Kama Bunge lingevunjwa jana, leo ilikuwa ni majonzi makubwa kwa CHADEMA


 
Huyo kijana uliyemzungushia alama na picha ya chini akiwa na Jembe a.k.a Jiwe aliwahi kuwa mwanafunzi wangu wangu katika harakati zake za kutafuta elimu. Ni hazina kubwa sana kwa CCM na Taifa.
 
JPM hana muda wa kudeal na Cdm. Anadeal na mambo makubwa kama ujenzi wa JNHPP ,Sgr,Hospital n.k

Hata wazungu wa Afrika kusini walijenga miradi mikubwa maradufu ya hii unayoibabaikia leo, lakini pia waliwahujumu akina Mandela na weusi wengine. Huenda unadhani ukisema anadeal na hiyo miundombinu, ndio utakuwa umetoa utetezi wa hizo hujuma za wazi.
 
Toa mifano hai nani kafungwa bila kosa kama Mandela? Nani Amepigwa risasi barabarani bila kosa?
 
Toa mifano hai nani kafungwa bila kosa kama Mandela? Nani Amepigwa risasi barabarani bila kosa?

Kwa taarifa yako hata Mandela alifungwa kwa makosa kama unachozungumzia ni makosa, ila ni makosa ya aina gani na yalikuwa na shinikizo gani hapo ndio ilipo hoja. Hawa cdm wanafungwa kwa makosa, ila ni makosa yenye utashi wa watawala walioko madarakani, kama ilivyokuwa kwa Mandela. Hayo ya kupigwa risasi hadharani bila kosa mbona yako wazi. Au hayo nayo mpaka utajiwe? Hapa naona unazidiwa na hoja, au lengo lako ni huu uzi uliouanzisha uwe na page nyingi?
 
Ili kumaliza mjadala na page zisiwe nyingi wataje hao wanaCdm waliofungwa bila kosa. Na waliopigwa risasi wataje.
 
Ili kumaliza mjadala na page zisiwe nyingi wataje hao wanaCdm waliofungwa bila kosa. Na waliopigwa risasi wataje.

Viongozi wa juu wa cdm, na Tundu Lissu kwa shambulio la risasi. Hii ni mifano michache ya dhahiri.
 
Wahame abaki Mbowe muone miujiza watu watakavyomiminika kuchukua fomu chadema.
 
Viongozi wa juu wa cdm, na Tundu Lissu kwa shambulio la risasi. Hii ni mifano michache ya dhahiri.
Lissu alipigwa na Chadema ushahidi anao Dk Godwin Mollel. Viongozi wa Cdm walifanya mkusanyiko usio halali. Pia walifanya vurugu. Je marehemu Chacha Wangwe nani alimuua?
 
Lissu alipigwa na Chadema ushahidi anao Dk Godwin Mollel. Viongozi wa Cdm walifanya mkusanyiko usio halali. Pia walifanya vurugu. Je marehemu Chacha Wangwe nani alimuua?

Shambulio la Lissu liko wazi sana hata asiyejua lolote anajua nini kiliendelea. Ndio maana nakuambia hata Mandela alifungwa kwa amri ya makaburu kwa kuwapinga, na kufanya mikusanyiko isiyo halali. Kesi ya marehemu chacha Wangwe iliendeshwa kwenye mahakama hizi hizi ambazo zinatii maagizo ya ccm, na kama hukuridhika na maamuzi ya mahakama za ccm, jinai haina mwisho, unaruhusiwa kwenda kwenye hizo mahakama kufungua kesi tena, ili upate hukumu itakayoendana na hiyo propaganda mfu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…