian Xia, Zhongyikupai, Zhuanzhuan, 58 Group, Google na Microsoft.
Katika orodha hiyo utagundua kuna kampuni nyingi kutoka China, sababu kubwa ni kuwa kampuni hizo zinaunga mkono juhudi za Serikali ya nchi yao ambayo imepiga marufuku na kufunga biashara yoyote inayohusika na bidhaa za pembe za ndovu.
Kila kampuni itatengeneza na kutekeleza sera na mikakati yake ili kusaidia kukomesha biashara ya wanyamapori mtandaoni kwa kushirikiana na WWF na Ifaw; mashirika ambayo yanasimamia na kudhibiti biashara ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa WWF, Cawford Allan amesema wahalifu na majangili wanaua na kuuza wanyamapori na bidhaa zake kwasababu hakuna sera za pamoja kwenye mtandao wa intaneti.
“Kukosekana kwa chombo cha pamoja kunatengeneza tatizo. Haya makampuni yameona tatizo na wameungana kuhakikisha intaneti haitumiwi vibaya na wafanyabiashara haramu”, alisema Allan.
Kinachoendelea Tanzania
Serikali kwa kushirikiana na WWF, Machi mwaka huu walizindua kampeni ya kuwavalisha tembo kola ili kuhakikisha tembo waliobaki wanalindwa dhidi ya majangiri katika hifadhi za taifa.
Kampeni hiyo itaanza kutekelezwa kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Selous, ambayo kwa miaka 40 iliyopita imepoteza asilimia 90 ya tembo wote wanaopatikana Tanzania. Kampeni hiyo itawasaidia askari wa wanyamapori kukabiliana na majangiri na kuhakikisha idadi ya tembo inaongezeka katika hifadhi za taifa.

WhatsApp-Image-2018-04-13-at-11.16.18.jpeg
​
Tembo aliyevalishwa kola maalum kufuatilia mienendo yake

Mradi huo ambao utatekelezwa kwa miezi 12 ambapo tembo 60 katika hifadhi ya Selous watafungwa kola shingoni. Hatua hiyo itawawezesha wasimamizi wa hifadhi kufuatilia mienendo ya tembo, kubaini na kukabiliana na hatari yoyote dhidi ya wanyama hao.
Kola hizo zitaunganishwa na mfumo wa ‘satellite’ ikiwa ni njia iliyohakikiwa na wanasayansi katika kufuatilia mienendo na ulinzi wa Tembo. Kabla ya Tembo kuvalishwa kola maalumu anapewa dawa ya usingizi na kuchukuliwa taarifa zake za kiafya. Atafuatiliwa kokote aendako na ikiwa atakabiliwa na hatari, askari watajitokeza mara moja kumsaidia.
Kwa miaka 40 iliyopita ujangili wa Tembo katika hifadhi ya Selous ilichochewa na biashara ya pembe za ndovu ambazo zilikuwa zinahitajika sana katika bara la Asia hasa nchini China. Inakadiriwa idadi ya Tembo katika pori hilo ilishuka kutoka 110,000 hadi 15,200.
Mwaka 2014, Shirika la Elimu na Utamaduni (UNESCO) liliiweka Selous katika orodha ya urithi wa dunia ambao uko katika hatari ya kutoweka kwasababu ya matukio yasiyo ya kawaida ya ujangiri wa tembo
Sijawahi kupinga uhifadhi bali hoja yangu ni kwamba tayari kuna maelfu ya Tani za pembe za ndovu zilizoko stoo ambazo zilikamatwa kutoka kwa Majangili..

Kuna haja gani ya kukaa nazo wakati zinaweza kuuzwa na pesa kusaidia kwenye uhifadhi?

Kwa hiyo haya mauaji kwako ni sawa? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220603-131339.png
    Screenshot_20220603-131339.png
    83.5 KB · Views: 15
Sijawahi kupinga uhifadhi bali hoja yangu ni kwamba tayari kuna maelfu ya Tani za pembe za ndovu zilizoko stoo ambazo zilikamatwa kutoka kwa Majangili..

Kuna haja gani ya kukaa nazo wakati zinaweza kuuzwa na pesa kusaidia kwenye uhifadhi?

Kwa hiyo haya mauaji kwako ni sawa? 👇
Kibali cha kuuza mpaka watoe UN au one of UN Agencies. Tena hupigiwa kura na nchi wanachama
 
Ndio kwa Hali ya Sasa ni lazima watoe ndio maana Nchi huwa inafanya ushawishi kwa kujenga hoja na kueleza kwa nini wanataka kuuza na pesa zitafanya nini...

Zimbabwe inafanya hiyo kampeni saizi na Tzn itaiunga mkono.

Mwisho Serikali za Kiafrika zinatakiwa kuwa na mipango yao ya Uhifadhi bila kutegemea Wazungu.
 
Kama Serikali imeruhusu mauzo ya wanyama hai,inakuaje mshindwe kuuza stock za pembe za ndovu?👇
 
Attachments

  • IMG-20220604-WA0046.jpg
    IMG-20220604-WA0046.jpg
    79.3 KB · Views: 16
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Serikali ya Tanzania imetunza na kuhifadhia shehena ya pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 186.

Shehena hii imekamatwa kutoka kwa majangili kwa miaka mingi Sasa ila imewekwa tuu bila sababu zenye mashiko kwa kisingizio cha kulinda uhifadhi na kwamba kuuza ni kuhamasisha ujangili.

Sidhani kama hii ni hoja yenye mashiko ikiwa Serikali inatuhusu uwindaji wa Wanyamapori kibiashara na imeanzisha mabucha ya nyama pori mikoa mbalimbali.

Sasa tumekaa na mali ya mabilioni yote hayo kwa sababu zipi hasa?

Naishauri Serikali iuze hizo pembe za ndovu na pesa itakayopatikana itumike kuunda Mamlaka Maalumu ya Uhifadhi na Fidia kwa wanaoathiriwa na Wanyamapori kwa kuuwawa na wanyama ama kuharibiwa kwa Mazao yao.

Nchi ya Zimbabwe imetangaza kuuza shehena yake kwa ajili ya kupata pesa za uhifadhi na mambo mengine, Tanzania tunakwama wapi?

View attachment 2245762
Mkuu ulitakiwa ujue ya kwamba kuna makubaliano ya kidunia ya kuwalinda tembo duniani. Mojawapo ya makubaliano hayo ni kutouza au kununua pembe za ndovu kutoka nchi yoyote. Lengo ni kuwafanya majangili kukosa soko nakuacha kuwaua.

Makubaliano mengine ni kuziteketeza kwa kuzichoma moto pembe za ndovu zinazopatikana katika nchi husika.

Tanzania tumeheshimu makubaliano ya kutouza, lakini bado tumeshindwa kuzichoma moto pembe hizo za ndovu. Kenya na Afrika Kusini waliishawahi kuzichoma pembe za ndovu katika kuheshimu makubaliano. Tanzania nasi tufanye hivyo sasa.
 
Yapo lakini kuna procedures za kufuata na kuuza
 
Back
Top Bottom